Ama kweli Lowassa amekwaa kisiki hatari!

Ama kweli Lowassa amekwaa kisiki hatari!

idawa, hebu semeni kwa nini mkutano wa magufuli Bariadi mjini haukuonyeshwa kwenye taarifa za habari ktk tv zote? Kwa nini ilionyeshwa mikutano kutoka sehemu zingine za mkoa wa Simiyu kama Lamadi nk. kasoro tu mkutano wa Bariadi ambao ni makao makuu ya mkoa?
 
Nenda kaangalie Masaki ile Haille Sellassie Road yote kila taa ya barabarani ina picha ya Magufuli. Nyerere Road, na kila ukuta ambao mwenyewe sio mkali. Ni aibu kukaa madarakani miaka 50 halafu utegemee picha ya mgombea kukupa kura. Kura zilipaswa kutoka kwenye maendeleo mliofanya.

Maisha ya ujanja ujanja hayafai. Naona mabasi ya mwendo kasi yamewekwa kwenye hold kusubiria 'siku fulani' ili angalau yalete kaimpact. Tehe tehe tehe! Taaban!

Kama Lowassa aliinajisi CCM tulia ainajisi na CDM. Na umesema AKINA LOWASSA, sasa Lowassa katoka, what about the rest?
Hakuna mgombea ambaye hana mabango mitaani hasa eneo analokubalika sio mbunge wala diwani.

Kwa hiyo ulitaka Ukawa tu ndio waweke mabango na ccm wabaki kimya kisa maendeleo waliyoyafanya.

Ni ngumu kuikosoa ccm bila kumhusisha na Lowassa na genge lake ,lazima ukubli Lowassa ni sehemu ya uozo unaouimba dhidi ya ccm.

Ndio maana wengi wetu tunaamini Lowassa ni genge tu la watu wenye uchu na rasilimali za Taifa hili hana uchungu wowote na nchi hii.

Ila kwa kuwa watanzania wengi tuna iq ndogo tunafuta mkumbo tu sio hoja na vigezo.
 
idawa, hebu semeni kwa nini mkutano wa magufuli Bariadi mjini haukuonyeshwa kwenye taarifa za habari ktk tv zote? Kwa nini ilionyeshwa mikutano kutoka sehemu zingine za mkoa wa Simiyu kama Lamadi nk. kasoro tu mkutano wa Bariadi ambao ni makao makuu ya mkoa?
Mkuu Mimi sio mwandiashi wa habari wala sina uwezo Wa kuamua mkutano upi uonyeshwe na upi usionyeshwe.

Labda ungewauliza waandishi wenyewe wa habari.

Na kama unazifahamu sababu za kutorushwa ungetujuza wewe.
 
hivi ww unafikiri Magufuli anaweza kujaza watu bila DIAMOND, ALLY KIBA, THE COMEDY, YAMOTO BAND, FUTUI NAKINA WEMA?????MAGUFULI ni saiz ya LISSU, ZITTO , JJ MNYIKA.
LOWASSA ni habari nyingine.

wote hao uliowataja ni watanzania wenye haki ya kumchagua na kumpenda kiongozi wanayeona anafaa. mbona humsemi afande sele , wolper na wengine. uzuri wa game ni kulumbana kwa hoja zenye mashiko. tuache kushabikia mabadiliko ambayo hujajipanga utachukua nafasi gani kwenye hayo mabadiliko zaidi ya kusubiri fujo ili upore mali za watu. ulishindwa kutenda kipindi chote cha miaka zaidi ya50 ya amani unataka kujitutumua sasa kwa kusubiri fujo? mimi simjui magofuli wala lowasa na wao hawanijui. lakini tunapofikia hatua za kuwachukia wasanii wetu ambao wametumia juhudi zao kujiwamua kimaisha inaonyesha kwakuwa tu wametumia haki yao kikatiba inatia kichefchef.
 
Kwenye mikutano yenu fanyeni haya halafu urudi tena hapa JF:

1. Msitumie malori kusafirisha watu
2. Msiwatangulize jukwaani akina daimond na ze komedi!

Mwisho wenu oct 25, wote mtarudi Monduli vichwa chini.

Magufuli Rais wa awamu ya tano.
 
Magufuli usikate tamaa ,watanzania wachache wenye uelewa na nchi yao wanatambua juhudi zako.!
Kwanza asikate tamaa. Pili Watanzania wachache! Bahati mbaya zaidi rais anachaguliwa na wapiga kura walio wengi!
 
Kwanza asikate tamaa. Pili Watanzania wachache! Bahati mbaya zaidi rais anachaguliwa na wapiga kura walio wengi!

Hao wachache sikumaanisha wapiga kura ,ila wenye kumsapoti kwa wapiga kura.
 
Kwa mtu anayejitambua anafahamu Magufuli ni Rais anayesubiri kuapishwa.
 
Mkuu hoja sio wasanii,Mbona na nyie mnatumia Chopa Kama kivutio.

Ukweli ni kwamba Lowassa anapwaya kwa Magufuli Pamoja na mtandao hatari alionao.!

Chopa ishakuwa kivutio tobaaaaa! ! Kweli Mnahaha! Ndo mwalimu wako alivokufundisha moja kati ya vivutio ni Chopa? Lumumba shughuli ipo
 
UKAWA wakichukua nchi 2020 hakuna kampeni za kichizi kama za ccm! Eti nao wanapiga kampeni kama wapinzani!? Eti tupeni miaka mi 5 tuboreshe ELIMU, pumbav miaka 54 yote mlishindwa ndo mje mweze 2015? Huo uwezo mmeutoa wapi? CCM haina uwezo huo (isome kwa sauti ya Sumaye). Eti juzi walivyokuwa Simiyu. eti tutaboresha zao la pamba, ina maana ndo limeanza kulimwa mwaka huu? Jamani ccm ya Magufuli haiwezi!
Kukosea na kutambua kosa ni hatua moja ya kusonga mbele.!
 
1. Kwani CHADEMA hawatumii malori/hawabebi watu?
2. Kwani CHADEMA/UKAWA hawatumii wasanii?....Hawa akina Ney wa Mitego...Bob Junior...Wolper..Shamsa Ford sio wasanii?...


Sijui CHADEMA/UKAWA wanapata wapi ujasiri wa kunyooshea vidole CCM?
 
Mnaongea as if matatizo yooote ya nchi hii yanaletwa na Lowassa. Mlipoanzisha operesheni ya kuvua GAMBA, mbona hamkumtoa? Haya yaliyofanyika baada ya yeye kuwa nje ya ofisi ya umma, mbona sio hoja zenu?

IQ ndogo unayo wewe na Watanzania wa zamani. Watanzania wa leo wana IQ kubwa na ndio maana wanawakataa. Kuna kashfa karibu 11 za karibuni, waliohusika wanagombea ubunge kwa tiketi ya CCM

Kumbe unakubali kuna baadhi ya makosa yamesababishwa na Lowassa, sasa kama kuna ufisadi anahusika unapata wapi ujasiri wa kumtetea.

Sawa tumeichoka ccm, na waliosababisha ccm ichokwe ni Pamoja na Lowassa na genge lake.

Leo anapata wapi uhalali wa kuwania urais ikiwa faili lake Lina makando kando yasiyo na majibu?

Na mkijitaidi kijibu mnasema Mbona ufisadi haukuisha hata pale alipoondoka .

Hivi toka lini kosa likafutwa kwa kosa.?
 
Kukosea na kutambua kosa ni hatua moja ya kusonga mbele.!

Tatizo mmepewa kazi ya kusafisha kaniki wakat rangi inajulikana! !

-Escrow (na wahusika mmewaputisha wagombee ubunge )nayo ni lowassa?
-vipi kuhusu EPA? Ni lowasa?
-TWIGA waliopanda ndege je?
-meno ya TEMBO?
- vivuko feki inakuwaje?
Kwa machache hayo unasemaje?

Mmejichafua (uhalo) mnazuga hamuoni wakat inzi na halufu vipesambaa
 
Back
Top Bottom