Amechoka kunivumilia anataka kuniacha!

CHE Raptino

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
1,027
1,067
Wakuu habari za muda huu?

Naomba niwashirikishe hii changamoto tunayoipitia kati yangu mimi na mzazi mwenzangu!

Ni muda wa miaka sita tangu tulipofahamiana na mama wa mtoto wangu, maisha yetu yamekuwa ya furaha na amani.

Mwaka 2014 nilipata nafasi ya kujiunga shahada ya kwanza katika mojawapo ya vyuo mkoani mbeya, na hapo tatizo ndipo lilipoanzia.

Niliamua kwenda kujiendeleza kitaaluma ili kuongeza maarifa na ujuzi kwa lengo la kuandaa mazingira murua ya baadae. Niliamua kuomba ruhusa kwa mwajiri wangu katika mojawapo wa halmashauri katika mkoa wa Simiyu.

Mwajiri hakuridhia kunipa ruhusa japo nilikua na sifa na vigezo vinavyohitajika ili kupata kibari hicho.

Kwa kuwa nina malengo yangu nikaamua kwenda masomoni na kumuacha mama na mtoto sehemu tuliyokuwa tukiishi. Baada ya mabadiliko ya uongozi hapa kwetu nchini niliondolewa kwenye pay roll kwani taarifa zangu zilionesha sipo kazini. Hali hiyo ilisababisha kuyumba kiuchumi tangu April 2016 na kupelekea maisha yetu kuwa magumu.

Mzazi mwenzagu amevumilia kwa kipindi chote hicho na sasa anasema anataka kunipunguzia matatizo na mawazo kwa kuniacha niendelee na harakati zangu za kusaka maisha na yeye aendelee na shughuli zake huku akimlea mtoto. Nitakapokaa sawa atanipatia mwanangu.

Sasa wakuu naomba ushauri wenu nifanyaje kwani nampenda sana mama wa mwanangu si mpango wangu mwanangu kuja kulelewa na mama mwingine au baba mwingine.

N. B nimetoa mahari ila ndoa bado hatujafanikiwa kufunga.
 
Da! Pole sana. Itakuwa ameshapata chimbo jipya mahali. Usijiumize kwa kuwaza sana, we endelea na masomo utajua cha kufanya hapo baadaye.
 
Jaribu kutumia watu wakaribu kama wazaz ndugu zake waeleze yanayowasibu wajue jins yakumshaur mana kama umemlipia mahar huyo ni mkeo na ndoa nikukamilisha tuu, pia jaribu kuongea nae na mweleweshe kua unachokitafuta nikwafaida ya familia pengine kahis ukishapata kaz waweza mtelekeza ukaoa mwingine au kuna MTU ameshamdanganya hivyo chagua ww kama kichwa chafamilia unafanyeje
 
ruba siifahamu mkuu ni nini?
Mdudu hatari sana kwa kufyonza damu. Anaishi kwenye madimbwi ya maji. Akikushika haachii.
upload_2017-5-1_17-59-55.jpeg
 
Back
Top Bottom