Ameniambia "Hujanijua vizuri eh"

MAKWAZO niloyaona kwa uzi wako ni haya: TAFADHARI=TAFADHALI
MAHALI= MAHARI

Kwingine nimekuelewa na nakushauri uachane mapema kabla hujamjua vizuri kama alivokueleza bt hayo MAKWAZO ya juu yafanyie kazi pulizi
 
Wakuu wasalaam!
Bila shaka hamjambo,kwa wenye changamoto poleni!

Wakuu nina miezi 8 kwenye mahusiano ila nimeanza kuishi nae miezi 4 iliyopita, ni binti 26 yrs mimi nina 33 yrs.

Issue kubwa amekuwa na kauli za kibabe sana kiasi zimenifanya kila mwezi na postpone kupeleka mahali kwao kwa sababu hatua za mwanzo nilishafanya.

Kila nikiwaza kupeleka mahali na haya maneno nayopewa na wife moyo unasita.

Nimekuwa na ni kawaida yangu kusaidia majukumu ya home kama kuchota maji, kupika hasa akiwa zake kazini maana mimi nawahi kurudi toka job, mimi ni mfanyakazi wa shirika (jina linahifadhiwa) na kazi ndogo ndogo mara moja moja nafanya, ndivyo tulivyolelewa home lakini siku akikuta sijafanya anafoka kana kwamba ni sehemu ya majukumu yangu ya lazima, nampenda na namhudumia kama baba wa nyumba.

Mfano; leo tumezinguana kwa issue ndogo lakini kanambia nanukuu "hujanijua vizuri kumbe"

Nimeongea nae sana kumsihi abadilike lakini naona bado, nimeshirikisha Dada yake lakini bado, nachowaza kwa sasa ni kukaa kijeshi tu, nikae kibabe nisimjali kiufupi kila mtu awe kimpango wake!

Na zaidi naona nazidi kupata moto kutopeleka mahali naona kama hatutadumu na huyu bibie, sijajua kinachompa jeuri, historia yake kwa ndugu zake inaonekana ana kiasili cha hii tabia, mimi nina asili ya upole lakini ni mkorofi nikichoka kuvumilia.

Issue ni nyingi naomba kuweka haya ya mhimu zaidi,kama una cha kunishauri mwanaume mwenzangu karibu, na wewe mwanamke toa neno tafadhari.

Naomba radhi kama kuna makwazo kwenye uzi huu!
We utaanzaje kuchota maji, kupika kwani ni mgonjwa.Ni hivi kuanzia leo ukiondoka ukiulizwa unarudi saa ngapi,sema saa moja afu ibuka home saa sita usiku,nguo zikianikwa nje hata mvua ikinyesha usianue jifanye ulisahau,ukila acha vyombo kwenye sinki hata ikipita siku mbili havijaoshwa usiviguse,akipiga simu kukuuliza unarudi saa ngapi mwambie narudi baada ya nusu saa afu unarudi masaa manne baadaye.Cha mwisho mtie mimba.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom