Kibo10
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 11,278
- 8,868
IMANI kubwa ni kwamba mwanamke ni mtu mpole, mkarimu, mwoga na sifa nyingine zinazofanana na hizo. Hata hivyo, wapo ambao wameshafanya matukio ya kutisha mpaka kuweka rekodi ya kipekee. Wafuatao ni 10 ambao wanaaminika ndiyo wenye roho mbaya zaidi kuwahi kutokea kwenye mgongo wa ardhi.
10. MALKIA MARY I
Alizaliwa Februari 18, 1516; alikufa Novemba 17, 1558.
Alikuwa Malkia wa England na Ireland kuanzia mwaka 1553 mpaka kifo chake. Ni mtoto wa Mfalme Henry VIII na Catherine wa Aragon. Malkia Mary alibatizwa jina la Mary wa Damu (Bloody Mary). Alikuwa Mkatoliki na kipindi cha utawala wake, aliua viongozi wote maarufu wa madhehebu ya Protestant, hivyo kusababisha waumini wengi kukimbia nchi.
9. MYRA HINDLEY
Alizaliwa Julai 23, 1942; alikufa Novemba 15, 2002.
Mwanamke huyu akiwa na mwanaume katili, Ian Brady, mwaka 1960 walifanya matukio tofauti ya mauaji, wakilenga zaidi watoto. Kwa ushirikiano wa wawili hao, waliteka watoto watano, wakawabaka na kuwaua. Watatu umri wao ni chini ya miaka 12, wawili miaka 16 na 17. Ushahidi wa video, ulionesha jinsi Myra alivyofanya ukatili kwa watoto hao. Akiwa Mahakama ya Manchester, England, hakuonesha wasiwasi wala kujutia tukio alilofanya. Alifariki dunia kutokana na maradhi ya moyo akiwa gerezani akitumia kifungo cha maisha.
8. ISABELLA WA CASTILE
Alizaliwa Aprili 22, 1451; alikufa Novemba 26, 1504.
Alikuwa Malkia wa Hispania. Pamoja na udikteta wake, Machi 31, 1492, alianzisha mpango wa kudhibiti uasi Kanisa Katoliki (Inquisition). Alimteua Tomas de Torquemada kuwa kamanda wa kusafisha watu ambao siyo Wakatoliki nchi humo. Kipindi hicho, watu wengi wasio Wakatoliki walipoteza maisha, huku Waislam na Wayahudi wapatao 200,000 wakiikimbia nchi hiyo.
7. BEVERLY ALLIT
Alizaliwa Oktoba 4, 1968.
Awali alishtakiwa kwa kuua watoto wanne na kujeruhi vibaya wengine watano. Akiwa na kesi tisa, raia huyu wa Uingereza, alipatikana na makosa mengine ya kuua watoto 13. Wakati tuhuma na ushahidi dhidi yake vikikusanywa, alikamatwa akifanya mauaji ya mtoto mwingine. Kwa sasa yupo gerezani akitumikia kifungo cha maisha jela.
6. BELLE GUNNES
Alizaliwa Novemba 11, 1859; alikufa Aprili 28, 1931.
Ni raia wa Marekani. Aliolewa mara mbili na kuwaua waume zake pamoja na watoto wake wote kwa nyakati tofauti. Alifunguliwa mashtaka ya kuwaua karibu watu wake wote wa karibu, rafiki yake wa kiume, watoto wake wawili wa kike, Myrtle na Lucy. Sababu ya kifo chake haikutajwa ila inadaiwa aliuawa na polisi wa Marekani.
5. MARY ANN COTTON
Alizaliwa Oktoba, 1832; alikufa Machi 24, 1873.
Mwanamke huyu raia wa Uingereza, aliwaua watoto wake nane kwa nyakati tofauti, wote kwa kuwawekea sumu. Aliolewa mara mbili na waume zake wote aliwaua kwa sumu. Vifo vya watoto na waume zake, vinafanana. Alinyongwa baada ya kukutwa na hatia ya kutenda unyama huo.
4. GRISELDA BLANCO
Alizaliwa Februari 15, 1943; alikufa Septemba 3, 2012
Anatajwa kuwa muuza unga mwanamke katili, mwenye uwezo mkubwa kuliko wote kuwahi kutokea katika historia ya dunia. Alitajwa kuua watu zaidi ya 200. Ni raia wa Colombia. Alihamia Marekani na kuunda mtandao ambao uliwezesha kuingiza cocaine nchini humo. Aliuawa Septemba 3, mwaka jana akiwa na umri wa miaka 69. Inadaiwa aliuawa na maharamia wenzake waliokuwa wamedhulumiana.
3. SAMANTHA LEWTHWAITE
Alizaliwa Desemba 5, 1983
Mwanamke huyo anajulikana kwa jina la 'Mjane Mweupe,' inaelezwa yeye pamoja na baba yake, waliwahi kuwa wanajeshi nchini Uingereza. Ni mjane wa Jermaine Lindsay, ambaye alijilipua kwa bomu la kujitoa mhanga Julai 7, mwaka 2005 nchini Uingereza na kuua watu 52. Samantha ni mhusika mkuu wa utekaji wa Jengo la Westgate, Kenya, tukio ambalo lilisababisha vifo vya watu 69 na wengine karibu 180 kujeruhiwa. Vilevile anahusishwa na matukio mengi ya kigaidi yaliyogharimu maisha ya maelfu ya watu.
2. IRMA GRESE
Alizaliwa Oktoba 7, 1923; alikufa Desemba 13, 1945.
Rudi Ujerumani zama za Nazi hususan kipindi cha Vita Kuu ya Pili ya Dunia ndipo utakutana na mwanamke huyu katili. Mwaka 1943 aliteuliwa kuwa kiongozi daraja la pili kwenye kambi ya Ravensbruck, akiwa msimamizi wa wafungwa 30,000, wake kwa wanaume. Aliwanyanyasa wafungwa hao kwa kuwafanyisha ngono na mbwa. Vilevile wengi waliuawa.
ELIZABETH BATHORY
Alizaliwa Agosti 7, 1560; alikufa Agosti 21, 1614
Mwanamke huyu mwenye uraia wa Hungary na Slovakia, anatajwa kuwa mwanamke muuaji wa siri, aliyeua watoto wengi kuliko mwingine yeyote duniani. Sababu ya kufanya mauaji haijulikani ila alikuwa anawachukua mabinti wadogo na kuwadanganya atawaajiri na kuwalipa fedha nyingi lakini matokeo yake alikwenda kuwaua kwa kuwachoma sindano ya sumu. Alipopatikana na hatia, alihukumiwa kifungo cha maisha.