Amechoka kunivumilia anataka kuniacha!

Amechoka kunivumilia anataka kuniacha!

Si wanawake tu hata wanaume wapo wengi tu, kaoa muda ana amua kujiendelea unavumilia akisha anza kupata kipato kikubwa ana anza usumbufu na kuona mke sio na kuanza dharau bila kumdhamini hivyo hilo tatizo lipo pande zote na michepuko inaongezeka
asee lakini wanaongoza wanawake
 
Kumbe mnavyosemaga amemganda kama ruba....ruba wenyewe hamuwafaham?
Ananyonya damu, hashikiki anateleza balaa. Anapenda madimbwi yenye tope yenye maji yaliyotulia. Sijawahi kusikia kama ana sumu.
Duuuuu mi sijawahi muona
 
Ukipata upendo toka kwa mumeo ukajihisi kweli napendwa ni rahisi kumvumilia kwa situations yoyote anapitia iwe kiuchumi,Maradhi n.k

Sijafahamu upande wako umempa sababu ya yeye kukuvumilia? ?
 
Ukipata upendo toka kwa mumeo ukajihisi kweli napendwa ni rahisi kumvumilia kwa situations yoyote anapitia iwe kiuchumi,Maradhi n.k

Sijafahamu upande wako umempa sababu ya yeye kukuvumilia? ?
Sababu za kunivumilia zipper kwa kuwa,

1.Maamuzi ya kujiendeleza tuliafikiana wote baada ya kutoridhika na maisha ya awali.

2. Anasema "najua unanipenda na una malengo mazuri na mimi, ila nimechoka kukuvumilia naona bora ufanye maisha yako na mimi yangu".
 
Sababu za kunivumilia zipper kwa kuwa,

1.Maamuzi ya kujiendeleza tuliafikiana wote baada ya kutoridhika na maisha ya awali.

2. Anasema "najua unanipenda na una malengo mazuri na mimi, ila nimechoka kukuvumilia naona bora ufanye maisha yako na mimi yangu".
Daaaa pole sana kama kweli anaelewa unampenda sana tu basi analake muache tu kulazimisha mambo sio vizuri
 
Daaaa pole sana kama kweli anaelewa unampenda sana tu basi analake muache tu kulazimisha mambo sio vizuri
Sawa dada Barbra.

Inaniuma Sana, nipo semester ya mwisho, nahangaika na research naye ameamua kuniongezea mzigo mwingine.

Anyway let me struggle. [emoji24]
 
Duuh ...pole mkuu

Lkn huyo mkeo mbona hajachukua maamuzi mbaya? Kaona akupunguzie mzigo...

Tunatofautiana uelewa na mtazamo
 
Anyway mapenzi ni demokrasia, nitampa uhuru, maisha ni darasa Tosha.

INANIUMA
 
Kama anaweza kutafuta kwa ajili ya mtoto, kwa nini hasikae mkaunganisha mnachokipata kidogo familia isonge

Let her go atakusumbua

Ukipata katika pitapita zako, mtumie pesa ya mtoto ya matumizi
 
Pole mkuu ,kwa kuwa umeishaamua kuanza shule jaribu kuongea nae mara ya mwisho na kama hatakuelewa huna budi kumuacha aendelee na anachokitaka.
 
Kwanza huyo hakuwa mkeo kabisa ila mtu mliyezaa naye tu, hakuona future yake kwako tangu mwanzo inawezekana umezidi kusingizia maisha sana hivyo ameona kuwa wewe huna muelekeo wowote ule zaidi ya jusubiria kisichoonekana.
Kama ungekuwa mwamaume wa nguvu ungeshamuoa kitambo hata kabla hujaenda sijui wapi huko kusoma. Mnapenda kupotezea muda watoto wa watu kwa kisingizio cha maisha, kama unajijua huwezi kuoa mpaka uunge unge maisha acheni kuwazalisha watoto wa watu halafu mnataka kuwalazimisha kuvumilia eti sijui maisha magumu.
Wanaume tumekuwa chanzo cha haya matatizo wenyewe, yaani mnataka wanawake wafanye mazoezi ya kuzoea shida tena wale ambao hata ndoa nao hamna, unafikiri wao hawana akili? Anajiuliza kama tangu tumezaa tumeshindwa kufunga ndoa halali ikitokea kesho kanigeuka itakuwaje wakati sina ndoa yoyote ? Lazima ajiongeze aisee, kama maisha magumu ishi mwenyewe ukijiweza oa na sio kutia mimba halafu baadae usingizie maisha ndio kikwazo eti uvumiliwe tena kwa muda usiojulikana.
Wanawake wamekuwa victims kwa visingizio hivi, mtu unakuta umeenda kusoma unarudi umemsahau binti wa watu kisa yeye mama wa nyumbani, hasa vijana wa kisasa wasiotaka majukumu kabisa, yaani wao wanataka wanawake wa kuwasaidia kimaisha tu na si vinginevyo sasa huyo kakuwahi kwa mbele kabla hujamuwahi. Kama kweli wewe una nia ya dhati nenda msikitini/kanisani kafunge ndoa acha makuu sijui kualika kijiji kizima uone kama atakimbia, lakini kama kila siku visingizio tu vya maisha aisee huyo binti ana akili sana kwani uvumilivu nao una kikomo chake, mwache aende akapumue na wewe utapata mwingine wa kula shida naye.
 
Back
Top Bottom