Aliyewaua wanawake 10 kunyongwa

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,296
160607061607_grim_sleeper_624x351_bbc_nocredit.jpg


Jopo la waamuzi mjini Los Angeles, limeamua kuwa mshukiwa mmoja ambaye alipatikana na hatia ya mauaji, anayefahamika kama 'Grim Sleeper', anapaswa kuhukumiwa kifo.

Lonnie David Franklin Junior alipatikana na hatia mwezi uliopita, ya kuwaua wanawake tisa na msichana mmoja mwenye umri wa miaka kumi na mitano katika kipindi cha miaka ishirini iliyopita.

Franklin junior alifahamika kama Grim Sleeper kwa sababu alitekeleza mauaji mengine baada ya miaka kumi na mitatu.

Aliwalenga wanawake masikini na wasichana wachanga ambao aliwaua na kutupa miili yao kwenye pipa za taka na mitaro ya kupitishia maji machafu.

Mshukiwa huyo sasa atakabithiwa hukumu yake agosti mwaka huu.


Chanzo: BBC
 
Hii iko vizuri. Kama aliuwa binadamu tena kwa makusudi mazima stahiki yake ni kifo. Hata kusubiri hadi Agosti wanamchelewesha sana mbwa huyu akiendelea kula na kuvuta hewa ya bure.
 
Back
Top Bottom