Amefufuka kweli? Au maneno tu!

Jana nikuwa jijini Mwanza nikapita viwanja vya furahisha nikaona matangazo na maandalizi ya mahubiri yatakayoanza j'tano. Kilichonivutia ni kwamba nikaona picha ya binti anayedaiwa kuwa alikufa na sasa amefufuka kwa maombi. Nauliza, hizi habari ni kweli au ni uzushi tu?
sasa wewe c ndo umeona tangazo nadhani ungeenda kwenye uwo mkutano ukashuhudie mwenyewe.
 
acheni bhanaa. cku hz biashara matangazo. juz tu hapa nilikuwa nasafiri kwa basi akaingia kijana anajiita mtumishi then akaanza kuhubiri injili ya vitisho. yan kama vle abiria tujiandae maana kifo ni popote, na ajali ni nje nje,hvyo anaombea safari ye2. baadae akaomba sadaka, basi wamama wakampa kwa wingi maana walikuwa wameogopa sana. jamaa akashuka, mbele kdogo akapanda jamaa mwingine na stori zle zle, tukaduwaa!
 
kama ni anasema amefufuliwa na binadamu mwenzie, hapo siwezi amini, ila kama amefufuliwa na Mungu tatizo lipo wapi hapo? Kwani Mungu hawezi kufufua wafu?
 
Haya ni maneno ya watu wasiomjua MUNGU wa kweli. Kwani kuna jambo lolote la kumshinda MUNGU? Yote yanawezekana kwake aaminiye na MUNGU hufanya jambo kwa utukufu wake.
<br />
<br />
Mungu hashindwi na lolote. Nauliza hivi kwani huyo mlokole aliyemfufua mtu ni Mungu au binadamu wa kawaida. Watanzania tuamke na hizi dini za uongo.
 
Mambo ya imani ni magunu sana na tukianza kuyajadili hatutapata ufumbuzi cha kufanya ni kila mtu kwa nafsi yake kumwamini Mungu kwa roho na kweli na kufata maandiko neno la Mungu linasemaje na kulisoma kwa bidii na kulielewa siyo kupotoshwa na watu wengine. Swala la Mungu kufufua mtu ni dogo kwake sana ukiamini anaweza kutenda makubwa zaidi ya hayo ila cha kujiuliza anatenda katika mazingira gani?
 
Lakini hii ya mwanza ni dili siyo kweli hawa kina malisa wote ni wahubiri wa uongo,wamepata utaalam toka nigeria hata wewe ukitaka address niko nayo nikuunganishe,but jiandae kutoa kafara
 
hata kwenye dini wanafanya marketing ... duh .... invitation to treat
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom