Am I a loner,selfish?

Habari za Pasaka. Jana ilikuwa sikukuu hivyo nilipata mialiko. Ajabu nilikataa mialiko yote nikaamua kukaa nyumbani peke yangu siku nzima na sikuboreka hata kidogo kwasababu nishazoea na nilipanga nisitoke.

Mwaliko wa kwanza Bi Mkubwa kanipigia asubuhi,anajua nakaa mwenyewe, kaniomba niende nyumbani nikajumuike nao. Bila kujiuliza nikamjibu leo sitaweza kuja nimetoka nje ya mji wakati nimepanga kushinda nyumbani.

Baadae kanipigia binamu wangu,me, kaniomba aje nae nikamwambia leo sitakuwepo nyumbani. Wa mwisho rafiki yangu mkubwa kanipigia jioni kaniuliza kama nipo tu nyumbani anipitie tukasafishe macho maeneo fulani, huyu nilimjibu tu kuwa nipo ila leo sitoki.

Nimekaa nikajifikiria naweza kuwa mbinafsi au loner fulani bila kujijua? Maanake napenda sana kukaa mwenyewe nyumbani au naweza kwenda sehemu ya starehe peke yangu. Na kuna marafiki wananishangaa nawezaje kukaa mwenyewe siku nzima!
Ni kawaida tu .Watu tumeumbwa tofauti.Labda kama unajisikia sad
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom