Ameamua kunikubalia baada ya kuzalishwa

Ameamua kunikubalia baada ya kuzalishwa

On Duty

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2020
Posts
566
Reaction score
1,084
Habar za asubuhi wana J/Forums.

Mimi ni kijana ambae nimekaa katika uchumba kwa muda wa mwaka na nusu sasa na sijawahi kukutana nae kimwili huyo mwanamke na tumekuja kupendana kwenye simu baada ya sisi sote wawili ku move away from home.

Lakini mwanzo huyu dada alinisumbua sana na kila nilipokuwa najarib kumwambia nampenda hakuonekana kuniamini badala yake alinambia tubaki kuwa marafiki wa kawaida tu,maana tulikuwa tunaishi vijiji jiran.

Kwakuwa nilimpenda kutoka moyon basi niliendelea kumsumbua na baadae kila nilipompigia simu alikuwa akipokea mwanaume na anasema na kunambia kuwa nisimsumbue mke wake.

Lakini huyo jamaa alikuwa hajamuoa isipokuwa walikuwa wanadate kisela tu na wala hajulikan kwa wazazi wa mwanamke.

Sasa ikafika kipindi wakazalishana halafu mshikaji akala kona.

Baada ya miaka Kama mitatu hivi nikapata tetesi kuwa yule mwanamke hakuolewa lakn kadhalishwa,kwakuwa nami alikuwa bado yupo akilini mwangu nikaamua kumvutia waya na sasa ananikubali kupita maelezo ila ana mtoto.

Lakini hutujawah kutana kimwili hadi sasa na Yuko mbali.

Sasa nawasilisha kwenu wapendwa,je ni kweli huyu mwanamke amenipenda kweli au ni kwasabab ameshazalishwa?
 
Cha kwanza kabla ya yote acha kubeti ndio akili zitakukaa sawa.

Screenshot_20210306-082456.jpg


Unforgetable
 
.... achana na hiyo takataka; wadada wazuri, wanaojiheshimu na wenye misimamo wako wengi. Hadi alikuwa anampa jamaa yake simu kukutisha unapompigia bado unamfuatilia? Hivi kwa hatua hiyo, hata asingekuwa amezaa, bado unakuja humu "kuomba ushauri"? Wewe ni wa ajabu!
 
Unajua kihalali kabisa tunatakiwa kuoa binti Bikra.

Haya, hiyo bikra imekuwa ngumu tumesamehe. Bikra hana halafu ana mtoto tena 😭

Kitakachofuata sana utachukua asiye na bikra, mwenye mtoto na aliyetumiwa tigo.

Kidogo kidogo ndiko unakoelekea.

Mimk nakushauri na wewe piga mashine tu, kama vipi na wewe zalisha halafu kula kona🤣

Hakuna mke hapo.
 
Unajua kihalali kabisa tunatakiwa kuoa binti Bikra.

Haya, hiyo bikra imekuwa ngumu tumesamehe. Bikra hana halafu ana mtoto tena 😭

Kitakachofuata sana utachukua asiye na bikra, mwenye mtoto na aliyetumiwa tigo.

Kidogo kidogo ndiko unakoelekea.

Mimk nakushauri na wewe piga mashine tu, kama vipi na wewe zalisha halafu kula kona🤣

Hakuna mke hapo.
Kwa huu ushauri ndiyo mtampoteza kabisa huyu kamanda kwa huyo mwanamke. Kiufupi tu ni kwamba, anampenda sana huyo mwanamke! Na yuko tayari hata kulea huyo mtoto aliyetelekezwa na mwanaume mwingine.

Jambo la kuombea hapa ni kwa huyo binti kujirudi na hivyo kuthamini, kumpenda na kumpa jamaa heshima anayo stahili. Kinyume na hapo, jamaa atateswa sana na mahusiano ya aina hii.
 
Back
Top Bottom