Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,703
- 218,236
ZANZIBAR: ALIYELALAMIKIA ZOEZI LA VITAMBULISHO AKAMATWA NA POLISI
Mkazi wa Jundamiti Kiwani Kisiwani Pemba, Abdalla Khamis Muhammed (Tuba) anashikiliwa na Polisi Mkoa wa Kusini Pemba kwa madai ya kufanya uchochezi baada ya kudai kitambulisho cha Mzanzibar Mkaazi.
Mohammed ni miongoni mwa wananchi zaidi ya 2,000 ambao hawajapata vitambulisho hicho kitakachomuwezesha kushiriki katika kufanyiwa uhakiki katika daftri la kudumu la wapiga kura visiwani humo.
Akiwa kwenye kikao ambacho walieleza matatizo wanayokumbana kuhusu vitambulisho hivyo, Muhammed alidai wananchi wengi katika eneo lao hawajapatiwa vitambulisho na kuziomba Mamlaka husika kulichukulia hatua.
Aliongeza, “Vijana wa CCM wako mstari wa mbele kutunyima vitambulisho hivyo, wanataka tupigane ili patokee mauaji lakini lengo sisi ni kushiriki uchaguzi kwa amani ili tupate viongozi tunawataka"
Aidha, Mtendaji wa Mamlaka ya Vitambulisho, Ali Mohammed Ali ameeleza kuwa utoaji wa vitambulisho hauna mlengo wa kisiasa na watu wanaokwenda kama majina yao yapo wanapewa bila ya upendeleo.
Hata hivyo Jeshi la Polisi halijaongea chochote kuhusiana na tukio hilo lakini bado linaendelea kumshikilia Mohammed.