Amebadilika siku chache kabla ya mahari

nafdat

Member
Jul 21, 2016
26
62
Salaam kwenu nyote.

Ninaomba ushauri wenu kwenu Kaka zangu na Dada zangu. Mimi ni binti.

Nimekutana na changamoto katika mahusiano yangu. Kisa ni hiki.

Nilikuwa katika mahusiano na kijana mmoja kwa takriban miaka 4. Baadae ikaonekana ni vema tufahamishe mahusiano haya ngazi ya wazazi. Kijana alikuja nyumbani kwa tararibu zote na kupangiwa mahari. Wakati wote huo mimi na kijana tuko vizuri na mawasiliano kwa hakika yalikuwa mazuri mno. Naweza kusema hakukuwa na jambo au tatizo baina yetu na mwenzangu ambalo labda lingekuwa kikwazo.

Hata hivyo, week moja kabla kuelekea siku ya mahari mwenzangu alinifahamisha kwamba wamehairisha kuja nyumbani kwetu sababu familia yake imeona gharama walizopangiwa ni kubwa. Naye alishikilia msimamo kwamba anaungana na familia yake.. Nilijitahidi sana kumweleza kwamba waje na gharama walizojiandaa nazo lakini haikuwezekana tena kwa mwenzangu. Ni kama alishaamua kusitisha jambo hili na mahusiano yote kwa ujumla na kwa hivyo sikuweza kubadili chochote kutokea hapo.

Nimejitahidi mara kadhaa kutaka kujua iwapo kuna sababu nyingine ya sababu hiyo lakin mara zote mwenzangu amekuwa akijikita katika sababu tajwa hapo juu. Hata ninapomuuliza mwenzangu juu ya nini kinachoendelea mpka wakati huu bado hanipi majibu. Kimsingi, inaonekana hakuna mahusiano tena kwa sasa.

Ninaumia kwa namna mambo yalivyoenda na yalivyohitimishwa kwa namna isiyotarajika. ona ni kama ndoto, labda nipo ndotoni lakini ni ukweli ambao watu wanapitia. Nipo katika wakati mgumu mno, ukizingatia kwamba taarifa za jambo hili ziliwaslishwa kwa ndugu, jamaa na marafiki.

Nimekuja kwenu naomba ushauri, nahitajika kufanya nini ili niweze kuchukuliana na changamoto hii? Kuna wakati nashindwa kama binadamu naogopa kumfuru Mungu wangu. Nashindwa kusahau na namkumbuka sana kila wakati.
 
born at 1970 sasa embu tueleze kuhsu umri kwanza
20220618_211346.jpg
 
Pole sana, ni kheri upigwe ngumi maumivu yataisha baada ya muda, ila maumivu ya mapenzi unaumia ndani kwa ndani na hayana dawa mbaya zaidi unajikuta unamfikiria huyo mtu kila saa, pasipo majibu sahihi.

Cha msingi ni kuwa mvumilivu maumivu, mawazo yapo hautoweza kuyakwepa hata uende ulaya, muda utakuponya polepole na utasahau. Kitu cha msingi usijiingize kwenye mahusiano mapya katika kipindi hikii utatumbukia kwenye shimo zaidi.
 
Pole sana.Huenda Kuna mambo mengine labda unatuficha. Kwa sababu kuishi miaka minne na mtu kisha aje kubadilika ghafla sio bure.Labda umeharakisha sana mambo na alihitaji muda zaidi ila aliogopa kukueleza kwasababu alijua ubgechukia na kumuacha.Jaribu kumwambia asahau kuhusu mahari na hakuna tena mahari arudishe moyo wake kwako muendelee tu uone atasemaje.
 
Fuatilia kwa makini nadhani utagundua kipi kimeingikia jambo lako, au kuna kitu hukiweka wazi kwa kulinda mapenzi yenu, na baada ya kupanga siku ya nahari na ndugu zako wengi kupata taarifa ya ujio wa wageni - siunajua ikishaingia kwenya familia na marafiki majirani kulijua hilo KATIYENU huwezi kujua labda amemwaga FIGISU, Pole Kila linalotokea chini ya jua lina sababu, muombe Mungu akupe mume mwema na mwenye upendo
 
Pole sana.Huenda Kuna mambo mengine labda unatuficha. Kwa sababu kuishi miaka minne na mtu kisha aje kubadilika ghafla sio bure.Labda umeharakisha sana mambo na alihitaji muda zaidi ila aliogopa kukueleza kwasababu alijua ubgechukia na kumuacha.Jaribu kumwambia asahau kuhusu mahari na hakuna tena mahari arudishe moyo wake kwako muendelee tu uone atasemaje.
Ahsante. Yeye bila kumshurutisha ndiye aliyemua tutoke hatua ya mahusiano tuliyopo twende kwa wazazi. Sikutumia nguvu kubwa.
 
Salaam kwenu nyote.

Ninaomba ushauri wenu kwenu Kaka zangu na Dada zangu. Mimi ni binti.

Nimekutana na changamoto katika mahusiano yangu. Kisa ni hiki.

Nilikuwa katika mahusiano na kijana mmoja kwa takriban miaka 4. Baadae ikaonekana ni vema tufahamishe mahusiano haya ngazi ya wazazi. Kijana alikuja nyumbani kwa tararibu zote na kupangiwa mahari. Wakati wote huo mimi na kijana tuko vizuri na mawasiliano kwa hakika yalikuwa mazuri mno. Naweza kusema hakukuwa na jambo au tatizo baina yetu na mwenzangu ambalo labda lingekuwa kikwazo.

Hata hivyo, week moja kabla kuelekea siku ya mahari mwenzangu alinifahamisha kwamba wamehairisha kuja nyumbani kwetu sababu familia yake imeona gharama walizopangiwa ni kubwa. Naye alishikilia msimamo kwamba anaungana na familia yake.. Nilijitahidi sana kumweleza kwamba waje na gharama walizojiandaa nazo lakini haikuwezekana tena kwa mwenzangu. Ni kama alishaamua kusitisha jambo hili na mahusiano yote kwa ujumla na kwa hivyo sikuweza kubadili chochote kutokea hapo.

Nimejitahidi mara kadhaa kutaka kujua iwapo kuna sababu nyingine ya sababu hiyo lakin mara zote mwenzangu amekuwa akijikita katika sababu tajwa hapo juu. Hata ninapomuuliza mwenzangu juu ya nini kinachoendelea mpka wakati huu bado hanipi majibu. Kimsingi, inaonekana hakuna mahusiano tena kwa sasa.

Ninaumia kwa namna mambo yalivyoenda na yalivyohitimishwa kwa namna isiyotarajika. ona ni kama ndoto, labda nipo ndotoni lakini ni ukweli ambao watu wanapitia. Nipo katika wakati mgumu mno, ukizingatia kwamba taarifa za jambo hili ziliwaslishwa kwa ndugu, jamaa na marafiki.

Nimekuja kwenu naomba ushauri, nahitajika kufanya nini ili niweze kuchukuliana na changamoto hii? Kuna wakati nashindwa kama binadamu naogopa kumfuru Mungu wangu. Nashindwa kusahau na namkumbuka sana kila wakati.
Pole sana.
 
Pole sana, ni kheri upigwe ngumi maumivu yataisha baada ya muda, ila maumivu ya mapenzi unaumia ndani kwa ndani na hayana dawa mbaya zaidi unajikuta unamfikiria huyo mtu kila saa, pasipo majibu sahihi.

Cha msingi ni kuwa mvumilivu maumivu,mawazo yapo hautoweza kuyakwepa hata uende ulaya, muda utakuponya polepole na utasahau. Kitu cha msingi usijiingize kwenye mahusiano mapya katika kipindi hikii utatumbukia kwenye shimo zaidi.
Ahsante. Nimepokea ushauri, nauzingatia.
 
Back
Top Bottom