Kwa Simulizi za Mwana JF, Maalim Mohammed Said, Sio Mtu wa Kubezwa, Mengine ni Ukweli Mchungu!, Ila Pia Sio Mtu wa Kupuuzwa!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,467
113,582
Wanabodi, mimi ni mshabiki na mfuasi wa simulizi za mwana Jf maarufu, mwenye powers fulani za ushawishi, Mkuu Maalim Mohamad said, nyingi ya simulizi zake zina some religious controversies zinazoibua very heated debates humu jukwaani, kwa baadhi ya watu kumsupport asemacho ni kweli, na wengine kubeza, kuwa ni urongo. Most times, supportes wengi ni watu wa dini fulani, na wabezaji ni watu wa dini fulani!.

Huu uzi ni wa kumtetea Mkuu Maalim Mohamed Said, kuwa japo ni kweli kwenye baadhi ya simulizi zake kuna urongo fulani wa makusudi wenye malengo fulani mahsus, lakini sio simulizi zote ni urongo, nyingine zina ukweli fulani, ambao ni ukweli mchungu, hivyo asibezwe.

Lakini pia natoa angalizo, kwa wahusika, hebu msikilizeni kwa makini mfano hoja zake katika mahojiano haya kwa mijubu wa bandiko hili,
Mohamed Said: TANU kilikuwa chama cha Kiislam, hili hakuna mtu anayeweza kulipinga - JamiiForums


Kwa vile hii video imeondolewa kule YouTube MUHAMAD Said amesema "kwenye Bunge la JMT, wabunge Waislamu ni asilimi 6%" !, hii maana yake aslimia 94% ya wabunge ni Wakristo!, kitu ambacho sio cha kweli kabisa!, huu ni urongo wa mchana kweupe!. Mohamed Said: TANU kilikuwa chama cha Kiislam, hili hakuna mtu anayeweza kulipinga

Ukimsikiliza kwa makini hoja zake, utakubaliana na mimi kabisa kuwa huyu mtu, sio wa kubezwa hata kidogo kwa kipaji chake, uwezo wake na usimulizi wake, ila pia sio wa kupuuzwa.

Leo nimekutana na Bandiko hili humu jf likimbeza, Maalim Mohamed Said,
Siasa za" Mohamed Said" ni za kusimuliwa na upotoshaji - JamiiForums
Mimi kwanza nimekemea kuwa mnyonge mnyongeni, haki yake, mpeni, na kisha nikatoa angalizo, huyu sio mtu wa kupuuzwa.

  1. Habari zake zote ni hearsay au habari za kusikia na kusimuliwa,
  2. Habari zake zote ni brainwashed au habari za mtu aliyejazwa
  3. Habari zake nyingi ni outdated au zilizopita na wakati na kukosa ushawishi kwa kundi la vijana,
Mkuu GUSSIE, japo hata mimi huwa napingana na Mkuu Maalim
Mohamed Said katika baadhi ya maeneo makuu mawili, urongo mahsus na udini wenye some ill motives behind, lakini mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni!, humu JF, hakuna anayemfikia kwa uwezo na kipaji cha oratorio!.

Tanzania tangu tupate uhuru, pamoja na vyuo vikuu vyetu vyote, tuna maprofesa wa historia wenye ma Ph.D kibao, lakini hakuna hata mmoja ameandika chochote cha maana katika historia ya taifa letu, hivyo Mohammed Said, anapoandika historia ya babu zake ni haki yake, na wewe andika historia ya babu zako!.

Naomba kumtetea Maalim Mohammed Said katika maeneo matatu haya

  1. Habari zake zote ni hearsay au habari za kusikia na kusimuliwa-Sii kweli, kuna aina tatu tuu za kupata habari, 1. Kushuhudia, hii inaitwa 1st hand information, 1st hand news, witnessing, kuona ni kuamini. 2. Kuhadithiwa au kusimuliwa na mashuhuda waliishuhudia,hii inaitwa 2nd hand information or 2nd hand news. 3. Kufanya reseach, utafiti kwa kusoma kilichotokea na kuandikwa na waliotangulia. Neno Hearsay ni habari za kusikia tuu ambazo hazina uhakika na hazijafanyiwa utafiti. Maalim Mohammed Said anakusanya info kutoka hivyo vyanzo vitatu, hivyo its not true kusema habari zake zote ni hearsay, japo kwenye fasihi simulizi, hearsay huwa haikosekani, na ndipo hapo maurongo huwa yanaibukia kwa yeye kudanganywa na wasimulizi wake na kuingia mazima na kuja kutudanganya humu.
  2. Habari zake zote ni brainwashed-sii kweli, sio kila kitu cha Mohammed Said ni brainwash, zipo simulizi zake nyingi za visa vya kweli vilivyotokea kwa lengo la uhifadhi wa historia ya kweli ya babu zake na wale wazee wa Gerezani lakini pia nakiri ziko habari zake fulani ni maurongo yenye malengo fulani.
  3. Habari zake nyingi ni outdated au zilizopita na wakati na kukosa ushawishi kwa kundi la vijana-pia hii si kweli. Historia zote duniani ni mambo ya kale, lakini sio kila jambo la kale ni outdated, history is the study of past events in relations to the present, and to determine the future. Kati ya wana jf wenye ushawishi mkubwa humu jf, ni Maalim Mohammed Said, kuna issue fulani kuhusu Zanzibar, tulibishana humu, ghafla iligeuka shubiri, maana sikujua kama ana wafuasi wengi kivile, waliibuka watu humu sio tuu kunisonga na kunizonga kama mainzi wanavyozonga mzoga au utumbo wa jana, hali ya hewa ilichafuka na hali kuwa mbaya hadi ilifikia stage ya mimi kutishiwa maisha nisikanyage Zanzibar, nitakiona cha mtema kuni. Ilimbidi Maalim awapooze vijana wake, na kuepusha shari zaidi, mode waliufunga ule uzi, hivyo kwenye hoja za ushawishi na ufuasi, Maalim Mohammed Said ana powers za ushawishi mkubwa na ana wafuasi wengi ndio maana nimesema humu, huyu sio mtu wa kupuuzwa.
  4. Mfano Maalim Mohamned Said akihamasisha wafuasi wake wakutane msikiti fulani siku ya Ijumaa, na baada ya swala ya Ijumaa, watakwenda kwa amani kulikomboa eneo fulani la babu zao, na lile jengo la Darusalaam lililojengwa na Waislamu, na ule msikiti wa maeneo yale uliogeuzwa kanisa, linaloekea Kibla, liliporwa enzi za wakoloni Wajerumani wakaligeuza ni jengo lao.
  5. Watajitokeza watu kila kona, patakuwa hapatoshi!.
  6. Wakoloni Wajerumani pamoja na udhalimu wao wote, walipokuja walilitwaa jengo la Darusalaam lilikokuwa makao makuu ya Uislamu, Wakauvunja msikiti mkuu, na ule msikiti mdogo wakaugeza kanisa! . Wakataka kuhamisha makaburi, ziliteremka bakora haikujulikana zilitokea wapi!. Kwenye kaburi la Atas pale Clock Tower, waliletwa watu 60 mijitu ya miraba minne kuvunja kaburi lile, waliibuka kundi la nyuki wa ajabu, wakikudunga tuu sindano, unakwenda kufia mbele huku unakimbia!, hivyo wakalazimika kuheshimu makaburi ya Waislamu, hivyo katika maeneo yote serikali ya mkoloni aliyopora kutoka kwa Waislamu, misikiti, walivunja ila yale makaburi ya msikiti, waliyaheshimu, hata wakijenga makaburi yanaachwa, hivyo hili jengo ninalolizungumza hapa la Darusalaam, hapo kwenye makaburi walipaacha na makaburi hayo yapo mpaka leo, japo hutujui ni ya kina nani, ila waliyahifadhi.
  7. Sasa katika Swala hiyo, Maalim Mohamned Said akatoa historia ya eneo fulani pale Feri lilikuwa eneo la msikiti, wakoloni Wajerumani wakalitwaa na kuuvunja msikiti ule, na kujenga jengo fulani jeupe, ushahidi ni makaburi ya Waislamu yaliyohifadhiwa humo, hivyo ikapigwa takbir twende tukalikomboe eneo letu na jengo letu, amini usiamini kuna mtu atafurushwa baru, hamtaamini!.
  8. Waislamu wa Ilala na Buguruni na Temeke, wao wakusanyikie lile jengo pale Taraza next to Dar Group ili kutangazia umma, kuwa Waislamu wa Dar es Salaam wamekomboa eneo lao. Waislamu wa Kinondoni wao wakusanyikie lile jengo pale oppsite Bamaga, kutangazia habari njema hiyo.
  9. Amimi usiamini, kuna mtu kwenye jengo hilo atafurushwa watu hamtaamini, polisi wote wa Kamanda Sirro can't stop them, labda wawatumie vijana wa Mabeyo, and there will be a blood bath!.
  10. Hivyo huyu mtu, Mkuu Maalim Mohammed Said, japo ni mswahalina wa swala 5, very humble na down to earth, na akiongea anaongea taratibu, kwa sauti kama ya mzaha mzaha, lakini kiukweli, huyu sii mtu wa mchezo mchezo!, kuna mbegu fulani huwa anaipanda, siku mvua za kutosha zikinyesha, hicho anachokipanda kikachipua, kikaota, kikamea na kikakomaa na kuzaa matunda...kuna mahali hapatakalika!. Nimemaliza, mwenye masikio na asikie.
Kwa wenzetu wa Swala, nawatakia Ijumaa Kareem, wale wenzangu na mimi Furahi Dei Njema.

P.
Update.
Wanabodi,
Kwanza asanteni kuchangia uzi wangu, hii ni page ya 60, na hii ni post ya 1202, nadhani hoja kuu za msingi zimemalizika.

Bandiko lilikuwa na hoja mbili kuu,
1. Mkuu Maalim Mohammed Said ni mwandishi mzuri, ana kipaji cha masimulizi, "story teller", na maadiko yake japo yana urongo ndani yake, lakini pia yana ukweli mchungu, ambao ulifichwa na sasa unafunuliwa.

2. Urongo katika baadhi ya hoja zake, sio urongo wa bahati mbaya, bali ni urongo wa makusudi mazima wenye malengo fulani mahsus, ili kutimiza malengo fulani, hivyo sisi tuliojaaliwa to read in between the lines na kubaini the hidden motives behind, nikasisitiza huyu sio mtu wa kupuuzwa, asipuuzwe.

3. Kwa vile hoja kuu ya bandiko hili ni urongo specific uliotolewa kwa matamshi, na video kutoka YouTube yenye matamshi ya urongo huo, nikaiweka humu, yenye sauti ya Maalim Mohammed Saidi mwenyewe in person akimwaga maurongo fulani,angalizo hili limesaidia, kwanza kwa video hiyo sasa imefutwa hadi kule YouTube, hivyo urongo huo hauendelei kuenea na kusambaa, hivyo lengo la uzi limekamilika.

4. Maadam Mkuu Maalim Mohammed Said, ameelekeza mahali alipoutoa urongo huo, natafuta muda, nitathibisha kama urongo huo kweli sio wake bali na yeye ameuokota huko alikouokota na kuja kuumwaga kule YouTube, nikithibitisha hili nitamuomba radhi kwa kumuita yeye ni mleta urongo, na ku share na nyinyi urongo ulikotokea,ila pia katika ulimwengu wa utandawazi, sio vizuri kuokota kila kitu unachosikia na kukisambaza.

5. Mwisho namshukuru sana, Mkuu Maalim Mohamned Said, uwepo wake, michango yake, ilmu aliyoshusha humu, wafuasi wake, wapinzani wake, wakosoaji wake na wachagiaji wa kawaida, asanteni sana.

Shukrani za pekee, ziende kwa Mkuu Maalim Mohammed Said, bila yeye, bandiko hili, lisingefika pages nyingi hivi, lingeishia kuwa kama bandiko langu hili

Sheikh Mkuu, Mufti Atoa Uhuru kwa Waislamu ..... - JamiiForums

Kwenye bandiko hili, licha ya kuwa ni bandiko lenye hoja muhimu sana kutoka kwa Mufti, lakini hebu litembelee uone limechangiwa na watu wangapi, unaweza usiamini..Hivyo Mkuu Maalim Mohammed Said, asante kuchangia, zile powers zako ninazozizungumza ndizo zimelifikisha hapa bandiko langu hili.
Ubarikiwe sana.

P.
 
Kuna upofu aina tatu.
1. Wa macho ndio unaotambulika sana...

2. Upofu wa moyo huu huwa haumuachi mwenye nao salama... kiazi anaweza kukiita pera!!

3. Upofu wa akili... mtu hataki kufikiri kwa akili zake bali hutumia akili za wengine...

Tukiyaepuka hayo tutamuelewa Mohammed Said...
Lakini kwa kuwa kuna mahali tunaegemea hatutamulewa maana kuna ulevi fulani katika nyoyo na bongo....
 
Wanabodi, mimi ni mshabiki na mfuasi wa simulizi za mwana Jf, Maalim Mohammed Said, nyingi ya simulizi zake zina controversies zinazoibua heated debates humu jukwaani, kwa baadhi ya watu kumsupport asemacho ni kweli, na wengine kubeza, kuwa ni urongo. mara zote supportes wengi ni watu wa dini fulani, na wabezaji ni watu wa dini fulani.
Umeandika ndoto zako. Umeshindwa kuja hata na moja la upotoshaji wa Mohamed Said. Kuhusu hiyo "white house" unayoizungumzia, soma hiyoooo, kisha useme huyo ni Mohamed Said?

 
sijaweza kumfuatilia kwa muda mrefu huyo mheshimiwa lakimi mada zake kuhusu historia ta tanganyika mpaka kuwa tanzania si ya kiundani sana.

sijaona akitoka nje ya dar es laam na zanzibar.
sijaona akitoa historia nje ya jamii fulani ya kiimani.
sijaona akirudi nyuma kabla ya ujio wa waeneza imani huku tanganyika.
sijaona akitoa historia maeneo mengine ya bara huku.
sijaona akitoka nje ya mashariki ya africa

pamoja na hayo lakini sio mtu wa kupuuzwa moja kwa moja.
lakini pia sio wa specific kwenye general histori hapa tanganyika kabla ya ujio wa wakoloni na wamisionari.

maybe kama alivyosema mleta mada, kwuwa ana run kwenye kuwaelezea wazee wake na imani yake. lakini yote ya yote bado anabaki chachu katika nyanja hio.
 
Mkuu hilo swali anatakiwa aulize mtoto mdogo ila kwa mtu mzima ni aibu kuuliza

Nakuja mfano mdogo tu kule Zanzibar kuna mkiristo alishawahi kuwa Rais? Km hakuna mzee wetu anacholalamikia ni nini? Au ndio udini umemtafuna hadi amepungukiwa maarifa?

Je Tanzania kuna cheo gani ambacho hakijakaliwa na muislamu?

Kumbuka historia inawakumbuka watu waliacha alama kwenye jamii
Leta wewe ukweli. Tunashindwa nini? Simpo tu. Unaandika tu, Mohamed Said kasema uongo huu... Ukweli wake ni huu....


Wewe na wenzako kama wewe mnakuja na ngonjera "Uongo, uongo, uongo" ukweli wenu uko wapi?
 
sijaweza kumfuatilia kwa muda mrefu huyo mheshimiwa lakimi mada zake kuhusu historia ta tanganyika mpaka kuwa tanzania si ya kiundani sana.

sijaona akitoka nje ya dar es laam na zanzibar.
sijaona akitoa historia nje ya jamii fulani ya kiimani.
sijaona akirudi nyuma kabla ya ujio wa waeneza imani huku tanganyika.
sijaona akitoa historia maeneo mengine ya bara huku.
sijaona akitoka nje ya mashariki ya africa

pamoja na hayo lakini sio mtu wa kupuuzwa moja kwa moja.
lakini pia sio wa specific kwenye general histori hapa tanganyika kabla ya ujio wa wakoloni na wamisionari.

maybe kama alivyosema mleta mada, kwuwa ana run kwenye kuwaelezea wazee wake na imani yake. lakini yote ya yote bado anabaki chachu katika nyanja hio.
Pendael24,
Nimeandika mengi ni bahati mbaya kuwa wewe huyajui lakini yapo.

Nimeandika mengi nje ya Dar es Salaam katika makala na paper
zilizochapwa na katika miswada ya vitabu ambavyo havijachapishwa,

Lakini kuna kitu kinaitwa, ''demarcation,'' hiki ni muhimu sana kwani
huwezi kuwa, ''Jack of all trades and master of none,'' kuwa wewe
huna, ''speciality.''

Elimu ya somo lolote haiko hivyo kuna kuwa na somo maalum ambalo
mtu analimudu kwa kulijua vyema.

Nakuwekea hapo chini links ambazo zitajibu hoja yako kuwa sijaandika
nje ya Afrika na nje ya Uislam.
  1. https://mohamedsaidsalum.blogspot.com/2015/05/from-pages-of-east-african-magazine-sal.html
  2. https://mohamedsaidsalum.blogspot.com/2013/12/islam-terrorism-and-african-development.html (mada nilitoa Chuo Kikuu Cha Ibadan)
  3. The Torch on Kilimanjaro, Oxford University Press, Nairobi, 2006
  4. Contributing author for an African anthology: The Mermaid of Msambweni and Other Stories, Oxford University Press 2007, Nairobi.
Huenda tukajuana vizuri endapo utapita hapo juu.
 
sijaweza kumfuatilia kwa muda mrefu huyo mheshimiwa lakimi mada zake kuhusu historia ta tanganyika mpaka kuwa tanzania si ya kiundani sana.

sijaona akitoka nje ya dar es laam na zanzibar.
sijaona akitoa historia nje ya jamii fulani ya kiimani.
sijaona akirudi nyuma kabla ya ujio wa waeneza imani huku tanganyika.
sijaona akitoa historia maeneo mengine ya bara huku.
sijaona akitoka nje ya mashariki ya africa

pamoja na hayo lakini sio mtu wa kupuuzwa moja kwa moja.
lakini pia sio wa specific kwenye general histori hapa tanganyika kabla ya ujio wa wakoloni na wamisionari.

maybe kama alivyosema mleta mada, kwuwa ana run kwenye kuwaelezea wazee wake na imani yake. lakini yote ya yote bado anabaki chachu katika nyanja hio.
Yànayokutisha ni majina au anapoandika kuwa Nyerere alifànyiwà dua na Waislam?

Si uje na wewe useme hata kanisa la Mtakatifu Josefu lilimfanyia maombi yaliyoongozwa na father John Smith. Kama haijawahi kutokea basi uelewe ukweli ni upi.

Tatizo ni nini?
 
Hayana ukweli mkuu ni upotoshaji tu ili kuvuruga jamii yetu

Victor,
Mimi ukweli na niliyoandika katika kitabu cha Abdul Sykes upo katika Nyaraka
za Sykes ambazo kwa hakika ni katika baadhi ya kumbukumbu za TAA na TANU.

Inasikitisha kuwa wenye nyaraka hizi kwa zaidi ya miaka 50 hawajapenda kuziweka
wazi kwa umma zikasomwa na wote.

Ukweli wako wewe tayari unao katika kitabu cha historia ya TANU kilichoandikwa
na Chuo Cha CCM Kivukoni (1981).

Naelewa sana pale wengi mnapotaabika kuhusu historia hii.

Hii inatokana na wao kupigwa na mshtuko kwa kusoma historia ambayo
hamkupatapo hata siku moja kufikiria kuwa ilikuwapo.

Akili inakataa kuamini haya wanayosoma ingawa nawaambia kuwa yote yamo ndani
ya Nyaraka za Sykes na ni ''documented.''
 
Leta wewe ukweli. Mnashindwa nini? Simpo tu. Unaandika tu, Mohamed Said kasema uongo huu... Ukweli wake ni huu....


Wewe na wenzako kama wewe mnakuja na ngonjera "Uongo, uongo, uongo" ukweli wenu uko wapi?
Usijipe uzalendo wa kiislamu.
Siyo siri Mohammed Said hana ajenda zaidi ya msimamo kuwa Uislamu unaonewa na mfumo Kristo.
Hawezi kufikiri kwa mapana zaidi.
Usiingie huo mtego wa kifikra.
 
Back
Top Bottom