Always a hungry man is an angry man

oba

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
310
65
Kama medical doctor nimejifunza umhimu wa glucose(sukari) kwa ubongo kuweza kufanya kazi vizuri na ndiyo maana mtu akiwa na njaa anakuwa mkali maana ubongo hautaki shida ya kuhitaji kufikiri zaidi wakati sukari imeisha mwilini.
Nimekuja kugundua kuwa watanzania walio wengi hasahasa vijana wana hasira sana na ndiyo maana tunakoelekea kama mambo hayatabadilika hasira hizo zaweza kuleta maafa au machafuko makubwa, lkn sababu ya hasira hizo ni nini?
1. Wengine hawali chakula zaidi ya mlo mmoja kwa siku, chakula kibovu kisichokuwa na virutubisho vyote. Ubongo wao unachoka kufikiria maisha huku miili yao ikiwa haina glucose kwa masaa zaidi ya 12.
2. Wengi wao wana njaa ya kazi hawana ajira na walipojiajiri wenyewe mfumo umeshindwa kulinda kazi zao na wakaporomoka.
3. Wengi wao wana njaa ya utajiri, wakijilinganisha na top layers/matajiri/viongozi waandamizi wa serikali wanagundua kuwa gap lililopo kati ya wadosi na wao ni kubwa mno kiasi kwamba haliwezi kuzibika; waishia kuwa na hasira
4. Wana njaa ya haki na usalama; wakiyatazama magereza ya nchi hii wanakuta yamejaa watu hohehahe, wezi wa kuku na mihogo, waliosingiziwa ubakaji, watoto wa wanyonge wakati wenye makosa ya uhaini wa kuhujumu taifa au kundi la watu wanapeta na magari yao ya viyoyozi, inauma sana, akili inaona njaa- Hasira!!
5. Wana njaa ya miundo mbinu imara; wakilima mazao yanaozea shamba-no barabara imara, wakifanya biashara ya fresh products zinaozea kwenye majokofu- umeme hakuna, wakipeleka watoto shule-div 0, n.k
FIVE DEVILS in one body!!!!mtanzania huyo ataacha kuwa na hasira?
Nawasilisha!
 
Back
Top Bottom