Aljazeera yachambua maandamano ya Mange, yaishangaa Serikali

Aljazeera yachambua maandamano ya Mange, yaishangaa Serikali

Al Jazeera walichochea Watu Liby, Tunisia, Algeria, Syria Na Maeneo Mengi tu Kwa kigezo Cha kupigania Demokrasia..
Al Jazeera wanachocheaje watu? reporting vitu live bila chenga maana yake ni uchochezi? kwa mfano kwa hiyo Clip nimeona police wa Tanzania wakiandamana, magari ya washawasha yameingia mtaani as well as RPC wa Dodoma akitoa vitisho na povu zito as if binti yake kapewa mimba na wahuni. Hii bila shaka utaiita ni "uchochezi wa Al Jazeera"
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Huu upuuzi mlishauleta hapa ukakosa support bado mnauleta tena?, hivi kuna MTU hajaamini kilichotokea kwamba watanzania hawawezi kuandamanishwa na mtukanaji Kama MANGE?..
Uu kwana hukuwaona polisi wakiandamana kila mkoa????
 
Mtabakia hvyo hvyo vilaza nyie mkiambiwa ukweli mnasema uchochezi sjui mabinadamu mengine mkoje?bola mngekuwa mazombi tuu mkajulikana

Na Wewe unapigania Demokrasia Na Uhuru wa kujieleza
Nimetoa maoni yangu sijatukana lakin Wewe kwenye kujibu utanirushia Matusi lakin Bado unajiona unapigania Uhuru WA kujieleza
 
Mkuu wanafanikiwa kuchochea pale penye dalili ya kuwaka Moto! Ukiona wanachochea ujuwe kuna Mfalme **** ktk Nchi husika ama kisha haribu amani au anaelekea kuhatarisha amani. Hoja yako hapa haina mashiko zaidi tu imejaa unafiki Mkubwa

Qatar kuna Ufalme na Wao wanatokea huko huko Qatar lakin hawajaguswa wala kupinga Ufalme wa kwao Qatar lakin wameona waje huku Tanzania. Kama hujaona huu unafiki Wewe nikuiteje!
 
Na Wewe unapigania Demokrasia Na Uhuru wa kujieleza
Nimetoa maoni yangu sijatukana lakin Wewe kwenye kujibu utanirushia Matusi lakin Bado unajiona unapigania Uhuru WA kujieleza
Pohamba wengine hatuna uvyama ila tuna taka haki itendeke siyo kushabikia ata ujinga ndiyo maana mnawashutumu watu weupe kila kukicha eti wachochezi.

Hebu tuwe wastalabu mtu ishu ziko wazi mfano 1.5t hazionekani nanikweli ripoti inaonyesha afu mkuu anajibu kiulaini tuu afu alie hoji anaitwa mchochezi tena eti katumwa.

Jamani pohamba muwe na aibu watanzania masikini hawajui lolote hawa watu wana hangaika jamani watu wanakufa kwa kukosa huduma muhimu,maji ni shida na mengine mengi.

Lakini watu hatuwi naumoja tunajenga taifa bovu sana piga magoti muombe mungu akufungue akili huenda umefungwa japo Sina imani Kama huelewi mazuri na mabaya bali ni makusudi tuu.

Acha niishie hapa ukweli unaujua japo utanibeza ila hamna namna ata yesu alie msaliti alijua kabisa anatenda kosa ila hela ali ipenda zaidi.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Huu upuuzi mlishauleta hapa ukakosa support bado mnauleta tena?, hivi kuna MTU hajaamini kilichotokea kwamba watanzania hawawezi kuandamanishwa na mtukanaji Kama MANGE?..
Hawawezi au wanadhibitiwa wasiandamane ?! Jiulize ni hiyari yao au ni serikali iko tayari hata kupoteza uhai wa watu kuzuia maandamano ?!
 
Mikutano ya kisiasa inakusaidia nini?,Uhuru wa kutoa maoni UPI unautaka mbona upo hapa unatoa maoni?,tatizo mmekaririshwa na wanasiasa.Fanya kazi zako kujitafutia kipato.Huyo kahaba Mange mganga njaa tu USA tofauti ni yupo nje ya nchi tu.
Haya maneno unayomzungumza Mange yakurudi wewe kama ni vizuri !!
 
Qatar kuna Ufalme na Wao wanatokea huko huko Qatar lakin hawajaguswa wala kupinga Ufalme wa kwao Qatar lakin wameona waje huku Tanzania. Kama hujaona huu unafiki Wewe nikuiteje!
Jikite zaidi kwenye hoja ya msingi je, Wananch wa Tanzania wako huru kwa ssa!? Wanachokisema hao hakipo Nchini!? Wwe unaweza kushawishiwa kukubari na kufanya jambo ambalo unaliona halina mashiko!? Kwa ujumla, hauwatendei haki unapowalaumu hawa jamaa, mwambie JPM aiongoze Nchi kwa uhuru na amani uone km hao wana habari watapata cha kutangaza khsu maada hiyo hii!
 
Mikutano ya kisiasa inakusaidia nini?,Uhuru wa kutoa maoni UPI unautaka mbona upo hapa unatoa maoni?,tatizo mmekaririshwa na wanasiasa.Fanya kazi zako kujitafutia kipato.Huyo kahaba Mange mganga njaa tu USA tofauti ni yupo nje ya nchi tu.

Mkuu ulitaka mikutano iwasaidie kitu gani ndio ujue ni muhimu? Kwenye mpira kunawasaidia nini watu; hebu jaribu kuzuia uone. Acheni hoja za kulazimisha jamani.

Huu utoko, bado mnautafutia soko tu ?

Mmmm!! Kazi ipo, ndio maana sitoki jf.
 
Hmmm!nilikuwa nasikiaga tu huko nchi za jirani eti leo nayo Tz tunaanza kusomwa nje kwa maovu ya viongozi wetu. Shame
 

Ungeandamana kwanza acha kubweka mitandaoni ,kama una jeuri ingia kwa road ,mambo sijui nani aishangaa Tanzania ni kuuza habari,kama kushangaa hawakuanza leo,mtashangaa na watashangaa sana hao shangazi zenu wa huko Uarabuni.Sisi hatuna habari kwanza ndio mwendo mdundo zaidi mbele kwa mbele,mtaongea sana miaka hii hadi 2025
 
Dah asee... Hizi figisu tunazo pandikiziwa hazita tuacha salama..
Wamepata cha kuongelea sasa wataongea hapo hadi mars wafahamu..
Ukweli ni kwamba magufuli kawashika pabaya.

Mwezi mtukufu tufunge kwa kuombea nchi yetu isije ikachafuliwa...

Amiin in-sha-allah mungu atatuaidia tutafanikiwa..

Dedication songs

Tazama Ramani utaona nchi nzuri yenye mito na mabonde mengi ya nafakaa,
Nasema kwa kinywa harafu kwa kufikiri nchi iliyo mashuhuri huitwa tanzaniaa...

And

Taaanzania tanzaniaa nakupenda kwa moyo wotee nchii yangu tanzania
Jina lako ni tamu sanaa
Nilalapo nakuotaa wewee
Niamkapo ni heri mama weee...

Naskia uchungu sana kuona wawatanzania tunajazwa chuki nyakati ambazo tukisha haribu tutakaa kuzkkumbuka the rest of pur life..

Before hujafanya lolote think about your family,your generation.

Mungu tusaidie...
 
Hapo kwny ufalme na demokrasia kumenshawish nkuone kdg unasubjectivity kwny kuchambua mambo.

Be analytical,be objective
Mtu mwenyewe kuandika tu huwezi! Utaelewa kweli nilichokisema? Ati be analytical, be objective. Unaishi kwenye dunia ya karne ya 9 kabisa huko. Hata huelewi kwamba hakuna mtu aliye objective. Labda kama uwe umetengenezwa maabara na kukulia humo humo. Hata hivyo navyo huwezi kuwa objective, mazingira ya maabara yata-influence fikra, maneno na matendo yako.
 
Unasema Tanzania hakuna amani Kwa kuwa hujaishi kwenye Nchi zisizo na amani!

Ukitaka kujua thamani ya Baba muulize Yatima usimuulize mwenye Baba
Usi cherry pick vya kujibu.
Pili, unaweza kusema neno amani kwako linamaanisha nini?
Nimekwambia amani bila haki ni bila bila.
 
Al Jazeera imefungiwa Egypt Kwa Uchochezi Na kazi Yao Ni Uchochezi tu

Walichochea Wa Egypt wamtoe Hosni Mubarak wakafanikiwa, baadae wakachochea Tena Wamisri wamtoe Al sisi Watu wakaingia Mtaani Watu elf 2 wakapigwa risasi za Moto Na kufa japo Al sisi hakutoka Kwao ikawa ajenda

Walichochea Watu Liby, Tunisia, Algeria, Syria Na Maeneo Mengi tu Kwa kigezo Cha kupigania Demokrasia a

Cha kushangaza Nchini kwao hao Aljazeera ( Qatar) wanaongozwa Na Utawala wa Kifalme Na hawajawahi kuzungumzia hizo Demokrasia kwenye Nchi zao

Hivi Sasa Nchi zote kubwa za Kiarabu wameiwekea Vikwazo Qatar Kwa sababu kadhaa mojawapo Ni television Yao ya Aljazeera kuwa ndio Wachochezi wa kubwa wa Vurugu.

Kwa Tanzania Inshallah hawatopata wanachokitaka

Amani kwanza mengine baadae
Kusema ukweli humu jukwaani mzee Pohamba sijawahi kumuelewa abadan. Ima ni moja kati ya wazee wasio na busara kabisa au Dishi itakuwa linayumba kila mawingu yakitanda. Kwa kifupi ni miongoni mwa hasara za taifa letu pendwa.
 
Al Jazeera imefungiwa Egypt Kwa Uchochezi Na kazi Yao Ni Uchochezi tu

Walichochea Wa Egypt wamtoe Hosni Mubarak wakafanikiwa, baadae wakachochea Tena Wamisri wamtoe Al sisi Watu wakaingia Mtaani Watu elf 2 wakapigwa risasi za Moto Na kufa japo Al sisi hakutoka Kwao ikawa ajenda

Walichochea Watu Liby, Tunisia, Algeria, Syria Na Maeneo Mengi tu Kwa kigezo Cha kupigania Demokrasia a

Cha kushangaza Nchini kwao hao Aljazeera ( Qatar) wanaongozwa Na Utawala wa Kifalme Na hawajawahi kuzungumzia hizo Demokrasia kwenye Nchi zao

Hivi Sasa Nchi zote kubwa za Kiarabu wameiwekea Vikwazo Qatar Kwa sababu kadhaa mojawapo Ni television Yao ya Aljazeera kuwa ndio Wachochezi wa kubwa wa Vurugu.

Kwa Tanzania Inshallah hawatopata wanachokitaka

Amani kwanza mengine baadae
Hapo mwisho umejamba! Amani iko wapi? Tanzania unaimba amani? Au ni hofu ya kupigwa kipigo cha mbwa koko?
 
Back
Top Bottom