Amefufuka kweli? Au maneno tu!

Stevemike

Senior Member
Joined
Mar 12, 2011
Messages
117
Points
195

Stevemike

Senior Member
Joined Mar 12, 2011
117 195
Jana nikuwa jijini Mwanza nikapita viwanja vya furahisha nikaona matangazo na maandalizi ya mahubiri yatakayoanza j'tano. Kilichonivutia ni kwamba nikaona picha ya binti anayedaiwa kuwa alikufa na sasa amefufuka kwa maombi. Nauliza, hizi habari ni kweli au ni uzushi tu?
 

Anold

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2010
Messages
1,447
Points
1,500

Anold

JF-Expert Member
Joined Jul 15, 2010
1,447 1,500
Jana nikuwa jijini Mwanza nikapita viwanja vya furahisha nikaona matangazo na maandalizi ya mahubiri yatakayoanza j'tano. Kilichonivutia ni kwamba nikaona picha ya binti anayedaiwa kuwa alikufa na sasa amefufuka kwa maombi. Nauliza, hizi habari ni kweli au ni uzushi tu?
Mkuu utatusaidia sana kama utafuatilia mambo hayo kwa kina kwa vyovyote itabidi waeleze ni hospitali ipi alifia, alizikwa wapi na cheti cha kifo kionyeshe. Hata hivyo ni makosa makubwa kujaribu kutumia kigezo cha miujiza kuwahamashisha watu, Mungu anataka moyo wa hiari, ndiyo maana Bwana Yesu alionya vikali dhidi ya kizazi hiki kinachotafuta miujiza hilo sio fundisho la Kanisa la Yesu.

Mbinu hiyo inatumiwa na watu wenye nia ya kukusanya watu kwenye mikutano wakiwa na nia na dhamira tofauti ambayo mara nyingi watu wanaokusanywa hawaijui. na idadi kubwa ya wakusanywa ni wanawake!!!
 

CLEMENCY

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2008
Messages
211
Points
195

CLEMENCY

JF-Expert Member
Joined Feb 4, 2008
211 195
Ndugu,
Mambo ya imani huwezi kuhoji. Amini na kusadiki. Kinyume na cha hapo na wewe kufa ili ukaulize kama kweli alifika huko! Kisha rudi humu humu JF utupe habari. Walahi tutasadiki.
Heading itakuwa "EXCLUSIVE: Mwana JF aamua kufa kwenda kuchukua ushahidi na kufufuka"
 

CHUAKACHARA

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2011
Messages
12,374
Points
2,000

CHUAKACHARA

JF-Expert Member
Joined Jun 3, 2011
12,374 2,000
Jana nikuwa jijini Mwanza nikapita viwanja vya furahisha nikaona matangazo na maandalizi ya mahubiri yatakayoanza j'tano. Kilichonivutia ni kwamba nikaona picha ya binti anayedaiwa kuwa alikufa na sasa amefufuka kwa maombi. Nauliza, hizi habari ni kweli au ni uzushi tu?
Wahuni hao, wanachukulia ujinga wa watanzania kuwa-fool in whatever way they like.
 

Katavi

Platinum Member
Joined
Aug 31, 2009
Messages
41,043
Points
2,000

Katavi

Platinum Member
Joined Aug 31, 2009
41,043 2,000
Kahudhurie hayo mahubiri hiyo jumatano, uje na ushahidi nadhani hapo utapata mengi kuhusiana na huyo aliyefufuka...
 

Angel Msoffe

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2011
Messages
6,794
Points
1,225

Angel Msoffe

JF-Expert Member
Joined Jun 21, 2011
6,794 1,225
jamani siwavunji moyo wakristo wenzangu ila hz dini za ck hz ni uongo na wizi m2pu, wanazusha mambo makubwa ili wapate waumini wawape sadaka, kwanini wawafufue watoka mbali wakati hata wao wamefiwa?? Huu ni uongo na wizi wa mchana kweuupee. MI CIAMINI KW M2 ANAWEZA KUFUFUA M2 MWINGNE.
 

Anold

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2010
Messages
1,447
Points
1,500

Anold

JF-Expert Member
Joined Jul 15, 2010
1,447 1,500
Ninachoamini mimi ni kuwa kama mtu amechukuliwa kwa njia ya kishirikina, maombi ya kweli yanaweza kufanya mtu huyo arudie kwenye hali yake. Sijajua vizuri watu hao waliofufua walienda kwenye kaburi kama Yesu alivyomfufua Razaro au ni kitu kingine, nafikiri kuna kuchanganya mambo ndiyo maana watu wanakuwa na hali ya kutoamini, ni vema haya mambo yajitosheleze kuliko kuyaacha yakitoa maswali. Mambo ya Imani yanaenda kwa imani lakini ni vizuri yakawekwa bayana ili kupunguza maswali. Pamoja na imani niliyonayo juu ya uwezo wa miujiza utokanao na uwezo wa kimungu nasita kuamini kuwa miujiza ni muhimu katika kumpenda Mungu, ila miujiza hutuimarisha kujua ukuu wa Mungu, ndiyo maana Bwana Yesu ilifika mahali akifanya Muujiza alikuwa akiwakataza wasitangaze. Shida ni Moja tu kuwa watu wanaanzisha huduma wakiwa na lengo zaidi ya moja, ndiyo maana tangazo la kuwaalika watu kupata uponyaji wakati mwingine halina tofauti na matangazo ya waganga wa kienyeji maana utasikia, wenye pepo mahaba, wenye kutaka vyeo, wenye kutaka kuolewa, wenye kutaka kumiliki magari waje waombewe what a shame!!!! Haya mambo yanahitaji umakini maana sidhani na sitaki kuamini kuwa Mungu anamipaka ya utendaji wake wa kazi. Imani hizi zinahitaji umakini mkubwa kabla hujazikubali.
 

Shenkalwa

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2011
Messages
580
Points
170

Shenkalwa

JF-Expert Member
Joined May 3, 2011
580 170
Rejea siku za mwisho. Maneno ya Mungu yako wazi kabisa: Watakuja mashahidi wa uongo, wengine mpaka watasema wao ndio Yesu, watu wenye kujipenda wenyewe, watu watapenda sana fedha..., wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana (Kama baadhi humu jf), wasiotii wazazi wao, wasiowapenda wakwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema, wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu, wenye mfano wa utauwa lakini wakikana nguvu zake. Ni budi kwa kila mmoja kuzipima nguvu zinazojitokeza nyakati hizi. Iwe ni katika ukristo au katika uislam. Mashetani na mapepo yanazidisha kasi ya kupingana na Mungu huku wakijitahidi kuonyesha kuwa wana uwezo ule ule alio nao Mungu. Nyakati hizi wamezuka wahubiri wa aina mbalimbali waliojipachika uaskofu, unabii, mitume, watu wenye upako nakadhalika. Ni vizuri kuzipima nguvu hizi kabla ya kuzishabikia kwa sababu zina vielelezo vyote vya dalili za kuwadia kwa siku za mwisho. Jambo la mtu kufa na kukufuliwa kwa njia yeyote lisingekuwa jambo la minong'ono bali lingekuwa ni jambo la mastaajabu na muujiza ambao ungepelekea watu kumininika kama walivyomiminika kwa babu wa loliondo ingawa kwa babu nako kuna maswali mengi ya kujiuliza yanayokosa majibu bado.
 

Forum statistics

Threads 1,382,081
Members 526,268
Posts 33,819,348
Top