• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

Amani nawatakia (wana JF)

C

Choveki

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2006
Messages
449
Points
195
C

Choveki

JF-Expert Member
Joined Apr 16, 2006
449 195
Wana Jambo Forum;

Salama nawatakia, wenzangu wa humu ndani
Nadhani mtapokea, salamu zenye amani
Choveki naulizia, wenzangu mu hali gani?
Amani nawatakia, wenzangu jambo foramu

Nizitoazo muhimu, salamu toka moyoni
Muondokewe magumu, moyoni pia vichwani
Nasema pia mdumu, wenzangu wa humu ndani
Amani nawatakia, wenzangu jambo foramu

Za kheri pia baraka, pokeeni nawapeni
Ziwafikie hakika, hata ikiwa mwakani
Natuma kwa kuandika, msome humu netini
Amani nawatakia, wenzangu jambo foramu

Mwendo twasema mdundo, tusiishie mwakani
Leteni, leteni nondo, tuweze mkoma nyani
Muongezee uhondo, hapa kwetu kijiweni
Amani nawatakia, wenzangu jambo foramu

Hapa hili jungu kuu, ukoko upo kwa ndani
Twazungumza makuu, yatukerayo nchini
Hatuogopi wakuu, mradi twakoma nyani!
Amani nawatakia, wenzangu jambo foramu

Mpaka kieleweke, hapa hakuna utani
Kotini tuwapeleke, mafisadi wa nchini
Kila leo tuteseke, twaulizia kwanini?
Amani nawatakia, wenzangu jambo foramu

Saba nafika tamati, siwaagii njiani
Ni mwisho si katikati, mjue wa kijiweni
Ni nyie wana kamati, nawambiya kwaherini!
Amani nawatakia, wenzangu jambo foramu

Mwana JF,
Choveki.
 

Forum statistics

Threads 1,404,953
Members 531,857
Posts 34,472,748
Top