Alshabaab waiteka ikulu ya Somalia

Alshabaab waiteka ikulu ya Somalia

Status
Not open for further replies.
Tuinamishe vichwa Vyetu tusali kidogo ili kukemea haya mambo mabaya yanayoendelea Somalia
 
Waislamu tuungane kupinga vitendo vya Al shaababu, haiwezekani mwezi mtukufu wewe unaenda kuteka ikulu.

Alshabab hawana imani ya kweli ya uislam, wangekuwa ni waislam wa kweli wangefuata hata maana ya neno Islam, wasingekuwa chinjachinja kiasi hiki eti kwa kutaka rehma za Mwenyez Mungu! Siamini na sintaamini kama mauaji wanayofanya eti yanamfurahisha Mwenyezi Mungu.
 
Al shabaab wameiteka ikulu ya Somalia na mapigano makali yanaendelea baina ya wanajeshi wa Serikali na wanamgambo hao wa Al shabaab. Bado haijafahamika kama Rais wa nchi hiyo kama yuko hapo Ikulu au nje ya Ikulu.

Source: Sky News

kuongoza nchi za kiislamu shida sana.
 
Naomba tujadili hili. Hivi unaweza kunambia kwanini Majeshi ya Kenya yako somalia?

Hata kama majeshi ya kenya yapo somalia, kabla sijakujibu na wewe nijibu,"Hivi wale wanaouawa Westgate na mpeketoni na wengine ni watoto wadogo wamemkosea nini aliyewalenga risasi au kumchinja yeye binafsi?
 
Al shabaab wameiteka ikulu ya Somalia na mapigano makali yanaendelea baina ya wanajeshi wa Serikali na wanamgambo hao wa Al shabaab. Bado haijafahamika kama Rais wa nchi hiyo kama yuko hapo Ikulu au nje ya Ikulu.

Source: Sky News

Villa Somalia is one of the most heavily guarded areas in Somalia
Islamist al-Shabab militants have attacked the presidential palace in the Somali capital, Mogadishu, and entered the heavily fortified compound.

An al-Shabab spokesman said fighting was ongoing, but a government official told the BBC the attack was over and the militants had all been killed.

President Hassan Sheikh Mohamud was not at the palace at the time
 
Mbona huulizi UDF na 'BDF' vile vile kwani nao wako huko?
Kwasababu KDF ndio wanaotakiwa kuhakikisha Al Shababu wanasambaratika. Kenya ndio inayo nufaika zaidi na usalama somalia hivyo wanatakiwa kuhusika kwa kiwango kikubwa.
 
kwanini wazungu hawaingilii haya mambo aisee !

Wazungu walishachemsha muda mrefu sana' USA anajua kilichomtoa kanga manyoya.Kilichobaki wanawatumia nchi jirani na SOmalia kama Kenya' Ethiopia na Umoja wa Afrika (AU.
))
 
Mkuu Majeshi ya AU toka Uganda,Burundi na baadhi ya Vikosi vya Jeshi la Ethiopia ndio wapo Mogadisho. Jeshi la Kenya wapo Kusini ya Somalia na mji wa bandari wa Kismayo. Ni kawaida Alshabab kutuma wapiganaji wa kujitoa mhanga kuingia Ikulu kwa nguvu. Baadaye huwa wanafurushwa!

inamaana huwa wanafurushwana au? maana kama ni kawaida basi hiyo ikulu inatumika kwa zamu
 
Nchi za kiislam hasa maka na madina

kwa ubongo wako wa sisimizi ndo umekueleza hizo ulizozitaja ni nchi eeh!
enyi wagalatia msio na akili..... ni nani aliye ...........
 
Rais wao sio huyu anahojiwa hapa ITV on meet the leaders program?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom