TANZIA Aliyewahi kuwa mkuu wa mikoa mbalimbali nchini, Abass Kandoro afariki dunia Hospitali ya Taifa, Muhimbili

siwezi kujisahau kwani natabua hilo ila walevi wa madaraka hujisahau

Inawezekana kuwa uko sahihi kuwa kuna walevi wa madaraka...lakinipia kumbuka wako walevi wa uchochezi, dharau, udhalilishaji, kutumika na kulalamika kwa kila kitu
 
Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake yeye ndio marejeo yetu...nimesikitishwa sana na kifo chake,,, alikuwa ni mtu very smart. Tunamuombea Mwenyezi Mungu amfutie makosa yake yote na amuingize mahala pema peponi.
 
Imethibitishwa Abass Kandoro hatunaye tena. Source inasema alihamishiwa Hospitali ya Muhimbili mapema leo baada ya hali yake kubadilika katika Hospitali Benjamin Mkapa ya Dodoma.

Kandoro amewahi kuwa katika nafasi ya ukuu wa Mkoa katika zaidi ya Mikoa Sita Tanzania Bara ikiwemo Dar es salaam, Arusha, Mwanza Singida na Mbeya.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipomtembelea Mkuu wa Mkoa Mstaafu, Abbas Kandoro hospitali ya Benjamin Mkapa mjini Dodoma, Aprili 25, 2018.

********************** UPDATES I Aprili 28, 2018 ************************
Rais Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa familia, ndugu jamaa na marafiki wa aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Kandoro.

----
Mwili wa Abas Kandoro ukiingizwa kwenye msikiti wa Manyema kwa ajili ya kuswaliwa kabla ya kuelekea nyumbani kwake Mbweni utakapoagwa na kusafirishwa kuelekea kijiji cha Ihemi mkoani Iringa kwa mazishi yatakayofanyika hapo Kesho.
Alazwe mahala pema peponi
 
Inawezekana kuwa uko sahihi kuwa kuna walevi wa madaraka...lakinipia kumbuka wako walevi wa uchochezi, dharau, udhalilishaji, kutumika na kulalamika kwa kila kitu
Ukisikia mtu anaongelea uchochezi jua ni kati ya wale walioishiwa hoja
 
Kuwa na akiba ya maneno mkuu.
Hakuna wa kukibeza kifo, ndo adui wa mwisho kwa kila binadamu.
Huyu marehemu Abbas Kandoro kwa tuliomfahamu alikuwa mtu mwema, na kumbukumbu hiyo inaishi hata baada ya kifo

Akiba ya maneno huwekewa wale waliojitambua sio nyie wabembeleza vyeo; Magufuli kawakalia kooni wanaume wazima mnashindwa kumwambia ukweli!! Kifo ni adui kwa nyinyi mnaojisahau lakini kwa sisi wengine kifo ni faradhi!!! Umeelewa?
 
Inategemea umaarufu wa nini hata Idi Amini alikuwa maarufu,

umaarufu wa Kandoro ulitokana na utendaji kazi wake uliotukuka tofauti na Bashite unaotokana na ukatili wake.
Na si ukatili tu jumlisha na ulimbukeni na showoff za kumwaga
Kandoro pamoja na kuwa RC lakini alikuwa mtu mwenye roho nzuri. Aliwaongoza watu bila ya kuwanyanyasa kutokana na ufuasi wao wa vyama vya siasa, tofauti na wakuu wengine wengi wa mikoa.

Mungu mwenye huruma amjalie pumziko jema.
Alikuwa mkali sana lakini mwingi wa hekima na busara, mchapa kazi kweli kweli, aliwaamini sana wasaidizi wake huku akimwachia kila mtu kutekeleza majukumu yake, aliijua vyema sana teamwork na ilimsaidia. Pia hakuweka siasa sana kwenye kazi. Awamu hii mambo yamebadilika sana na wasaidizi wote wanaucheza muziki wa mkulu.
 
Hapo wanaccm tunavizia rambirambi wanafamilia wakizembe tu mimi na ndugu yangu gambo tutapotea nazo kama upepo
 
Akiba ya maneno huwekewa wale waliojitambua sio nyie wabembeleza vyeo; Magufuli kawakalia kooni wanaume wazima mnashindwa kumwambia ukweli!! Kifo ni adui kwa nyinyi mnaojisahau lakini kwa sisi wengine kifo ni faradhi!!! Umeelewa?
Wewe ndobhuwezi elewa kitu.
Ungejua nina pesa kuliko mkoloni ungeshangaa.
Tatizobmwafikiri humu mtandsoni wote watoto kama wewe.
Sibembelezi mtu kimaisha.
Lakini zaidi ya yote nakuomba ufe tukulilie vizuri.
Kabla ya yote nikutakie in advance RIP.
 
Back
Top Bottom