Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 5,313
- 4,750
Dini zina nafasi kubwa sana kwenye mtengamano na amani ya lo lote lile. Ndiyo maana kwa kuliona hili, baadhi ya nchi serikali zake zinatawaliwa na dini moja, hususanj huko Uingereza nk Anglican High Church..
Nchi yetu ina dini kuu mbili, waislamu na wakiristo. Ingawa katiba ya nchi yetu inasema serikali haina dini lakini ukweli unabaki pale pale kwamba dini hizi mbili zina influence (nguvu) kubwa sana kwenye utengamano na amani ya taifa letu.
Ndiyo maana hata kama haiko kwenye maandishi ya kikatiba, mtiririko wa utamaduni wetu ukuu wa nchi umekuwa wa kupokezana kati ya hizi dini kuu mbili. Alianza mkiristo (Nyerere), akafuata muislam (Mwinyi), akaja mkiristo (Mkapa), akafuata muislam (Jakaya), halafu akaja mkiristo (Magufuli) na sasa tuna muislamu (Samia). Na bila shaka awamu ya saba atakuwa mkiristo.
Mtiririko huo haukuja kwa bahati mbaya (coincidence). Ni utamaduni wetu wa kuheshimu nguvu ya dini zetu hizi kwenye ukuu wa nchi na ndiyo uliochangia kwa kiasi kikubwa kwa amani tunayojivunia ya taifa letu. Na mara zote isipokuwa awamu hii dini hizi zimekuwa na utiifu mkubwa kwa mkuu wa nchi na serikali yake. Dini hizi zimekuwa zikituaminisha kuwa mkuu wa nchi ni chaguo la Mwenyezi Mungu na kwa wakristo 'ya Kaisari mpe Kaisari, ya Mungu mpe Mungu'.
Inasikitisha kuona kwamba katika awamu hii ya muislamu, TEC ambayo mtendaji wake mkuu ni ndugu au swaiba mkuu wa kiongozi wa chama kimoja cha siasa anayeutafuta ukuu wa nchi kwa njia ya yote ile ikiwemo ya vurugu, limekuwa likimsakama na kumdharirisha sana mkuu wa nchi na serikali yake. Hotuba wa raisi wa TEC ya Pasaka inaonesha wazi matakwa ya kanisa hili la kuingilia kesi iliyoko mahakamani ya mtuhumiwa wa uvunjifu wa amanj ya nchi yetu ambayo TEC wanaita ni kesi ya watuhumiwa wa kudai haki.
Hotuba/ waraka wa Pasaka ni tofauti sana ule wa Eid El Fitri wa waislam uliojitikita kwenye kudumisha amani. TEC mnakotaka kutupeleka si pa zuri. Huyo katibu mkuu wenu, Dr Kitima, hana tofauti na aliyekuwa kabibu mkuu wenu, Dr Slaa, Mtimueni kama mlivyofanya kwa Slaa akaungane naye kwenye siasa na kuoa.