Ally Salum Hapi, Ukweli huishi milele daima kaka.!

Wahenga walishawahi kunena kua "Uongo hufika kwa njia ya mkato lakini huishi kwa muda mfupi" na "Ukweli huchelewa kufika lakini hudumu milele"

Leo asubuhi akihojiwa na kituo cha StarTV kwenye mjadala unaohusu hali ya kisiasa kwa ujumla nchinj DC wakinondoni ndugu Alli Hapi ametoa tafsiri ya neno Demokrasia kua ni "Ni kuwapatia wananchi huduma muhimu kama Maji,Afya,Elimu,barabara nk." Kwakweli nikaamini kua kuna watu hufanya makusudi kabisa kuuweka pembeni ukweli na kuamua kuongea tu ilimradi watu flani flani waridhike.

Hivi kweli ndugu Alli akikutana na mtoto wa darasa la tatu akamuuliza "Neno demokrasia lina maana gani? halafu huyu mtoto akajibiwa jibu kama hili ataelewa nini? hivi demokrasia ni kutimiza ahadi ulizoahidi kwa wananchi kweli? Kupeleka Umeme kijijini ni demokrasia? Demokrasia ina maana gani hasa?Abraham Lincoln ailiposema kua demokrasia ni utawala wa watu kwa ajili ya watu nkwa watu alimaanisha nini? Inamaana hata hili hulielewi kaka?

Hata Marehemu Muamar Gadafi wa Libya na Sadam Husein wa Iraq nao walikua wakiwapatia wananchi wao huduma zote tena kwa 100% mpaka mwingine aliwasaidia hata vijana kuona na kuwalipa pesa za matumizi wasiokua na kazi.Lakini wananchi hawa walikua wakilia kila siku kua hakuna Demokrasia, walilia kua hakuna Uhuru wa kufanya siasa,walilia kua hakuna Uhuru wa kuongea ama kukosoa serikali yao, walioonekana kupinga serikali waliitwa wachochezi na wengine kuitwa wahaini, wengine waliopinga serikali waliuawa,waliteswa,walifungwa na wengine walikimbilia uhamishoni.

Unachokiona Libya na Iraq kwa sasa ni kwa sababu wananchi walitaka Demokrasia na sio huduma za kijamii,kwa sababu walipatiwa kila walichotaka ispokua demokrasia tu.

Kiufupi ndugu yangu Alli Hapi wewe ni msomi mzuri sana na mjenga hoja mzuri, simamia ukweli huwezi kufukuzwa kazi kwa sababu ya kuusema. Kwa nafasi uliyonayo kwa sasa you are supposed to be focused and distinguished person na sio kuogopa kuusema ukweli.Ukweli huchelewa kufika lakini hudumu milele na Uongo hufika kwa haraka ila huishi kwa muda mfupi.
Kila mtu anatafsiri ya demokrasia ktk muktadha wake. Abraham Lincoln alikuwa ni binadamu siyo kwamba ndiyo alikuwa mjuvi wa tafsiri ya demokrasia kuliko wengine
 
Aibu hii itawala milele mana siku zinakuja ambapo upotoshaji huu utatumiwa kama reference kuonyesha namna tabaka tawala linavyotumia madaraka yake kupotodha umma ambao majority ni illiterate
Mnataka kuniambia nyie manyani kwasababu mzungu moja alitoa tafsiri ya ukuaji wa binadamu kutokea kwenye nyani? Mjitambue kuwa kila MTU anaweza kutoa tafsiri ya neno demokrasia siyo lazima afuate ya Lincoln
 
Ukitaka kujua maana ya democrasia, nenda ukagombee uenyekiti wa Chadema.

DJ mkwepa kodi atakuekezea vizuri sana.
 
Tafsir ya abraham lincolin ni tafsir iliyobase kwenye ideas za kibepar ie ndani yake ilikuwa nasura ya vita baridi.

Wajamaa nao walijiita wanademokrasia kwamtazamo wakiuchumi kwakuwa wao walikuwa wanatengeneza usawa ktk umiliki.
##dhana ya demokrasia nisawa nashimo lisilojulikana uhalisia wake wa ndani,ukiingia utakutana na moto mkali##

Kila mtu anatafsiri ya demokrasia ktk muktadha wake. Abraham Lincoln alikuwa ni binadamu siyo kwamba ndiyo alikuwa mjuvi wa tafsiri ya demokrasia kuliko wengine

Mnataka kuniambia nyie manyani kwasababu mzungu moja alitoa tafsiri ya ukuaji wa binadamu kutokea kwenye nyani? Mjitambue kuwa kila MTU anaweza kutoa tafsiri ya neno demokrasia siyo lazima afuate ya Lincoln
Mmeamua tuu kubisha

Asili ya democracy inatoka wapi
 
Kwahiyo tumefundishwa na hao waliotuletea?

Kwanini sasa tusiamini hiyo maana yao tunataka kuweka ya kwetu?
Maana yao ni finyu ie demo/people na cratis/power!
Maana yao imeishia hapo...!

Kwahiyo hatuwez kuchukua maana ya abraham linkoln moja kwamoja coz yeye sio mgiriki,kwahiyo maana asili huwa inachukuliwa kutoka kwa wenye neno nasio washehereshaji/mainterpretor.

##waliotafsir kinyume na linkoln wapo sawa kama alivyosawa linkoln##
 
Ndo hivo tena, watu inabidi kujivua ufahamu na kutetea hata mambo batili ili mradi tu mkate usipotee..
Nakumbuka miaka ya 90 mwanzoni wakati bunge likiwa bado ni la chama kimoja kuna ubishi ulitokea bungeni kati ya mbunge mmoja wa CCM (bahati mbaya sikumbuki jina), pamoja na John Malecela ambaye alikuwa waziri mkuu na kiongozi wa shughuli za serikali bungeni na ubishi wenyewe ulikuwa ni kuhusu tafsiri ya neno uzalendo au mzalendo ni mtu wa aina gani..
Yule mbunge yeye alisema kuwa mzalendo ni mtu mchapa kazi, mkweli, muadilifu, mwenye kuweka mbele maslahi ya wengine kwanza, anayeipenda nchi yake na yuko tayari kuitetea na kujitoa kwa ajili ya nchi yake. Mheshimiwa waziri mkuu yeye alikomaa na definition yake kwamba mzalendo ni yule anayeiunga mkono CCM na serikali yake!!..
 
..wakishindwa kupeleka huduma hizo kwa wananchi watabadili maana ya demokrasia.

..na kulingana na tafsiri yao ya demokrasia bila shaka hakuna demokrasia ktk taifa letu.
Mwisho wa siku watasema demokrasia ni kuvaa shati la kijani...
 
Maana yao ni finyu ie demo/people na cratis/power!
Maana yao imeishia hapo...!

Kwahiyo hatuwez kuchukua maana ya abraham linkoln moja kwamoja coz yeye sio mgiriki,kwahiyo maana asili huwa inachukuliwa kutoka kwa wenye neno nasio washehereshaji/mainterpretor.

##waliotafsir kinyume na linkoln wapo sawa kama alivyosawa linkoln##
Kwamba kujenga barabara na shule ndio demokrasia? Hata kama tunatengeneza definitions za kwetu si kwa kiwango hicho.
 
If you order a politician to stop doing politics, even for a day, are you not in effect saying you are banning politics? And is that something you want to try?
And when you allow yourself to do the same thing that you are banning your rivals from doing, is that not the same thing as entering the boxing ring with an opponent who has his hands tied behind his back, and you are the referee and chief judge, having picked all the other judges into the bargain?
 
Mimi sijasoma sana lakini naapa kwa wasomi hawa najiona kumbe niko juu sana tu. Ni aibu sana kwa kila anayejiita msomi halafu unapindisha ukweli na hii mpaka viongozi wa dini. Tanzania ni janga.
 
Tangu wakati wa Nyerere tulikuwa na definition sahihi ya democrasia na wakati huo ulikuwa wa ujamaa. Ni kwa vipi leo imebadilika?
 
8
Hahaha
Mkuu hakuna definition iliyo universaly accapted ya demokrasia, wewe una ng'ang'ania liberal view of democracy.
Soma historia , soma na vitabu utaelewa na sema nini.
Ndio maana nika kwambia kila mtu alikuwa sahihi kwa upande wake.
unadanganya ndugu
 
tafsiri sahihi ya demokrasia ni ile inayofundishwa mashuleni full stop.
 
Back
Top Bottom