Alshabaab waiteka ikulu ya Somalia

Alshabaab waiteka ikulu ya Somalia

Status
Not open for further replies.
Majeshi ya Kenya na washirika wake wapo wapi wakawasaidie wenzao kuikomboa Ikulu.
 
hao wakenya wako somalia kwa shinikizo la marekani,, wakenya wanaumia kulinda maslahi ya marekani. toka kenya waende somalia wameshakufa wangapi? tafakari , wasomali wanawapenda sana al shabab,, serkali ya somali haina sapoti yoyote na wasomali..

Unaishi wapi wewe ambaye hujui Kenya imeingiaje ktk Vita na Alshabab Somalia?
 
KDF wako wapi sasa? Nchini kwao hakukaliki... huko walikokwenda kwa nguvu zote ikulu imebebwa......sasa hawa KDF wamejificha wapi? Au wamerudi Westgate kupora soda?

Tumuulize huyu lawmaina78 ndo balozi wa KDF humu
 
Last edited by a moderator:
Poleni jirani zetu..ila hao jamaa wako mbali sana na uislamu!!
Dini haijahimiza kitu kma hicho na si jihhad hyo!
 
inamaana huwa wanafurushwana au? maana kama ni kawaida basi hiyo ikulu inatumika kwa zamu

Ni kawaida hawa jamaa kutuma wapiganaji wa kujitoa mhanga kuishambulia Ikulu na maeneo mengine muhimu. Ni mashambulizi ya kustukiza. Mashambulizi ya aina hii ufanywa na Mataliban kule Afghanistan dhidi ya Vikosi vya Jeshi la Nato na USA.
 
Al shabaab wameiteka ikulu ya Somalia na mapigano makali yanaendelea baina ya wanajeshi wa Serikali na wanamgambo hao wa Al shabaab. Bado haijafahamika kama Rais wa nchi hiyo kama yuko hapo Ikulu au nje ya Ikulu.

Source: Sky News

Mkuu wangu badili heading ya habari yako. Angalau andika Ikulu ya Somalia yashambuliwa. Wapiganaji wa kujitoa mhanga 9 hawawezi teka Ikulu.
 
wakuu mbona sasa ni taarifa ya habari ila vyombo vyetu vya habari kama TBC hakuna habari kama hii?
kwani ccm ina activity yoyote somalia hata tbc irushe habari zao?? (jocking), btw, AMISOM si wapo huko???
 
LAZIMA MAJESHI YA KENYA NA AMISOM NA AU YAONGEZE BIDII LAKINI ITAKUWA NI BURE KAMA WASOMALI MAJORITY WANAWAPENDA AL SHABAB/KIUSALAMA WA DUNIA EA NA USALAMA BAHARINI NI LAZIMA AL SHABAB WAONDOSHWE haraka/
 
Kwani al shabaab wana interest gani hapo somalia,and who is behind the so called al shabaab???
 
rais wa Somalia yuko salama wakati tukio linatokea alikuwa kwenye sherehe nyumbani kwa mwakilishi maalum wa UN nchini humo.
 
Al shabaab wameiteka ikulu ya Somalia na mapigano makali yanaendelea baina ya wanajeshi wa Serikali na wanamgambo hao wa Al shabaab. Bado haijafahamika kama Rais wa nchi hiyo kama yuko hapo Ikulu au nje ya Ikulu.

Source: Sky News
Safi sana hao ndiyo wanaume
 
Kwasababu KDF ndio wanaotakiwa kuhakikisha Al Shababu wanasambaratika. Kenya ndio inayo nufaika zaidi na usalama somalia hivyo wanatakiwa kuhusika kwa kiwango kikubwa.
Wenye jukumu la kulinda Ikulu ni UDF na Burundi.
 
Ya kaisari tumuachie kaisari. ya somalia tuwaachie wasomali.. Al shabab inapendwa sana somalia,,, leo somalia ni sherehe kila mahali
Binadamu ndivyo walivyo, kesho utawasikia wanalalamika na kuwalaani Shabab!
 
KDF wako wapi sasa? Nchini kwao hakukaliki... huko walikokwenda kwa nguvu zote ikulu imebebwa......sasa hawa KDF wamejificha wapi? Au wamerudi Westgate kupora soda?

lawmaina78 ingawa unaugulia maumivu ya kipigo cha brazil vs germany,please pitia hiyo post hapo juu.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu unachuki na nchi yetu

Naomba nimjibie. Hana chuki na nchi yetu, ila ana chuki na kikwete na genge lake. Na Mtanzania yeyote mwenye uchungu na nchi yake lazima atakuwa na hisia kama hizo!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom