Amebadilika siku chache kabla ya mahari

Wewe dada nahisi nakufahamu lakini potelea mbali

Ni hivi kijana muoaji hawezi kuja hapo kubargain mahari, na baba yako anataka muoaji aongozane na Baba yake

Ambapo baba wa muoaji alifika na akaishia njiani kusubiri kama mtabadili mawazo na kumpokea sasa

Mzee kaamua kuondoka kwenda kuendeleza miradi yake na kasema Dunia imezaa hawawezi kosa mwanamke
 
Salaam kwenu nyote.

Ninaomba ushauri wenu kwenu Kaka zangu na Dada zangu. Mimi ni binti.

Nimekutana na changamoto katika mahusiano yangu. Kisa ni hiki.

Nilikuwa katika mahusiano na kijana mmoja kwa takriban miaka 4. Baadae ikaonekana ni vema tufahamishe mahusiano haya ngazi ya wazazi. Kijana alikuja nyumbani kwa tararibu zote na kupangiwa mahari. Wakati wote huo mimi na kijana tuko vizuri na mawasiliano kwa hakika yalikuwa mazuri mno. Naweza kusema hakukuwa na jambo au tatizo baina yetu na mwenzangu ambalo labda lingekuwa kikwazo.

Hata hivyo, week moja kabla kuelekea siku ya mahari mwenzangu alinifahamisha kwamba wamehairisha kuja nyumbani kwetu sababu familia yake imeona gharama walizopangiwa ni kubwa. Naye alishikilia msimamo kwamba anaungana na familia yake.. Nilijitahidi sana kumweleza kwamba waje na gharama walizojiandaa nazo lakini haikuwezekana tena kwa mwenzangu. Ni kama alishaamua kusitisha jambo hili na mahusiano yote kwa ujumla na kwa hivyo sikuweza kubadili chochote kutokea hapo.

Nimejitahidi mara kadhaa kutaka kujua iwapo kuna sababu nyingine ya sababu hiyo lakin mara zote mwenzangu amekuwa akijikita katika sababu tajwa hapo juu. Hata ninapomuuliza mwenzangu juu ya nini kinachoendelea mpka wakati huu bado hanipi majibu. Kimsingi, inaonekana hakuna mahusiano tena kwa sasa.

Ninaumia kwa namna mambo yalivyoenda na yalivyohitimishwa kwa namna isiyotarajika. ona ni kama ndoto, labda nipo ndotoni lakini ni ukweli ambao watu wanapitia. Nipo katika wakati mgumu mno, ukizingatia kwamba taarifa za jambo hili ziliwaslishwa kwa ndugu, jamaa na marafiki.

Nimekuja kwenu naomba ushauri, nahitajika kufanya nini ili niweze kuchukuliana na changamoto hii? Kuna wakati nashindwa kama binadamu naogopa kumfuru Mungu wangu. Nashindwa kusahau na namkumbuka sana kila wakati.
Dada hapo hujaelewa nini tena?
Unataka kuolewa na mtu asiyekuhitaji?
Kama umeshaona mahusiano yamevurugika na kijana hana mpango tena wa kutaka kuja kukuoa, maana yake hakuna tena ndoa. Usilazimishe sana akwambie kila sababu, vingine ni siri za moyo wake au siri za familia yake, usichimbe sana.

Nini ufanye sasa?
Jipange kutafuta mahusiano mapya na kijana mwingine, huyo sio wa kwako tena.

Note
Kama huyo kijana alishakupiga miti mara kadhaa, kuna uwezekano mkubwa sana ikawa ndio sababu ya kukuacha. Usiniulize kwa nini.
 
Wewe dada nahisi nakufahamu lakini potelea mbali
Ni hivi kijana muoaji hawezi kuja hapo kubargain mahari, na baba yako anataka muoaji aongozane na Baba yake,
Ambapo baba wa muoaji alifika na akaishia njiani kusubiri kama mtabadili mawazo na kumpokea sasa
Mzee kaamua kuondoka kwenda kuendeleza miradi yake na kasema Dunia imezaa hawawezi kosa mwanamke
Mungu akubaruki. Hili ni sawa na jambo usilolijua...
 
Dada hapo hujaelewa nini tena?
Unataka kuolewa na mtu asiyekuhitaji?
Kama umeshaona mahusiano yamevurugika na kijana hana mpango tena wa kutaka kuja kukuoa, maana yake hakuna tena ndoa. Usilazimishe sana akwambie kila sababu, vingine ni siri za moyo wake au siri za familia yake, usichimbe sana.

Nini ufanye sasa?
Jipange kutafuta mahusiano mapya na kijana mwingine, huyo sio wa kwako tena.

Note
Kama huyo kijana alishakupiga miti mara kadhaa, kuna uwezekano mkubwa sana ikawa ndio sababu ya kukuacha. Usiniulize kwa nini.
Shukrani. Point taken
 
Hitimisho hili limenifunza kwamba watu wanabadilika muda wowote Dada yangu. Huyu kijana huwezi kumdhania. Sikutegema kwamba tungefikia mwisho wa namna hii.
Hao ndio wanaume. Sasa tulia kabisa unaweza kuta alikuwa anawachanganya wote. Kwa sasa kubaliana na hiyo dissapointment but usikurupuke kuingia kwenye mahusiano mengine.

By the way mie ni kaka yako😜
 
Salaam kwenu nyote.

Ninaomba ushauri wenu kwenu Kaka zangu na Dada zangu. Mimi ni binti.

Nimekutana na changamoto katika mahusiano yangu. Kisa ni hiki.

Nilikuwa katika mahusiano na kijana mmoja kwa takriban miaka 4. Baadae ikaonekana ni vema tufahamishe mahusiano haya ngazi ya wazazi. Kijana alikuja nyumbani kwa tararibu zote na kupangiwa mahari. Wakati wote huo mimi na kijana tuko vizuri na mawasiliano kwa hakika yalikuwa mazuri mno. Naweza kusema hakukuwa na jambo au tatizo baina yetu na mwenzangu ambalo labda lingekuwa kikwazo.

Hata hivyo, week moja kabla kuelekea siku ya mahari mwenzangu alinifahamisha kwamba wamehairisha kuja nyumbani kwetu sababu familia yake imeona gharama walizopangiwa ni kubwa. Naye alishikilia msimamo kwamba anaungana na familia yake.. Nilijitahidi sana kumweleza kwamba waje na gharama walizojiandaa nazo lakini haikuwezekana tena kwa mwenzangu. Ni kama alishaamua kusitisha jambo hili na mahusiano yote kwa ujumla na kwa hivyo sikuweza kubadili chochote kutokea hapo.

Nimejitahidi mara kadhaa kutaka kujua iwapo kuna sababu nyingine ya sababu hiyo lakin mara zote mwenzangu amekuwa akijikita katika sababu tajwa hapo juu. Hata ninapomuuliza mwenzangu juu ya nini kinachoendelea mpka wakati huu bado hanipi majibu. Kimsingi, inaonekana hakuna mahusiano tena kwa sasa.

Ninaumia kwa namna mambo yalivyoenda na yalivyohitimishwa kwa namna isiyotarajika. ona ni kama ndoto, labda nipo ndotoni lakini ni ukweli ambao watu wanapitia. Nipo katika wakati mgumu mno, ukizingatia kwamba taarifa za jambo hili ziliwaslishwa kwa ndugu, jamaa na marafiki.

Nimekuja kwenu naomba ushauri, nahitajika kufanya nini ili niweze kuchukuliana na changamoto hii? Kuna wakati nashindwa kama binadamu naogopa kumfuru Mungu wangu. Nashindwa kusahau na namkumbuka sana kila wakati.
Wameachwa wengi kwa style hio... Shukuru unapumua
 
Na kwanini mlimwambia alipe mahari wakati mzigo ameshautafuna na kuutumia kwa miaka minne mfululizo?

Hivi zama hizi bado kuna wanaume wanaopapatikia kuoa?
Sasa akitokea huyo mwanaume wa kutaka kuoa bado watu wanamdai alipe mahari, how? Akisepa mnalaumu.

Badilikeni jamani.
 
Back
Top Bottom