Ama kweli Lowassa amekwaa kisiki hatari!

Ama kweli Lowassa amekwaa kisiki hatari!

Ni sawa na kujifunga kitambaa cheusi na kutembea barabara yenye miba.
Utakula jeuri yako.
 
Hakika ninawaeleza,hali ya CCM hivi sasa ni tete,waasisi wa kudondoka kwa CCM ni Viongozi wa CCM wenyewe!!Natarajia kura nyingi za CCM kwa UKAWA.Waliotoka CCM ni wengi mno,waliojitambulisha hadharani ni wachache wengi wanaugulia moyoni ni maelfu kwa maelfu!!
Nimezaliwa miaka ya 70 na nimeishi vijijini ndani kabisa katika mikoa zaidi ya nane (Njombe,Arusha,Kagera,Morogoro ,Iringa,Rukwa,Mbeya,Pwani na Tanga) mijini pamoja na nje ya nchi.Kati ya mataifa yaliyokuwa na rasilimali ambazo asilimia 90 ya watu wa Nchi hiyo hawanufaiki nazo ni Tanzania.Tuna kila ina ya madini.tuna gesi na makaa ya mawe,tuna mbuga na misitu.ardhi safi na vyanzo vya maji,bahari,milima na mabonde yenye rutuba.Wananchi wa Tanzania ni "maskini wa kutupwa" kuna watu kesho yao ni kitendawili kigumu na wengine wapo hata jiji maarufu la Dar es Salaam. Maisha yamekuwa maigizo. Takwimu zinaonesha ujinga umeongezeka kwa asilimia za kutisha,vijana wengi hawajui kusoma wala kuandika.Wanaendelea na masomo ya Vyuo Vikuu ni wale wenye uwezo wa fedha na mali.Wengi wameshindwa kuendelea kwa sababu hawana uwezo ni mikopo ina utata mwingi..Mpaka leo tunavyoandika magonjwa ambayo yametokomea duniani Tanzania ndio mahala pake.Jiji la Dar limekumbwa na ugonjwa wa aibu wa kipindupindu na wengi wameaga dunia kwa sababu ya uchafu.Mahospitalini wagonjwa wamelala mzungu wa nne kwa magonjwa mbalimbali na wakina mama wakijifungulia mitaroni ama vichochoroni!!!..Upande wa pili,watoto wa vigogo wanasoma nje ya nchi ama katika shule ambazo ada ya mwaka ni Milioni 80.Matibabu yao ya mafua na kikohozi ni ulaya na Marekani.Mavazi yao yamedizainiwa na Madizaina maarufu duniani.Mapumziko yao ni Vegas ama London.Benki zao ni Uswisi na Visiwa vya Uingereza. Vyakula vyao vinaagizwa kutoka Italy na Singapore,Usafiri wao ni ndege za kukodi na magari ya kifahari.Barabara za vumbi hawazijui asilani...Kuing’angania CCM ni miongoni wa matatizo yetu Watanzania.Wakati umefika ni LAZIMA IONDOKE ili kama itakuwa na Jipya IJITAFAKARI….
 
2010 Dr.Slaa angekua Rais wa Tanzania, na kwenye mitandao ccm haijawai kushinda ila Mwisho Siku wengi wetu huduwaa.!
tatizo CCM mabao ya mkono kwa sana vinginevyo chama kingekuwa kiliisha jiozea kaburini long time!
 
nahicho ndicho kitusikitishacho...majority are misinformed(due to limited access) because of the corrupted system.

Hata mitandaoni msifikiri mna watu wengi.Mna mazuzu tu.Watu wengi makini siku hizi wamebaki wasomaji tu bila kuchangia chochote.Wamewaacha Bavicha mjaze matusi yenu kwa ushabiki wa kipunga na kinyumbu kwa huyo FISADI WENU.Ukitaka kujua angalia "NUMBER OF COMMENTS NI NDOGO UKILINGANISHA NA NAMBER OF VIEWS" kwa Thread husika...
 
1. Kwani CHADEMA hawatumii malori/hawabebi watu?
2. Kwani CHADEMA/UKAWA hawatumii wasanii?....Hawa akina Ney wa Mitego...Bob Junior...Wolper..Shamsa Ford sio wasanii?...

Umewataja wasanii 6 tu wakawaida kutoka UKAWA.

Vipi kuhusu zile YUTONG 2 za CCM zinazotembea na wasanii mikoani..?

😂😂😂😂👆
 

Usiwalaumi wananchi kwa kuwaita eti wajinga!

Hivi ulishawai kuamini mikakati ya wapinzani hasa Chadema.

Ikiwa Leo kiongozi anatoa kauli hii, baada siku mbili anaigeuka kauli yake tena Bila hata kuomba radhi kwa kauli ya awali nani alaumiwe.

Ikiwa Chadema yote ikiongozwa na Mbowe wametuaminisha ufisadi wa Lowassa kwa miaka nane, tena wamefikia hatua ya kutuasa atakae mchagua Lowassa akapimwe akili, Leo Bila hata aibu wala kutuomba radhi kwa kutudanganya miaka yote hii wanatuambia huyu mtu ni Safi hana tuhuma zozote.

Hata kama mtaji wa ccm ni ujinga, binafsi naamini mtaji wa ccm ni ujinga na upuuzi wa viongozi wa upinzani

Chama ni misingi, ila upinzani hauna misingi wala itikadi ya kueleweka, kifupi ni vigeu geu wasioamini kile wanachokisimia.

Sio wote tupo tayari kupigia kura hata maiti kama wengi wenu mnavyoapa.

CCM tumeichoka sana tu, ila upinzani hauko tayari kuongoza nchi zaidi ya Sanaa za Ruzuku.
 
Kaondoka sasa hilo waachien wananchi wao wataamua 25 October wamfanye nini! ?
Hao wengine mafisadi wenzie wako wapi?

.
Makamba jana kwenye mkutano Kigoma kasema mafisadi 10 wamebaki ccm ambapo nanba saba ya hayo mafisadi ni Jk mwenyewe.
.
 
Mkuu hoja sio wasanii,Mbona na nyie mnatumia Chopa Kama kivutio.

Ukweli ni kwamba Lowassa anapwaya kwa Magufuli Pamoja na mtandao hatari alionao.!

Umedanganywa wewe, utamwona Magufuli si muda mrefu akitumia chopa. Chopa inarahisisha kufika maeneo mengi kwa wakati mfupi.

Umeambiwa;-
Kwenye mikutano yenu fanyeni haya halafu urudi tena hapa JF:

1. Msitumie malori kusafirisha watu
2. Msiwatangulize jukwaani akina daimond na ze komedi!
 
Kuna watu ni thinker less kweli we ccm hadi Leo unategemea kura za watu wa kijijini?? Huko ambako wamechoka na kukasirika wakisikia ccm,, kwa dunian kwa taarifa yenu kinachotoa kwenye social media kinatokea kwa watu ambao hawatumii social na watumiaji wana upload tu, tuliokuwa mtaani tunaona hali halisi
 
Mkuu hoja sio wasanii,Mbona na nyie mnatumia Chopa Kama kivutio.

Ukweli ni kwamba Lowassa anapwaya kwa Magufuli Pamoja na mtandao hatari alionao.!

Oct 25 utanyamaza
 
Pamoja na Kujiandaa Kuchukua nchi kwa zaidi ya miaka 25.

Pamoja na kuwanunua aslimia kubwa ya wahariri na waandishi wa kawaida wa vyombo vya habari


Pamoja na kuwanunua robo tatu ya wajumbe wa kamati kuu hadi kufikia hatua ya kumzomea Mwenyekiti.

Pamoja na kuvinunua vyama vikubwa vinne vya upinzani na yeye akiwa ndio mgombea pekee.

Pamoja na kumiliki mtandao mpana zaidi na wa hatari nchini Mafioso & Mafisadi Unity (MMU)

Lakini bado anaonekana kupwaya kwa Magufuli,alieanza harakati za urais juzi ,tena hana mtandao ,hana vyombo vya habari vya kueleweka hata ule mtandao hatari Mafioso & Mafisadi Unity (MMU) unamwogopa na kumwangalia kwa jicho la tatu.!

Magufuli usikate tamaa ,watanzania wachache wenye uelewa na nchi yao wanatambua juhudi zako.!

Afadhali umekubali ww mwenyewe ni wachache wanaomkubali,
 
Ingekuwa urais unapatikana kwenye mitandao basi Lowasa angekuwa rais,lakini bahati nzuri wapiga kura asilimia kubwa ni wale ambao hawajawahi kutumia mtandao

kwa taarifa tu ni kwamb,watanzania weng wa hari ya chini wanamkubari lowasa,mpaka vijijini,xubir october ndipo mtafunguka akiri,kwa sasa pombe yenu imewalevya
 
Usiwalaumi wananchi kwa kuwaita eti wajinga!
maadui matatu aliosema nyerere(na sasa wameongezeka) ni upi umetokomezwa..ujinga hufutwa na elimu na jukumu la serikali kuelimisha na kufuta ujinga...

Hivi ulishawai kuamini mikakati ya wapinzani hasa Chadema.
ni kipi ni kikuaminishacho katika chama tawala....fikra zako chaguo lako..umeridhika na ccm endelea kutotaka(kuamini mikakati ya ccm) mabadiliko
Ikiwa Leo kiongozi anatoa kauli hii, baada siku mbili anaigeuka kauli yake tena Bila hata kuomba radhi kwa kauli ya awali nani alaumiwe.
unaongozwa zaidi na mihemko ya hisia na chuki kuliko kureason suala kwa ushahidi..kauli za jumla jumla niote kauli ipi kati ya zipi...
magufuli umteteaye umesahau aliahidi kompyuta kwa kila mwalimu..siku kadhaa ccm wakakanusha naye wala hakuomba radhi wala kuliongelea tena..#unafikimbaya
Ikiwa Chadema yote ikiongozwa na Mbowe wametuaminisha ufisadi wa Lowassa kwa miaka nane, tena wamefikia hatua ya kutuasa atakae mchagua Lowassa akapimwe akili, Leo Bila hata aibu wala kutuomba radhi kwa kutudanganya miaka yote hii wanatuambia huyu mtu ni Safi hana tuhuma zozote.
rasi wako alikwambia za kuambiwa changanya na zako..sasa sijui status ya ''zako''
Hata kama mtaji wa ccm ni ujinga, binafsi naamini mtaji wa ccm ni ujinga
ewaaa..na huku ukiendelea kumpigia chapuo Magufuli(watu haohao waliowekeza kwenye ujinga)


Chama ni misingi, ila upinzani hauna misingi wala itikadi ya kueleweka, kifupi ni vigeu geu wasioamini kile wanachokisimia.
unaweza niambia misingi na itikadi ya CCM ya Magufuli wako kwa ushahidi wa matendo yao?
Sio wote tupo tayari kupigia kura hata maiti kama wengi wenu mnavyoapa.
ungetambua no 1 enemy wa maendeleo nchi hii ungeng`amua kwa undani misingi ya kauli hiyo na si kuibeba kama ilivyo..
..naendelea kusisitiza mtaji wa ccm ni ujinga...

CCM tumeichoka sana tu,
umeichoka huku unampigia debe mgombea wake..sasa wewe unatofauti gani hao unaodai hawana misimamo...?ama hakuna wagombea wengine ukiacha hao wawili..
huku si kujitekenya kisa kucheka mwenyewe..
huwezi kukandia ccm na Ukawa kisha ukatumia nguvu nyingi kumnadi Magufuli kana kwamba hakuna wagombea wa vyama vingine...

ila upinzani hauko tayari kuongoza nchi zaidi ya Sanaa za Ruzuku.

nasisitiza..unaongozwa na mihemko na hisia katika kufikiri yajayo huku ukifunika kombe tulioshuhudia yakitendeka kutoka chama tawala....
 
.
Makamba jana kwenye mkutano Kigoma kasema mafisadi 10 wamebaki ccm ambapo nanba saba ya hayo mafisadi ni Jk mwenyewe.
.

Hapo sasa! So bila shaka lumumba wanajua kuwa at least wapi ni salama!

Kudili na fisadi mmoja! ? Au Kudili na mafisadi 10?
Watuache! !! Changes are inevitable
 
Kwenye mikutano yenu fanyeni haya halafu urudi tena hapa JF:

1. Msitumie malori kusafirisha watu
2. Msiwatangulize jukwaani akina daimond na ze komedi!

Weeeeeee....
Subutuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu
Kama wao wanaume wallahi wafanye hayo halafu uone watakavyojaza watoto wa chekechea uwanjani.
Ile sio kampeni ni show ya fiesta ndiyo inayofunga nyomi.
 
Mkuu Mimi sio mwandiashi wa habari wala sina uwezo Wa kuamua mkutano upi uonyeshwe na upi usionyeshwe.

Labda ungewauliza waandishi wenyewe wa habari.

Na kama unazifahamu sababu za kutorushwa ungetujuza wewe.

Mkuu idawa, nilitegemea wewe unayejua waandishi, vyombo vya habari, vyama na wafuasi kununuliwa...! Haitakuwa kazi kwako kujua tukio lisilo la kawaida hivyo kutokea ktk kampeni za mgombea urais kwa chama tawala! Hebu ichukue kama changamoto mkuu, mgombea afanye mkutano kwenye makao makuu ya mkoa halafu isionekane popote kwenye taarifa za habari za siku hiyo!!!
 
Back
Top Bottom