Ally Salum Hapi, Ukweli huishi milele daima kaka.!

Ally Salum Hapi, Ukweli huishi milele daima kaka.!

Nimekwambia achana na kusoma vitabu vinavyopotosha maana halisi ya neon Demokrasi. Neno demokrasi lina maana moja tu, matapeli wakaona kuna hela ya bure na hivyo kuandika vitabu na kupotosha maana halisi ya neno hilo. Hakuna idea mpya yoyote utayoipata kwa kusoma kitu kilichopotoshwa badala ya kuendelea kujiongezea ujinga na kuamini kitu potofu kwamba ndiyo maana halisi ya neon husika. Hakuna consensus kwa wale waliopotoshwa kama wewe lakini wale wanaotambua THE TRUE DEFINITION ya neno demokrasi hawatakuja na definition potofu kama ufanyavyo wewe hapa.

Sija potosha nime soma idea za watu mbali mbali kuhusu demokrasia, nimesoma viongozi na jamii mbali mbali walivo kuwa na fikra zao kuhusu demokrasia.
Wewe mwenye niki kwambia uniambie accepted definition ya demcracy huwez kunipa kwa sababu hakuna "concesus", sasa wewe unatumia "popular definition" ambayo ni ya ki liberali ila sio kuwa hiyo ya kwako tuu ndiyo iko sahihi
Ndio maana nika sema soma vitabu, usiogope kupata idea mpya ndugu
 
Acha upotoshaji wa kuandika kile utakacho wewe. Definition ya democracy ni moja tu popote pale duniani. Na achana na kusoma vitabu vinavyopotosha maana ya demokrasi. Kusoma vitabu vinavyoandika maana potofu ya demokrasi si ujanja. Hata wewe leo hii kukitaka kuandika kitabu na kupotosha maana ya demokrasi kama ambavyo unafanya hapa unaweza kufanya hivyo na watu wakakuamini kwamba ulichoandika ndiyo maana halisi ya democracy pamoja na kuwa ni maana potofu.
Aise ww ni mtu wa ajabu sana, aliyekwambia tafsiri ni moja nani, aliyekwambia hiyo tafsiri unayoijua ww ndo hiyo hakuna mtu anayeruhusiwa kuja na tafsiri nyingine ni nani, ww umeishia la ngapi mkuu?

Kama dunia na wanadamu wangekuwa hivyo unavyodhani ww sasa hv tungekuwa bado tupo kwenye ujima, utumwa N.k kwa kuwa nayo nilikuwa mifumo ya utawala na ilikubalika, lkn ilibadilika kwa kuwa walikuja watu na mawazo mapya na namna tofauti kabisa ya muono wa mambo.
Muono wa Lincoln hauwazui watu kufikirii tofauti!!
 
Yupo sahihi kabisa. Tatizo kubwa la baadhi ya watanzania ni kuamini kila kilichosemwa na watu wa mataifa ya nje ndiyo sahihi. Huyu DC yupo sahihi kabisa kwa sababu yeye ametoa definition ya neno "Demokrasia " kwa mtazamo wa kitanzania zaidi. Kiongozi mkamilifu kabisa hawezi kuimba wimbo unaohusu Demokrasia huku watu wanakufa na njaa, wanakosa madawa hospitalini, hawapati elimu ipasavyo, hawapati umeme na huduma mbalimbali za jamii. Kipi cha muhimu zaidi kati ya demokrasia na huduma za jamii? KWA MAONI YANGU MIMI NI KWAMBA, ILI NCHI IWEZE KUPIGA HATUA KUBWA ZA MAENDELEO NI LAZIMA KWANZA KUWEKA PEMBENI "DEMOKRASIA". Hivyo namuunga mkono huyu DC kwa 98% kwani anajitambua na anajua mahitaji ya watanzania kuwa ni huduma bora za jamii. LIBYA na IRAQ walilewa huduma za jamii zilizokuwa zikitolewa na viongozi wao, wakasema wanataka demokrasia tena kwa mabavu. Kwa ulevi huo huo wakawaita watu wa mataifa ya nje ili wawasaidie kutafuta demokrasia kwa nguvu. Je, hiyo demokrasia waliipata? Kwa taarifa yenu ni kwamba, mpaka sasa wananchi wa IRAQ na LIBYA wanajutia kitendo cha kuwaua marais wao kwa sababu za kijinga.
Mkuu toa tafsiri sahihi ya maneno haya!
Demo-
Cracy-
 
Amini utakavyo mmeshajazwa ujinga wa kusoma vitabu na bila kutafakari kwa kina na kufanya utafiti wenu wenyewe. Ndiyo tatizo la ELIMU MULUGO, ukishasoma kitabu basi umemaliza na kuamini chochote kilichoandikwa ndani ya kitabu husika.

Huyu alitaka kuongoza mapinduzi ya kumpindua Kipara enzi hizo pale Udsm. Ila kipara alikuwa mjanja sana na mapinduzi hayakufanikiwa. Sijui kipara atakuwa wapi sasa hivi? Nilitegemea angekuwa na kacheo kidogo. Alikuwa politician kuliko Salum.
Kipara yupo mtaani tuu namuona ona. Uchaguzi uliopita ulikula kichwa
 
Jana huyu Bwana Mdogo nilimshauri pia pale alivamia Ofisi za TRA kutaka kujua makusanyo ya kodi...na nilimliza maswali mawili;
Je anajua wajibu na mipaka ya kazi yake na pili je anataaluma ya Tax administration.
Sasa kama leo tena amebofoa kwa makusudi kabisa ili kumridhisha mtukufu hii ni laana sasa.
Ila Watz. wote tusiopenda unafiki tuwakosoe bila kuogopa japo awamu hii hawataki kukosolewa zaidi ya vigelegele,ngonjera na vifijo never allow this hell situation.
 
Kweli kabisa yani. Watu wa nafasi za kuteuliwa wanajishushia hadhi zao kisa kulinda uteuzi. Hatari sana.
Kule kwetu wanaitwa "viongozi wa Barabarani"
 
Demokrasia ni dhana ambayo haina tafsiri moja, na hakuna maana moja ya demokrasia inayo kubalika na dunia nzima
Labda useme ulitaka aongelee demokrasia kwa mtazamo wa ki magharibi, hapo uta kuwa sahihi.
Tafsiri ya Gaddafi ilikuwa ina mashiko yake lakini, ilikosa vinasaba vya u magharibi na watu wake ndio walitaka wawe na demokrasia kama hiyo ndio waka mtoa.
Hapi alikuwa sahihi ila si kwa mtazamo wa ki magharibi. Na wewe uko sahihi ila si kwa mtazamo wa ki jamaa, na ki dhahania nyingine za demokrasia
Mtazo wa kimagharibi ni upi na ule usio wa kimagharibi ni upi? Moja ni moja milele usibadilishe iwe mbili hata siku moja. Hata neno democracy limetokea magharibi pia nchi za ki socialist hazikuweza kuandika democracy kwenye vitabu vyao ndio maana zimeshindwa.
 
Amini utakavyo mmeshajazwa ujinga wa kusoma vitabu na bila kutafakari kwa kina na kufanya utafiti wenu wenyewe. Ndiyo tatizo la ELIMU MULUGO, ukishasoma kitabu basi umemaliza na kuamini chochote kilichoandikwa ndani ya kitabu husika.
Ww ndo haufikiri na kutafakari, ndo maana umengangania hicho kilichoandikwa na wengine na umekiamini asilimia mia kiasi kwamba unaamini hakuna watu wengine wanayo haki ya kufikiri tofauti.

Hv kama maana ya democrasia ndo hiyo unayosema ww ni sahihi, unadhani viongozi wanaochaguliwa wanatenda yale waliowachagua wanataka watende? Ww unaamini mtu mwingine anaweza kutenda, kufikiri na kuamua kama ww ambayo ungetenda, kufikiri na kuamua! ( dhana ya democrasia ni watu kuamua kufikiri na kutenda ndani ya muktadha wa waliowachagua)Kama sio, unadhani hicho unachokingangania bado kinareflect ukweli?.

Mwisho ni Mara ngapi viongozi wa Nchi hizo mnazotolea mapovu kuwa zimeendelea kidemocrasia wamekuwa wakichukua maamuzi kinyume na matakwa ya RAIA wao, ni mara ngapi RAIA wa USA wamepinga maamuzi flani kuchukuliwa lkn viongozi wanafanya kinyume na matakwa, kama hiyo aliyosema mtoa maada ndo maana ya democrasia na umengangania kweli!

Kumbuka story ya mbayuwayu, za kuambiwa changanya na zako!
 
Hahaha
Mkuu hakuna definition iliyo universaly accapted ya demokrasia, wewe una ng'ang'ania liberal view of democracy.
Soma historia , soma na vitabu utaelewa na sema nini.
Ndio maana nika kwambia kila mtu alikuwa sahihi kwa upande wake.
Alikua sahihi kwamba demokrasia ni kupeleka huduma kijijini?
Acheni kuwa kama vinyonga. Kipindi cha Mwinyi mlisema demokrasia ni kuruhusiwa kufanya kila kitu, kipindi cha mkapa mkasema demokrasia ni uwekezaji, kipindi cha Jk mkasema demokrasia ni hari mpya na kasi mpya leo hii wakati wa jpm manasema demokrasia ni kuwa na viwanda na kupeleka huduma kijijini
 
Hapo Hapi naona anajaribu kujotofautisha na waliotoa tafsiri, bila kukariri maana ya democrasia pengine yuko sahihi. nawaza tu.
 
Hawa MA dogo hizi position wamekutana nazo tu kutokana na background zao huko kweny Uvzzm zao na kujipendekeza Sana kweny system ndo mana wapo hapo.

Kuhusu kusimamia kweny UKWELI milele hawawez labda atakapo hama chama.

Inasikitisha kuona kijana shupavu kusimamia uongo na upotoshaji wa waz kweny Media.

Tutayaona MENGI Sana kweny hii Government ya awamu ya tano ambayo hayajawah tokea.

Naomba mniombee wa Tanzania mtayaona

Ndo maana watu wengi kwa kipindi hiki wanadharau sana wasomi na elimu ya vyuo vingi!
Fikiria uko na mtoto wa kidato cha kwanza ndo unatazama hicho kipindi afu kiongozi mkubwa kama yeye tena mwakilishi wa Rais wilayani anajibu kama vile, huyu mtoto atajifunza nini hapo kama siyo kuamini elimu haiwasaidii wasomi??

Viongozi wanatakiwa kuwa makini sana na kauli zao maana kwa kazi yake ni sawa na Rais katika wilaya! Neno lake ni neno LA RAIS!

WABADILIKE WANALETA UKAKASI
 
Hahaha
Mkuu hakuna definition iliyo universaly accapted ya demokrasia, wewe una ng'ang'ania liberal view of democracy.
Soma historia , soma na vitabu utaelewa na sema nini.
Ndio maana nika kwambia kila mtu alikuwa sahihi kwa upande wake.
Hivi hata Mugabe au Mseveni akiandika kitabu akatafsiri maana ya demokrasia na wewe utakimbiki ku-quote tu? Wizi mtupu.
 
Wahenga walishawahi kunena kua "Uongo hufika kwa njia ya mkato lakini huishi kwa muda mfupi" na "Ukweli huchelewa kufika lakini hudumu milele"

Leo asubuhi akihojiwa na kituo cha StarTV kwenye mjadala unaohusu hali ya kisiasa kwa ujumla nchinj DC wakinondoni ndugu Alli Hapi ametoa tafsiri ya neno Demokrasia kua ni "Ni kuwapatia wananchi huduma muhimu kama Maji,Afya,Elimu,barabara nk." Kwakweli nikaamini kua kuna watu hufanya makusudi kabisa kuuweka pembeni ukweli na kuamua kuongea tu ilimradi watu flani flani waridhike.

Hivi kweli ndugu Alli akikutana na mtoto wa darasa la tatu akamuuliza "Neno demokrasia lina maana gani? halafu huyu mtoto akajibiwa jibu kama hili ataelewa nini? hivi demokrasia ni kutimiza ahadi ulizoahidi kwa wananchi kweli? Kupeleka Umeme kijijini ni demokrasia? Demokrasia ina maana gani hasa?Abraham Lincoln ailiposema kua demokrasia ni utawala wa watu kwa ajili ya watu nkwa watu alimaanisha nini? Inamaana hata hili hulielewi kaka?

Hata Marehemu Muamar Gadafi wa Libya na Sadam Husein wa Iraq nao walikua wakiwapatia wananchi wao huduma zote tena kwa 100% mpaka mwingine aliwasaidia hata vijana kuona na kuwalipa pesa za matumizi wasiokua na kazi.Lakini wananchi hawa walikua wakilia kila siku kua hakuna Demokrasia, walilia kua hakuna Uhuru wa kufanya siasa,walilia kua hakuna Uhuru wa kuongea ama kukosoa serikali yao, walioonekana kupinga serikali waliitwa wachochezi na wengine kuitwa wahaini, wengine waliopinga serikali waliuawa,waliteswa,walifungwa na wengine walikimbilia uhamishoni.

Unachokiona Libya na Iraq kwa sasa ni kwa sababu wananchi walitaka Demokrasia na sio huduma za kijamii,kwa sababu walipatiwa kila walichotaka ispokua demokrasia tu.

Kiufupi ndugu yangu Alli Hapi wewe ni msomi mzuri sana na mjenga hoja mzuri, simamia ukweli huwezi kufukuzwa kazi kwa sababu ya kuusema. Kwa nafasi uliyonayo kwa sasa you are supposed to be focused and distinguished person na sio kuogopa kuusema ukweli.Ukweli huchelewa kufika lakini hudumu milele na Uongo hufika kwa haraka ila huishi kwa muda mfupi.
Mkuu nakubaliana na wewe DC kachemka kutoa tafsiri ya Demokrasia ila hata wewe umechemka pia. Hiyo tafsiri ya Abraham Lincoln ina mapungufu sana,kipindi anatafsri hivyo Marekani kulikuwa na vita vya ndani kati ya Blacks waliokuwa Kusini na Whites waliokuwa Kaskazini...hivyo hiyo tafsiri ilitumika kupunguza msuguano wa hizo pande mbili. Maana halisi ya Demokrasia ni mfumo wa uongozi kwa ajili ya kunufaisha wachache (tabaka tawala) kama Wafanyabiashara wakubwa, wasomi nk.Kinachofanyika ni kuwaaminisha watu kama alivyofanya Abraham Lincoln.
 
Yupo sahihi kabisa. Tatizo kubwa la baadhi ya watanzania ni kuamini kila kilichosemwa na watu wa mataifa ya nje ndiyo sahihi. Huyu DC yupo sahihi kabisa kwa sababu yeye ametoa definition ya neno "Demokrasia " kwa mtazamo wa kitanzania zaidi. Kiongozi mkamilifu kabisa hawezi kuimba wimbo unaohusu Demokrasia huku watu wanakufa na njaa, wanakosa madawa hospitalini, hawapati elimu ipasavyo, hawapati umeme na huduma mbalimbali za jamii. Kipi cha muhimu zaidi kati ya demokrasia na huduma za jamii? KWA MAONI YANGU MIMI NI KWAMBA, ILI NCHI IWEZE KUPIGA HATUA KUBWA ZA MAENDELEO NI LAZIMA KWANZA KUWEKA PEMBENI "DEMOKRASIA". Hivyo namuunga mkono huyu DC kwa 98% kwani anajitambua na anajua mahitaji ya watanzania kuwa ni huduma bora za jamii. LIBYA na IRAQ walilewa huduma za jamii zilizokuwa zikitolewa na viongozi wao, wakasema wanataka demokrasia tena kwa mabavu. Kwa ulevi huo huo wakawaita watu wa mataifa ya nje ili wawasaidie kutafuta demokrasia kwa nguvu. Je, hiyo demokrasia waliipata? Kwa taarifa yenu ni kwamba, mpaka sasa wananchi wa IRAQ na LIBYA wanajutia kitendo cha kuwaua marais wao kwa sababu za kijinga.
Kwa hiyo ukikanyaga democracy ya watu ndo madawa hospital yatakuwepo?
Barabara, maji, umeme na huduma zingine huletwa na kukanyagwa kwa democracy?

Mimi naona imani yako imekaa kisiasa sana kama siyo kumtetea bila kujua unachokitetea.

Mi napingana na vifananishi ambavyo vimekuwa ndo reference hadi kwa mkuu wa nchi wa nchi za Libya, Iraq, Syria na zingine kuhusu hilo jambo LA democracy wa nchi yetu. Mimi nafikiri viongozi wangechukua kama reference ili na sisi tusiingie kwenye mtego huo!
Naona ni vizuri kusema ukweli kama kuna jambo haliendi sawa.
 
Back
Top Bottom