Ally Hapi, Anguko lako kisiasa umelitengeneza mwenyewe!

Ally Hapi, Anguko lako kisiasa umelitengeneza mwenyewe!

[SLETS, post: 28955017, member: 116662"]hajaweka upande wa RC maana hayo yaliishajadiliwa na videos zikawekwa humu na youtube zipo.
Tunadeal ma kilichopo sasa toka kwa waziri Jaffo, na kukumbushia huo udhalilishaji.
Huwezi ukatenga kauli ya waziri na maneno ya RC. Nimeweka mtiririko wa tukio na mwanzo nikasema, waziri hakufuatilia kwa undani tukio. Mwisho nikahitimisha hakutenda haki

Waziri hautenda haki kwani suala limekuzwa na kuonekana la kitatibu badala ya kiutawala
Ingekuwa ni la kitabibu, Tanganyika medical board ndiyoingehusika. Hapo tungesema RC kavuka mipaka. Kwavile ni la kiutawala hakuna shaka lilikuwa ndani ya shughuli zake
Ukweli ni kwamba RC Hapi anapenda sifa za kijinga, licha ya kumsema vibaya yule daktari pasipo kufuata utaratibu, pale anaposema "huyu daktari simtaki kwenye mkoa wangu hata akikutea hana kosa apangiwe kazi sehemu nyingine sio kwenye mkoa wangu
Kupenda sifa ni tatizo nje ya lililopo. Ukianza kumhukumu kwasababu anapenda sifa hutakuwa umemtendea haki kwa suala lililopo mezani. Utakuwa umefanya 'prejudice'

Kumsema Dk nalo nimeliongelea kwamba halikfata kanuni za utumishi, utawala wala uongozi
Ndiyo maana nilisema RC alikuwa na fursa ya kuongea na management kujua kwanini walichukua hatua hizo. Inawezekana ni kwa nia njema lakini imefanyika vibaya

Kumkataa Dk anayo haki kama kiongozi wa mkoa. Haki hiyo ameitumia kwa kumuagiza RAS aandike barua wizarani ya kumkataa katika eneo lake. Kwa aliofanya kazi siku nyingi wanaelewa haki hiyo. Boss anaweza kukukataa katika idara akiwa na sababu za kuridhisha, RC anayo haki
" huyu mwendawazimu nani kamuambia Iringa ni yake?
Haya ni makosa si kwa RC tu bali kwa viongozi wa zama hizi.Mwalimu Nyerere alitumia sana neno ' Sisi, tumeamua, tulikubaliani,tukaona, tulipanga'. Hata salamu zake zilianza kwa 'ndugu wananchi'
Sikuwahi kumsikia na kama ilitokea ni mara chache sana kumsikia Mwl akisema 'sitaki'. Alikuwa anasema hutukubali au maneno kama katika uongozi wetu, nchi yetu n.k.
Siku hizi watu hawatumii nafasi za kitaasisi wanatumia nafasi zao 'nimeagiza, nimesema, wilaya yangu, wizara yangu. Hivyo ni mwendelezo tu wa matatizo ya uongozi na matumizi ya lugha
je kuchochea daktari kubadilishwa kituo cha kazo ndio kutafuta suluhisho?
Ni jambo la busara kwani kumfanyia demotion na kumwacha hapo kutazua matatizo makubwa zaidi
Kwanza, akiwa Dk atakuwa amepoteza public trust. Wateja wake watamwangalia kwa jicho tofauti la kushindwa, kumbe si kitaaluma ni kiutawala.
RC alitakiwa kukaa chini na uongozi sa hospitali husika kujua chanzo cha lile tatizo nini nini, na litatuliwe, sio kuropoka ropoka kwenye hadhara ili tu watu washangilie
Hili ni tatizo, na alipaswa afanye hivyo
Nilisema alipaswa akutane na management aelewe ukubwa wa tatizo, na kama lilifanyika kwa nia njema ya kujenga au kwa nia nyingine
 
Alipokuwa mwembamba / amekondeana alikuwa na ' akili / upeo ' mno ila alipoanza tu ' Kunenepa ' tiketi yake ya ' Upopoma ' ameshaikata tayari. Naomba niishie hapa tafadhali.
Hivi kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya mabadiliko ya mwili na mabadiliko ya akili?
 
Chakaza, post: 28955759, member: 1840"]Mkuu Nguruvi3, bado kosa linabaki palepale kuwa RC katumia makosa ya kimanagement kuyafanyia maamuzi kisiasa.
Ukisoma bandiko langu #190 nimelieleza vizuri na kwa kina. Hata nilipomaliza nilisema kuna tatizo la watu kujua admin na management. Kwamba, suala la utawala na uongozi linachanganywa na siasa
Nikasema huo ndio mtizamo wa RC na ni makosa ya kukosa shule za uongozi
Hilo kosa LA Daktari jee lilikuwa LA kumsimamisha hadharani na kumdhalilisha kiasi kile mbele ya wagonjwa wake wa kesho?
Hapa nitamtea, RC alikuwa katika harakati za kutafuta ukweli.

Alianza na DMO kisha RMO ambao wote hawakujua suala hilo isipokuwa Superintendent(Mfawidhi). Lilipotua kwake hali ikawa ngumu kwani wenzake walisema hawana habari. Katika bandiko 190 nikasema, ukitazama utabaini alikuwa katika panic au hawezi kujieleza.

Hilo si kosa pengine angeweza katika vikao vya ndani
Kuhusu kumdhalilisha nalo nimelisema, kwamba, hakukuwa na sababu za kumdhalilisha
Alipoona Dk hana majibu muafaka angeweza kutumia mbinu nyingine wakalimaliza ndani ya vikao kwa namna yoyote iwe kujadiliana au kutimuana.
Nao bila kufahamu (pengine kwa kukosa elimu au hulka) wakashangilia kwa bidii udhalilishaji huo wa kutafuta kiki za kisiasa?
Ni hulka ya Watanzania si kwa hili na mengi tu yanayoendelea.

Kutokana na hulka hiyo wanasiasa hufanya kila wawezalo ku 'score political points' kwa gharama za wananchi wenyewe
Hatari ya kudhalilisha taaluma ni kuwa kesho Mwananchi huyo mshangiliaji anaweza kujikuta theatre na huyo daktari bila RC kuwepo na kibinadamu tunajua nini matokeo ya hali hiyo.
Hapana kazi ya udaktari ina miiko yake hawezi kumhukumu mgonjwa.

Hata hivyo, ni wazi kuwa morali ya Dk na wenzake itakuwa imeshuka na hilo linaweza kuwa cost wananchi, Kwamba,anaweza kutimiza wajibu hata pale ambapo angeweza kwenda mbali
Makosa ya maamuzi ya ki management yapo kila siku na zipo namna za kuweka sawa bila kuathiri utendaji wa kitaaluma has a kwa hizi noble professional.
Nakumbuka hata Mama Samia aliwahi kulionya hili jambo akiwa Geita
Nakubaliana nawe kwa management.

Hata hivyo usisahau bandiko 190,hili si suala la kitaaluma(professional) ni la kiutawala

Kazi ya kwanza ya Dk ni taaluma na hiyo inasimamiwa na Tanganyika medical board
Utawala ni fursa tu na si kazi ya msingi ya Dk.

Kwavile ni suala la utawala likihusisha malipo n.k. ni makosa tunapolifanya la kitaaluma.
Ikiwa Dk anachukua rushwa ni suala la kitaaluma kimaadili (ethics). Kwa hili ni utawala

Kwa nchi za wenzetu managaement ni taaluma inayojitegemea.
Si lazima Mkuu wa Hospitali awe Dr. Kwa mazingira yetu ilionekana kutoa nafasi hizo ni jambo jema tukizingatia upngufu wa wataalamu wa admin na management

Chuo cha IDM kilikuwa kina kozi ya Hospital administrations, kwa lengo hilo
IDM ilikuwa inatoa mafunzo kwa viongozi nje ya taaluma zao ili wamudu management

Tunayoyaona ni zao la kufuta IDM bila sababu za msingi.
 
Kosa la Waziri Jaffo

Katika tweet yake ameonyesha kukerwa na madaktari kudhalilishwa
Nakubaliana naye kwamba RC hakutenda haki, alikuwa na fursa ya kuzungumza nao nje ya mkutano, kuchukua hatua , kuwafokea n.k. katika vikao vya kazi

Hatua aliyochukua katika mkutano wa hadhara ilikuwa udhalilishaji. Na hapa si kwa Dr tu, hata angekuwa mtumishi mwingine.

Kuna taratibu za utumishi sijui ni kwanini zipo ikiwa wenye dhamana nazo hawazitumii.
Huu mtindo wa 'kutumbua' hadharani kwa maswali mawili matatu ni aina ya 'poor management'

Kosa la Waziri.
Tweet yake haikuonyesha tatizo ni nini kati ya RC na Dr. Hilo limewaacha wengi hasa hapa jamvini kuamini kuwa tatizo ni la Kitaaluma. Siyo! tatizo ni la kiungozi na utawala

Pengine waziri hakupata ukweli, na sijui kwanini hakuupata ikiwa ana nyenzo zote za kuupata
Badala ya kuwa suluhu, amezidi kuwachanganya wananchi wasioweza kutaofuatisha masuala ya kitaaluma na kiutawala

Katika admin na management, Jaffo anapaswa kumuomba RC radhi na atafute ukweli
Alichokifanya si suluhu ni kuwachanganya wananchi
 
Angefukuzwa huyo
Kuwa kiongozi ni karama ambayo ukipewa lazima uitunze na kufuata misingi yote muhimu. Wewe baada ya kupewa u RC Iringa ukadhani adui yako ni mwakilishi wa wananchi Mch.Msigwa badala ya umasikini.

Pia watumishi wa umma ukawaona kama takataka mbele yako ambao wengi wao wameitumikia nchi hii kwa miaka mingi kwa uadilifu mkubwa sana.

Sasa wewe ukaleta hayo na ona sasa yanakutumbukiza shimoni kisiasa kwa kasi usiyotegemea.

Ulipaswa kulazimishwa kuomba radhi hadharani au uwajibike. Utajikuta kama Wema.View attachment 912420
 
Kosa la Waziri Jaffo

Katika tweet yake ameonyesha kukerwa na madaktari kudhalilishwa
Nakubaliana naye kwamba RC hakutenda haki, alikuwa na fursa ya kuzungumza nao nje ya mkutano, kuchukua hatua , kuwafokea n.k. katika vikao vya kazi

Hatua aliyochukua katika mkutano wa hadhara ilikuwa udhalilishaji. Na hapa si kwa Dr tu, hata angekuwa mtumishi mwingine.

Kuna taratibu za utumishi sijui ni kwanini zipo ikiwa wenye dhamana nazo hawazitumii.
Huu mtindo wa 'kutumbua' hadharani kwa maswali mawili matatu ni aina ya 'poor management'

Kosa la Waziri.
Tweet yake haikuonyesha tatizo ni nini kati ya RC na Dr. Hilo limewaacha wengi hasa hapa jamvini kuamini kuwa tatizo ni la Kitaaluma. Siyo! tatizo ni la kiungozi na utawala

Pengine waziri hakupata ukweli, na sijui kwanini hakuupata ikiwa ana nyenzo zote za kuupata
Badala ya kuwa suluhu, amezidi kuwachanganya wananchi wasioweza kutaofuatisha masuala ya kitaaluma na kiutawala

Katika admin na management, Jaffo anapaswa kumuomba RC radhi na atafute ukweli
Alichokifanya si suluhu ni kuwachanganya wananchi
Aaah Nguruvi3 bwana Leo umekuwaje? Jaffo tweet yake inaonyesha amei address kwa madaktari kuwaomba wamsamehe RC kwa kitendo alichofanya kwa Daktari bingwa mwenzao. Tena akisema huenda alifanya hayo akiwa na hasira.
Kwanza hapo inaonyesha hawa aliowalenga wanajua nini kimetokea. Na pia kwa kusema "huenda alikuwa na hasira" anamaanisha pia Daktari anaweza kuwa anamakosa lakini hatua zilizochukuliwa hazikufuata taratibu. Jaffo hana kosa.

Lingine, Hatuwezi katika muundo wa sekta ya afya TZ kutenganisha taaluma ya utabibu na utawala unapomhusisha DAKTARI MFAWIDHI WA HOSPITAL. Maana kapewa cheo hicho kutokana na taaluma aliyo nayo, huwezi kuta mtu mwenye MBA pekee akapewa huo udaktari mfawidhi.

Ila Nguruvi3 nadhani tuko pamoja, vijana hawa wa sasa wanapaswa kupewa uelekezi katika nafasi za uongozi wanazopewa.
Mara nyingi namuangalia kijana wa Dar jinsi anavyopeleka uongozi wake na maisha yake unaona kabisa no vigumu kupata busara za kiuongozi.
Badala ya kupenda kuambatana na wenye busara anakuwa rafiki mkubwa na makundi ya vijana wenye maadili machafu kwa Jamii. Simtaji maana nitageuza mjadala huu kuwa Kosovo Ila nimeeleweka
 
Ukivuruga ujanani utapata tabu sana maana zama zikipita unarudi kufaiti na kina madamu be humble.
 
Sasa kwanini hakumtumbua kama alimaanisha? Magu tunayemfahamu anaweza kukuteua saa mbili asubuhi na akakutumbua saa 3 asubuhi!
Sasa kwa nini aliyasema hayo. Kwa taarifa yako tu maana naona wewe bado kabisa. Naive. Style ya dictator hiyo. Hapi anafanya kazi at the mercy of the president. Anafanya kazi kwa neema tu ya rais. Hastahili kabisa. Usirukie kusema ni hivyo kwa wateuliwa wote. Hapana, si wote. Tunajua wapo wanaostahili. Kumbuka lazima awepo RC wa Iringa. Sio utashi wa rais! Akiwepo aliyeteuliwa kwa mazingira ya Hapi na yakatangazwa hadharani, chunga sana. Neema, ngekewa tu. Hajiamini hata chembe. Lolote atakaloambiwa kufanya na mteuzi wake, atalifanya na kuzidi. Hii kuzidi ndio tunaona na kushangaa. Aliyemteua sanasana atamtetea. Kunyamazia alichofanya ni kumtetea.
 
Kosa la Waziri Jaffo

Katika tweet yake ameonyesha kukerwa na madaktari kudhalilishwa
Nakubaliana naye kwamba RC hakutenda haki, alikuwa na fursa ya kuzungumza nao nje ya mkutano, kuchukua hatua , kuwafokea n.k. katika vikao vya kazi

Hatua aliyochukua katika mkutano wa hadhara ilikuwa udhalilishaji. Na hapa si kwa Dr tu, hata angekuwa mtumishi mwingine.

Kuna taratibu za utumishi sijui ni kwanini zipo ikiwa wenye dhamana nazo hawazitumii.
Huu mtindo wa 'kutumbua' hadharani kwa maswali mawili matatu ni aina ya 'poor management'

Kosa la Waziri.
Tweet yake haikuonyesha tatizo ni nini kati ya RC na Dr. Hilo limewaacha wengi hasa hapa jamvini kuamini kuwa tatizo ni la Kitaaluma. Siyo! tatizo ni la kiungozi na utawala

Pengine waziri hakupata ukweli, na sijui kwanini hakuupata ikiwa ana nyenzo zote za kuupata
Badala ya kuwa suluhu, amezidi kuwachanganya wananchi wasioweza kutaofuatisha masuala ya kitaaluma na kiutawala

Katika admin na management, Jaffo anapaswa kumuomba RC radhi na atafute ukweli
Alichokifanya si suluhu ni kuwachanganya wananchi
Mi nimeona clip inaonyesha RC na daktari wana makosa mwanzo nilipoona watu wamlaumu RC nikajua ndo kakosea kumbe ni wote, ila RC Happi ajifunze kauli kuna clip niliona ana mropokea mama diwani huko Iringa bila kumsikiliza, kauli zilikuwa za vitisho kupita maelezo
 
Huyu jamaa kapikwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam akaambukizwa sisa za visasi. Hawa watu wanatakiwa kuwa chini ya uangalizi kwa muda mrefu sana. Kuwapa ukuu si vizuri kwa ss
 
Mi nimeona clip inaonyesha RC na daktari wana makosa mwanzo nilipoona watu wamlaumu RC nikajua ndo kakosea kumbe ni wote, ila RC Happi ajifunze kauli kuna clip niliona ana mropokea mama diwani huko Iringa bila kumsikiliza, kauli zilikuwa za vitisho kupita maelezo
Rejea bandiko 190
 
Huyo nasikia alikuwa anapenda sana chipukizi tangu shuleni
madaktari ni watu muhimu kuliko blaa blaa
Haka katabia kanakuwa sugu hadi kwa Walimu. Mwendo ni huo huo
Sema athari ya Mwl ipo mbali sana ndio maana tunaonekana takataka! Madaraka ya kulevya
 
Back
Top Bottom