Ama kweli ukeweza ni moto wa duniani.......!

Ladyheart

Member
Jan 30, 2009
58
7
Leo nimeudhuria msiba wa mwanafunzi mwenzangu,ambaye amefiwa na mama yake mdogo,...katika msiba huo mengi yalijitokeza lakini moja kubwa ni hili la kimada wa mume wa huyo marehemu,....kimada huyo alitoa siku 3 za mke kuishi au kufa na kumuachia mume atanue nae.....na hatimae mke leo amefariki.....je nani wa kulaumiwa hapo wana Jf..mume aliyetafuta nyumba ndogo au mwanamke aliyetoa maneno ya kutishia maisha...
 
Wote wawili hao ni mashetwani, mume na kimada wake, na adhabu yao wataipata hapa hapa duniani
 
Ukimada na ukewenza siyo sawa. Kimada aliyeendekezwa na huyo mume hadi kufikia hatua ya kumtoa mke wa ndoa roho,hawezi kulaumiwa, huyo mume ndiye muuaji.

Ukiona mumeo anampandisha cheo kimada hadi kumfanya akutishie maisha na wewe ukabaki tu unasubiri utolewe roho, basi utakuwa mjinga.
 
Heading ya uzi wako haifanani na habari yenyewe, ukewenza katu haihusishi vimada, na kamwe haiwezi kuwa 'moto' kwa kuwa sharti la mume kukubalika kuoa mke wa pili, watatu au wanne ni uadilifu na kuishi na wake zake kwa wema na ihsani. Angalia usipotoshe, ukawatisha watu.
 
Leo nimeudhuria msiba wa mwanafunzi mwenzangu,ambaye amefiwa na mama yake mdogo,...katika msiba huo mengi yalijitokeza lakini moja kubwa ni hili la kimada wa mume wa huyo marehemu,....kimada huyo alitoa siku 3 za mke kuishi au kufa na kumuachia mume atanue nae.....na hatimae mke leo amefariki.....je nani wa kulaumiwa hapo wana Jf..mume aliyetafuta nyumba ndogo au mwanamke aliyetoa maneno ya kutishia maisha...

huu co ukewenza ni ukimada...wakalaumiwa ni wote wawili mwanaume na kimada wake... dah mke anakufa kwa ajili ya mtu wa kupita!!!!!!!!!!!!!!
 
Binafsi naona mwanaume maana kama si yeye mabaya hayo yasingempata huyo mama,na mume alikuwa na uwezo wa kumuokoa mke wake,
 
Sikuzake za kufa zimefika mengine inakua sababu iliwatu wapate lakusema,hakuna binadamu mwenye uwezo wakumtoa roho mwenzie ispokua mwenyezi mungu awe ametaka..
 
Sikuzake za kufa zimefika mengine inakua sababu iliwatu wapate lakusema,hakuna binadamu mwenye uwezo wakumtoa roho mwenzie ispokua mwenyezi mungu awe ametaka..

Mungu alimwambia shetani amjaribu Ayubu,ila tu atunze uhai wake,hivyo basi hata shetani aweza toa mtu uhai bila mapenzi ya Mungu
 
Sikuzake za kufa zimefika mengine inakua sababu iliwatu wapate lakusema,hakuna binadamu mwenye uwezo wakumtoa roho mwenzie ispokua mwenyezi mungu awe ametaka..

mbna wachawi wanachukua misukule na kihalisia tunaamini kwamba fulani amekufa kwa mapenzi ya Mungu
 
sad story~ haya mambo ni kweli yapo ila mimi nashangaa kwanini tusiyamalize! sie wanaume ndo chanzo cha matatizo ktk familia zetu! kwanini wanawake wengi? tujifikilie upande mwingine je, mke wako angekuwa na uwezo wa kuwa na wanaume wengi unngejisikiaje? kwanza mie naamini hakuna mapenzi kati ya watu watatu au zaidi!
 
Waswahili wanasema maneno uumba,pengine huyu dada hajasababisha yeye hicho kifo...hilo ni funzo kwe2 wanawake,kwani tunapenda kutoa maneno bila kufikiria mbele kitatokea nn...
 
namlaumu sana huyo mume ms.e... kama nini.anawezaje kumpa kimada nafasi kubwa ivo katika maisha yake?halafu atakuwa sio mwanaume uyo ni wakiume.mwanaume wa ukweli anaijua nafasi ya mke wake na katu hawezi kumruhusu kimada kumsogelea au hata kumuongelea mkewe. Nachukia sana men design hii
 
Back
Top Bottom