Aliyetoroka karantini akamatwa Iringa

Aliyetoroka karantini akamatwa Iringa

The Sheriff

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2019
Posts
747
Reaction score
2,120
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amesema alipigiwa simu na mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Dniale Chongolo na akamjulisha kuhusu mtu aliyetoroka karantini.

Mtu huyo baada ya kutoroka Dar alionekana yuko Iringa, uongozi wa wilaya walishirikiana na jeshi la polishi kujua anapokaa mtu huyo na wamempeleka kantini.

Mtu huyo inasemekana alitoka Norway, na ana siku nne tangu aingie hapa Tanzania. Alikaa karantini siku tatu na kuamua kutoroka.

Nyumba aliyokaa pia iko chini ya karantini na mganga mkuu wa wilaya atawapima wote wanaoishi katika nyumba hiyo.

Kasesela amesema kuna mwingine wiki iliyopita alitoroka karantini ya Tunduma na hadi sasa hawajui yuko wapi, lakini mtu huyo alikuwa Mmalawi.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siwezi kulaumu mtu anaetoroka, hivi unawezaje kumpangia mtu sehemu ya kukaa halafu alipie kwa mfuko wake? wanajuaje kama watu wanaweza mudu hizo gharama za kukaa hoteli.

Isitoshe sehemu ambazo wanatakiwa kufikia watoa huduma udhani kama wapo trained ku deal na namna ya ku limit maambukizi kwenye maeneo yao ya kazi iwapo kuna mtu analogonjwa humo (nina uhakika wahudumu watakuwa wanaingiza vyakula mpaka vyumbani, badala ya kugonga na kuacha milangoni) if anything hizo sehemu zilizotengwa zinaweza kuwa infection centres za baadae kama bado hotel zenyewe zinatoa huduma na kwa raia wengine.

Quarantine mtu anaweza kukaa ata nyumbani kwake na familia yake kuna masharti tu ya kuishi ndani ya nyumba ambayo yeye na familia lazima waheshimu.

Wewe unamwambia mtu akakae hoteli wakati ulipi bill iweje, yaani watu aisee. Ubunifu zero.
 
Okay, let's assume alikuwa anaumwa...
Vipi watu alio safiri nao + maeneo yote aliyo yashika + alipo kula + alipo lala + alipo nunua mahitaji yake + alipo fikia + wenyeji wake + wale wote walio kwenye cycle yake + wale wote walio kwenye cycle ya aliokutana nao..??
 
Huyo ni kichaa
Mwingine kasema "Jamani tuko wote karantini hapa, muda wowote nitakufa, si kwa sababu ya korona, hapana, arosto ya gongo ndiyo itaniua"
 
Umelaliwa jombaa?
Issue sio kuwa na Korona issue ni yeye kukaidi kukaa chini ya uangalizi wa kitabibu.
Aisee acha kunywa banana za kupewa utafanywa vibaya..!!
Hamna bana. Wewee unayequnyer porini ni nani virusi vya korona visikupate?
 
Mtu mmoja mwanama ambaye aliwekwa karantini baada ya kutoka Norway siku nne zilizopita ametoroka karantini na kukamatwa Iringa. Mkuu wa Wilaya Iringa amethibitisha kukamatwa kwa mtu huyo maeneo ya Mtwivila.





 
Back
Top Bottom