mi mwenyewe nashauri sadaka ziwe zinatozwa kodi na pia CAG awe anapita huko. maana zile ni pesa za umma isije ikawa wakina lusekelo wanajitajirisha tu.
Jangaaa lingine hili!
tujadili, kwa nini janga?
Akichangia hoja leo bungeni, Ally Mohemed Keissy mbunge wa Nkasi Kaskazini kwa ticket ya CCM ameshauri harambee zote au michango yote, ikiwepo michango ya makanisa, misikiti, harusi au chochote ili mradi watu wanachangia pesa basi itozwe kodi.
Pia aliitaka serikali ipeleke matangazo yake YOTE TBC ili kukijengea uwezo kituo hicho, amesema hata serikali ya uingereza hupeleka matangazo BBC
kujua zaidi kuhusu mh keissy, soma cv yake hapa Parliament of Tanzania
Huyu mchizi kumbe hata darasa la saba hakumaliza, angesoma huyu balaa lake lingekuwa kubwa. Michango ya harusi isitozwe kodi ifutwe kabisa.
Nyumba za vigogo masaki walipe kodi. Mmachinga Ana maduka mtaji laki mbili faida elfu hamsini kwa mwaka wao masaki wanapangisha kwa dolari $ au hawaoni hili