Wanajamvi, lazima mpate ukweli halafu mfanyie uchambuzi na si kukuupuka tu
Maamuzi ya waziri hayakuzingatia ukweli uliosemwa. Nimeiona video nzima iliyopo You tube
1. Suala ni la kiutawala si la kitatibu. Mkuu wa mkoa alikuwa na haki ya kulisikiliza
2.Kuna matatizo kwa pande zote, Mkuu wa mkoa kama mtawala, na Dakatari kama msimamizi
Dk Mfawadhili
Alishindwa kutetea maamuzi yake. Nilichobaini ni 'panic' au kushindwa kujieleza
Maamuzi ya kutoza fedha yalikuwa na lengo la kuimarisha huduma.
Dk. mfawidhi alitakiwa aeleze yalikuwa maamuzi ya management na si yake kwa lengo zuri
Maamuzi hayo hayakuzingatia sera ya Taifa, hivyo alitakiwa atetee uamuzi huo ni kwanini
Maamuzi ya management yalitakiwa yamfikie DMO na RMO, Dk mfawadhi hakufanya hivyo, kosa
Dk hakutakiwa ku 'operate' kama hospitali binafsi, alitakiwa awafahamishe mamlaka nyingine
Kwa kufanya hivyo, RMO angewajibika kwa matatizo yaliyotokea au angeshauri vinginevyo kabla
Mkuu wa Mkoa (RC)
Baada ya kupata ukweli alipaswa asiwe na jazba.
Ingelikuwa vema akatoa tamko, sera ya Taifa ifuatwe na anatengua maamuzi ya management-hospitali
RC hakutakiwa kueleza maongezi yake na Dk kwani ilikuwa ni mazungumzo ya kikazi( faragha)
Kuyaeleza ni kumdhalilisha Dk, kiutawala halikubaliki ''Praise publically criticize privately'.
RC alitakiwa akutane na menejementi kujua ni kwanini wanahitaji fedha ikiwa sera ya Taifa inatoa
Je, kuna tatizo jingine au ni kukiuka tu taratibu? Alitakiwa aongee nao apate ukweli kwa upande wao
RC hakupaswa kutangaza kumtimua wadhifa hadharani.
RC ana nafasi ya kuandika barua au kumsimamisha kazi kwa utaratibu wa kushindwa usimamizi. Hakufuata taratibu za kiuongozi na utawala
Kutangaza hadharani ilikuwa kumshushia hadhi kwa mtazamo wa kisiasa na si kiutawala.
Kushindwa uongozi hakupaswi kumdhalilisha. Dk anabaki kuwa mtaalamu bila kuwa kiongozi na hilo linapaswa kulindwa ili aweze kuendelea kupata 'public trust'. Kazi ya Dk ni matatibu, uongozi ni ziada
Mwisho, watu wanachanganya mambo. Hakuna suala la kitatibu lililoongelewa suala zima ni la kiutawala. Laiti angegusia mambo ya kitaaluma RC angekuwa amevuka mpaka wa kazi
Tatizo kubwa katika hii issue ni kukosekana kwa mafunzo ya management kwa viongozi, kiasi kwamba masuala ya kiutawala wanayaelekeza kisiasa.
RC maongezi yake yalilenga siasa zaidi ya kutatua tatizo kwa njia za kiutawala na uongozi
Waziri hakutenda haki kwa kutoweka upande wa RC. Mleta mada hakutenda haki kwa kutoweka upande wa RC na alichosema. Uzi mzima umekuwa 'sensational' bila kuzingatia facts
JokaKuu Moderator