Aliyetoa taarifa juu ya dhuluma ya vitambulisho Zanzibar akamatwa na Polisi

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,348
217,391
ZANZIBAR: ALIYELALAMIKIA ZOEZI LA VITAMBULISHO AKAMATWA NA POLISI



Mkazi wa Jundamiti Kiwani Kisiwani Pemba, Abdalla Khamis Muhammed (Tuba) anashikiliwa na Polisi Mkoa wa Kusini Pemba kwa madai ya kufanya uchochezi baada ya kudai kitambulisho cha Mzanzibar Mkaazi.

Mohammed ni miongoni mwa wananchi zaidi ya 2,000 ambao hawajapata vitambulisho hicho kitakachomuwezesha kushiriki katika kufanyiwa uhakiki katika daftri la kudumu la wapiga kura visiwani humo.

Akiwa kwenye kikao ambacho walieleza matatizo wanayokumbana kuhusu vitambulisho hivyo, Muhammed alidai wananchi wengi katika eneo lao hawajapatiwa vitambulisho na kuziomba Mamlaka husika kulichukulia hatua.

Aliongeza, “Vijana wa CCM wako mstari wa mbele kutunyima vitambulisho hivyo, wanataka tupigane ili patokee mauaji lakini lengo sisi ni kushiriki uchaguzi kwa amani ili tupate viongozi tunawataka"

Aidha, Mtendaji wa Mamlaka ya Vitambulisho, Ali Mohammed Ali ameeleza kuwa utoaji wa vitambulisho hauna mlengo wa kisiasa na watu wanaokwenda kama majina yao yapo wanapewa bila ya upendeleo.

Hata hivyo Jeshi la Polisi halijaongea chochote kuhusiana na tukio hilo lakini bado linaendelea kumshikilia Mohammed.
 
Pohamba,
Wewe utajitetea ila ukweli unaujuwa Mungu yupi uyo anakubana modomo kusema kweli? acha unafiki, Mungu hawezi kamwe kusimama na watu kama nyie mnaotetea maovu muda wote, njaa tu na vyeo vya kidunia vimewalevya miaka nenda miaka rudi ni kuwatesa wapemba kwa sababu ya misimamo yao ya kusimamia haki itendeke.
 
Hii ndio aina ya uonevu tulionao kwetu. Serikali ama wana CCM wamepiga hesabu zao na wameona mtelezo sio mdogo na mwaka huu tunawazika kabisa wala hawato tajwa jina lao tena visiwani kwa hiyo njama kila aina watatumia lakini tunawaambia kuwa hiyo sio dawa. Mchezo tumemaliza nyinyi subirini tarehe ya kura tu. Munafikiri kuwa nyanyasa raia ndio mutashinda?. Yaguju. Hamutoki mwaka huu. Na kama hamutujui basi subirini fimbo ya kumaliza wanga.
 
Sasa sijajua kama mkaazi husika amevunja sheria gani ya inchi mpaka kuonekana ametoa maneno uchochezi kwa kutaka kufahamu kwa nn wao hawwjapata hivyo vitambulisho ila pia kama ametaja UVCCM vijana wao kua ndo kikwazo basi ahojiwe kww hilo na ushaidi wa neno lake autoe ila kama amesema hayo maneno kwa kuhisi tu basi hiko ni kosa jinai kushutumu bila uthibitisho' Kila mtu awe makini na mienendo yake.
 
Hivi hili linchi letu limekuwa na laana gani?? Kila siku utasikia foul nyingi hasa ktk mambo ya uchaguzi.

Laana kwa matendo ya wizi wa kura mke wa nkurunzinza kapelekwa kenya akiwa na korona.

Namuomba Mungu wote wenye mpango wa kuiba kura kyk uchaguzi huu awatunuku maradhi ya korona ba ikibidi wapate kabisa ukimwi
 
Sijaona kibaya chochote alichokisema huyu mtu hata kustahili kuchukuliwa na polisi....

Ni malalamiko ya kawaida na yanapaswa kujibiwa kikamilifu na wenye mamlaka; mathalani;

1. Je, kweli kuna watu 2,000 au idadi yoyote wamejiandikisha na lakini hawajapewa shahada (ID) zao mpaka muda analalamika huyu mtu?

2. Kama ndivyo, ni kwanini? Je, hawastahili? Machine za kufyatulia ID ni mbovu?

3. Jibu la swali la 2, linazaa swali hili;

Kwamba, kama kuna ubovu mashine, kwanini waliojiandikisha kwa muda na siku zile zile na hawa wanaolalamika wanapata na wengine hawapati?

4. Halafu huyu Ally Mohammed Ally, Mtendaji wa Mamlaka ya Vitambulisho Zanzibar badala ya kujibu hoja analeta siasa...

Haiingii akilini kwa kusema tu eti;

"......utoaji wa vitambulisho hauna upendeleo wa kisiasa, na yeyote ambaye jina lake limo anapewa kitambulisho...."

Hii kauli haijibu maswali ya wanaolalamika..

å Kwanza kama kiongozi inapaswa kujiridhisha kuwa, kweli kuna watu 2,000 wa eneo hilo wanastahili na lakini hawana Voters ID zao?

å Je, wana sifa na walijiandikisha?

å Kwanini mpaka muda huo hawana Voters ID zao?

å Kama kigezo ni "....kuwa kwenye orodha...." Kama asemavyo Ally M. Ally; Je, amajiuliza kwanini hawa wanaolalamika hawako kwenye orodha? Kwanini walalamike wakati hawako kwenye orodha? Wana sifa ya kupiga kura? Why...,why....

å Je, ni kweli ZEC imeweka watu wa CCM kuamua hatima ya watu wengine ktk upigaji kura?

å ZEC, inategemea nini kama wanakubali kupachikiwa vijana wa CCM kufanya shughuli nyeti kama hii kuhusu uchaguzi?

Wao si wanataka Chama chao CCM kishinde?

Si watafanya kila mbinu kujihakikishia hilo ikiwa ni pamoja na hiki kinachoendelea huko Zanzibar?

Hii ni shida.

Wazanzibari wasipokuwa makini, wajue kuwa dhambi ya ghasia na umwagaji damu iko milangoni pao. Wanapaswa kuishinda....!!
 
Hii ndio aina ya uonevu tulionao kwetu. Serikali ama wana CCM wamepiga hesabu zao na wameona mtelezo sio mdogo na mwaka huu tunawazika kabisa wala hawato tajwa jina lao tena visiwani kwa hiyo njama kila aina watatumia lakini tunawaambia kuwa hiyo sio dawa. Mchezo tumemaliza nyinyi subirini tarehe ya kura tu. Munafikiri kuwa nyanyasa raia ndio mutashinda?. Yaguju. Hamutoki mwaka huu. Na kama hamutujui basi subirini fimbo ya kumaliza wanga.
Mtatumia mbinu gani wakati wao wanaiba kura??
 
Back
Top Bottom