Ally Salum Hapi, Ukweli huishi milele daima kaka.!

Ally Salum Hapi, Ukweli huishi milele daima kaka.!

Tangu wakati wa Nyerere tulikuwa na definition sahihi ya democrasia na wakati huo ulikuwa wa ujamaa. Ni kwa vipi leo imebadilika?
Pamoja TZ ilikuwa yajiita yakijamaa lakin wajamaa walikuwa hawana ushawih kama wamagharib, ndo maana wakaanza kujiita wajamaa nakujitegemea kuashiria walikuwa wanaanza kuuacha ujamaa slightly.
 
Hahaha
Mkuu hakuna definition iliyo universaly accapted ya demokrasia, wewe una ng'ang'ania liberal view of democracy.
Soma historia , soma na vitabu utaelewa na sema nini.
Ndio maana nika kwambia kila mtu alikuwa sahihi kwa upande wake.
Upo sahihi
 
Demokrasia ni dhana ambayo haina tafsiri moja, na hakuna maana moja ya demokrasia inayo kubalika na dunia nzima
Labda useme ulitaka aongelee demokrasia kwa mtazamo wa ki magharibi, hapo uta kuwa sahihi.
Tafsiri ya Gaddafi ilikuwa ina mashiko yake lakini, ilikosa vinasaba vya u magharibi na watu wake ndio walitaka wawe na demokrasia kama hiyo ndio waka mtoa.
Hapi alikuwa sahihi ila si kwa mtazamo wa ki magharibi. Na wewe uko sahihi ila si kwa mtazamo wa ki jamaa, na ki dhahania nyingine za demokrasia
Kuna maana ambazo angalau zimekubalika Kidunia. Lakini kama kwa sababu na wewe unajitoa akili, basi kawafundishe au kuwaambia watoto wako kuwa hiyo ndo maana ya demokrasia.
 
Kwamba kujenga barabara na shule ndio demokrasia? Hata kama tunatengeneza definitions za kwetu si kwa kiwango hicho.
Sio defn zakwetu bali demokrasia nimfumo uliotengenezwa kwanjia yakuendelea kukoloni nandio maana, maana yake inatofautiana kutoka kambi moja nanyengine yategemeana na nguvu yapande hizo,
##defn ya wagirik ni "nguvu yawatu",ila mainterpretor wao wakainterprete kwa maana zao, namiongon mwa maana moja wapo niyawajamaa nanyingine ya mabepar##
 
Wavivu wa kusoma utawajua tuu

Leta hoja zako kunipinga hapo
Maisha hayaendi kwa kukariri ndugu
[emoji28] usiishie kwenye definition tu, jiongeze mpaka origin yake, types, pillars of democracy and what does it mean by a democratic state ongeza na advantages of being a democratic state pia challenges to democracy especially in African states such as Tanzania. Usijiondoe ufaham kwa sababu ya 'tumbo'
 
Kila mtu anatafsiri ya demokrasia ktk muktadha wake. Abraham Lincoln alikuwa ni binadamu siyo kwamba ndiyo alikuwa mjuvi wa tafsiri ya demokrasia kuliko wengine
Jiongeze anzia mbali kule Greece ilikoanzia
 
Yupo sahihi kabisa. Tatizo kubwa la baadhi ya watanzania ni kuamini kila kilichosemwa na watu wa mataifa ya nje ndiyo sahihi. Huyu DC yupo sahihi kabisa kwa sababu yeye ametoa definition ya neno "Demokrasia " kwa mtazamo wa kitanzania zaidi. Kiongozi mkamilifu kabisa hawezi kuimba wimbo unaohusu Demokrasia huku watu wanakufa na njaa, wanakosa madawa hospitalini, hawapati elimu ipasavyo, hawapati umeme na huduma mbalimbali za jamii. Kipi cha muhimu zaidi kati ya demokrasia na huduma za jamii? KWA MAONI YANGU MIMI NI KWAMBA, ILI NCHI IWEZE KUPIGA HATUA KUBWA ZA MAENDELEO NI LAZIMA KWANZA KUWEKA PEMBENI "DEMOKRASIA". Hivyo namuunga mkono huyu DC kwa 98% kwani anajitambua na anajua mahitaji ya watanzania kuwa ni huduma bora za jamii. LIBYA na IRAQ walilewa huduma za jamii zilizokuwa zikitolewa na viongozi wao, wakasema wanataka demokrasia tena kwa mabavu. Kwa ulevi huo huo wakawaita watu wa mataifa ya nje ili wawasaidie kutafuta demokrasia kwa nguvu. Je, hiyo demokrasia waliipata? Kwa taarifa yenu ni kwamba, mpaka sasa wananchi wa IRAQ na LIBYA wanajutia kitendo cha kuwaua marais wao kwa sababu za kijinga.
Shudu.
 
Wahenga walishawahi kunena kua "Uongo hufika kwa njia ya mkato lakini huishi kwa muda mfupi" na "Ukweli huchelewa kufika lakini hudumu milele"

Leo asubuhi akihojiwa na kituo cha StarTV kwenye mjadala unaohusu hali ya kisiasa kwa ujumla nchinj DC wakinondoni ndugu Alli Hapi ametoa tafsiri ya neno Demokrasia kua ni "Ni kuwapatia wananchi huduma muhimu kama Maji,Afya,Elimu,barabara nk." Kwakweli nikaamini kua kuna watu hufanya makusudi kabisa kuuweka pembeni ukweli na kuamua kuongea tu ilimradi watu flani flani waridhike.


Hivi kweli ndugu Alli akikutana na mtoto wa darasa la tatu akamuuliza "Neno demokrasia lina maana gani? halafu huyu mtoto akajibiwa jibu kama hili ataelewa nini? hivi demokrasia ni kutimiza ahadi ulizoahidi kwa wananchi kweli? Kupeleka Umeme kijijini ni demokrasia? Demokrasia ina maana gani hasa?Abraham Lincoln ailiposema kua demokrasia ni utawala wa watu kwa ajili ya watu nkwa watu alimaanisha nini? Inamaana hata hili hulielewi kaka?


Hata Marehemu Muamar Gadafi wa Libya na Sadam Husein wa Iraq nao walikua wakiwapatia wananchi wao huduma zote tena kwa 100% mpaka mwingine aliwasaidia hata vijana kuona na kuwalipa pesa za matumizi wasiokua na kazi.Lakini wananchi hawa walikua wakilia kila siku kua hakuna Demokrasia, walilia kua hakuna Uhuru wa kufanya siasa,walilia kua hakuna Uhuru wa kuongea ama kukosoa serikali yao, walioonekana kupinga serikali waliitwa wachochezi na wengine kuitwa wahaini, wengine waliopinga serikali waliuawa,waliteswa,walifungwa na wengine walikimbilia uhamishoni.

Unachokiona Libya na Iraq kwa sasa ni kwa sababu wananchi walitaka Demokrasia na sio huduma za kijamii,kwa sababu walipatiwa kila walichotaka ispokua demokrasia tu.


Kiufupi ndugu yangu Alli Hapi wewe ni msomi mzuri sana na mjenga hoja mzuri, simamia ukweli huwezi kufukuzwa kazi kwa sababu ya kuusema. Kwa nafasi uliyonayo kwa sasa you are supposed to be focused and distinguished person na sio kuogopa kuusema ukweli.Ukweli huchelewa kufika lakini hudumu milele na Uongo hufika kwa haraka ila huishi kwa muda mfupi.
Labda Ndio Uelewa Wake Umeishia Hapo Mh. DC Hapi
 
Sio defn zakwetu bali demokrasia nimfumo uliotengenezwa kwanjia yakuendelea kukoloni nandio maana, maana yake inatofautiana kutoka kambi moja nanyengine yategemeana na nguvu yapande hizo,
##defn ya wagirik ni "nguvu yawatu",ila mainterpretor wao wakainterprete kwa maana zao, namiongon mwa maana moja wapo niyawajamaa nanyingine ya mabepar##
Kwa hiyo wewe "people's power" unaielezea vipi? Fafanua hiyo ya wajamaa ikoje na application yake ikoje katika Tanzania ya leo, na hali kadhalika ufanye hivyo kwa hiyo ya kibepari halafu tuone kama kuna inayoendana na definition ya mwenye heri Hapi
 
Maskini Tanzania, sasa tunaanza kupiga kelele kama Chura kwenye maji huku Wanyama wakiendelea kunywa maji! Heri kutawaliwa na wazungu tukajua kuwa ukoloni umerudi!
 
definition of democracy is controversy....... we choose our own way ......then its fine!
 
Mbona CHADEMA wanajiita chama cha Demokrasia lakini kinaongozwa kidikteta na Mbowe....Ukipishana kauli na Mbowe tu anakutimua
 
Kwa hiyo wewe "people's power" unaielezea vipi? Fafanua hiyo ya wajamaa ikoje na application yake ikoje katika Tanzania ya leo, na hali kadhalika ufanye hivyo kwa hiyo ya kibepari halafu tuone kama kuna inayoendana na definition ya mwenye heri Hapi
"nguvu yawatu"
-maana ya linkolin anakusudia ktk siasa ie watu wanamaamuzi yakumuweka kiongozi, watu wanamaamuzi yakujitungia sheria zao, watu wanamaamuzi nauhuru wakufanya watakavyo, watu wanauhuru wakumiliki, watu wanauhuru wakujieleza,watu wanauhuru wakuabudu, kwamaana hiyo yaonyesha democracy is just a term with no implementation.

Wajamaa wao, watu wanauhuru wakibinafsi/personal freedom, watu wanastaki kupata mgawo sawa ktk mali iliyochumwa ie kuondoa matabaka yakiuchumi,
Pia kwamaana hiyo democracy not applicable today.
Nakwamaana hizo democracy haitekelezeki sasa nahata kabla ya salum happy.
###dunia haina democracy###
 
Mnabishana bure tu bila kujiuliza hata viswali vidogo.
Kwani huyu DC alikuwa kwenye Intellectual debate au political debate? Mnatoana macho bila hata kujiuliza, mkitaka haya mualikeni kwenye kipindi cha kitaaluma na sio siasa. Mkiwekeza kwenye siasa mtavuna siasa.
DC hajaenda kutoa definition ya democracy pale, yeye kaulizwa mtazamo wake kwenye demokrasia sasa mlitegemea nini kutoka kwake zaidi ya siasa(mtazamo wake)? Inabidi huyo DC awashangae nyinyi kwa kutojua hata muktadha wa mada yao, na kama mnahisi ni upotoshaji kwa watoto wenu na vizazi basi mnastahili lawama hizo kwa kushindwa kuwaambia siasa ni nini.
Mnaogopa maneno ya DC huko mnashangilia tafsiri za Lisu ambazo nazo hazistahili kusililizwa pia na watoto.
 
Huyu alitaka kuongoza mapinduzi ya kumpindua Kipara enzi hizo pale Udsm. Ila kipara alikuwa mjanja sana na mapinduzi hayakufanikiwa. Sijui kipara atakuwa wapi sasa hivi? Nilitegemea angekuwa na kacheo kidogo. Alikuwa politician kuliko Salum.
Nakumbuka vizuri hilo sekeseke, jamaa alikuwa anaitikisa Revo sqr karibu kila wiki, alikuwa najua kujenga hoja na nguvu kubwa ya ushawishi, ila mkate wa kila siku umemtoa kwenye reli kabisa,
 
Mnabishana bure tu bila kujiuliza hata viswali vidogo.
Kwani huyu DC alikuwa kwenye Intellectual debate au political debate? Mnatoana macho bila hata kujiuliza, mkitaka haya mualikeni kwenye kipindi cha kitaaluma na sio siasa. Mkiwekeza kwenye siasa mtavuna siasa.
DC hajaenda kutoa definition ya democracy pale, yeye kaulizwa mtazamo wake kwenye demokrasia sasa mlitegemea nini kutoka kwake zaidi ya siasa(mtazamo wake)? Inabidi huyo DC awashangae nyinyi kwa kutojua hata muktadha wa mada yao, na kama mnahisi ni upotoshaji kwa watoto wenu na vizazi basi mnastahili lawama hizo kwa kushindwa kuwaambia siasa ni nini.
Mnaogopa maneno ya DC huko mnashangilia tafsiri za Lisu ambazo nazo hazistahili kusililizwa pia na watoto.
Tumia akili kidogo usiwe mtumwa wa fikra! Kwa hali ya mazingira na maisha yetu kwa sasa tunatakiwa kua na Maana ipi ya Demokrasia? Sijakataa kua neno Demokrasia ni broad, lakini tazama mazingira tuliyonayo kwa sasa.
 
Kuna watu humu wanataka kupanua mjadala kua mkubwa huku maana bora na sahihi ya neno demokrasia inajulikana wazi pamoja na neno lenyewe kua broad.Tusizibe masikio kutaka kutetea haramu, kwa mtazamo wake Alli ni Sahihi kwake yeye lakini sivyo ambavyo watanzania wanahitaji.
 
Mkuu umeongea kitu kikubwa sana japo watu wamegeuza madaraka kuwa upofu na ukiziwi, hawasikii hawaambiliki, likini watu wanataka haki kwa mujibu wa katiba, kuwa kiongozi haimaanishi ufanye yale yanayokupendeza kufanya na kutokufanya yale usiyopendezwa nayo hata kama yako kwenye katiba. Unaweza kutekeleza katiba kwa 99% ila watu wakaku evaluate na kukuhukumu kwa kutotekeleza 1%. Maana ya uongozi ni dhamana, ni kwamba unatakiwa kufanya utendaji wako kwa 100% na sio vinginevyo, ukiona huwezi basi jua hupaswi/hukupaswa kuwa kiongozi.
 
Back
Top Bottom