Aliyetaka kuuza albino mzimamzima jela miaka 17 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aliyetaka kuuza albino mzimamzima jela miaka 17

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by MziziMkavu, Aug 21, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 21, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Thursday, August 19, 2010 11:41 AM
  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mwanza, imemuhukumu kifungo cha miaka 17 jela, au faini ya shilingi milioni 80 Nathan Mtei (28) baada ya kupatikana na hatia ya kumsafirisha na kumtorosha mlemavu wa ngozi kwa lengo la kumuua.

  Hukumu hiyo ilitolea jana mbele ya Hakimu Mkazi, Angelo Rumisha, huku shauri hilo likiongozwa na Mwanasheria wa Serikali, David Kakwaya.

  Awali akisoma hati ya mashitaka kabla ya hukumu hiyo, ilidaiwa kuwa mshitakiwa alitenda makosa hayo Agosti 15 mwaka huu, mkoani Mwanza kwa lengo la kudhamiria kumuua Robinson Mtwana (20) [albino] ambaye ni raia mwenzake wa nchini Kenya

  Kakwaya alidai kuwa, kitendo cha kusafirisha binadamu kutoka sehemu moja kwenda nyingine ni kosa la kisheria na ni tendo la kinyama na kuiomba mahakama itoe adhabu kali dhidi ya mshitakiwa huyo .

  Kabla ya hakimu kutoa hukumu alimtaka mshitakiwa ajitetee ili asimpe adhabu kali na kuiomba mahakdfama kamda ifuat avyo.

  “Naomba mahakama iruhusu kesi hiyo ikasomewe Kenya” pia naomba mahakama inisamehe inisamehe kwa kuwa anahisi mganga wa kienyeji alichangia kumshawishi kutenda makosa hayo.

  ALiongeza kwa kuiomba mahakama kuwa “ nina familia ambayo inanitegemea”

  Hivyo baada ya Kwakwaya kumaliza Hakimu alitoa adhabu kwa mshitakiwa ambapo alisema kwa kosa la kwanza atatumikia miaka tisa jela au kulipa faini ya Shilingi milioni 80 na kwa kosa la pili atatumikia jela miaka minane.

  Na kuongeza kuwa endapo mshitakiwa atalipa faini adhabu hiyo itabadilika .

  Pia Hakimu alimpa siku 45 mshitakwia huyo kukata rufaa ndani ya mahakamda kuu endapo hajaridhishwa na hukumu iliyotolewa dhidi yake.

  Source: NIFAHAMISHE Tanzania news portal .: Habari za Tanzania :.

  Hiyo ndio Tanzania yetu Mtu anauzwa kaam watu wauzao Ng'ombe? Kasheshe kweli bongo yetu.
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Aug 22, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Albino aliyenusurika kuuzwa arejeshwa Kenya


  Sheilla Sezzy,
  Mwanza

  JESHI la Polisi mkoani Mwanza jana limemsafirisha mlemavu wa ngozi (Albino) Robinson Mkwama mpaka mpakani mwa Kenya baada ya kunusurika kuuzwa na Nathani Mtei raia wa Kenya.

  Akizungumza na Mwananchi Mkuu wa Upelelezi mkoani Mwanza, Deus Kaizilege Msimeki alisema polisi wamelazimika kumsafirisha Albino chini ya uangalizi maalumu wa polisi mpaka mpakani ili kumhakikishia usalama wake.

  Alisema kulikuwa hamna haja ya kuendelea kumweka Mwanza kutokana na kesi yake kuisha mapema baada ya aliyekuja kumuuza kuhukumiwa kifungo cha miaka 17 jela kutokana na makosa mawili aliyotenda.
  Aliendelea kueleza kuwa Albino huyo alisindikizwa na polisi wa Tanzania hadi mpakani Sirari na atakabidhiwa kwa Wizara ya Uhamiaji ya Kenya na kwamba wizara hiyo, itakuwa na jukumu la kumsafirisha hadi nyumbani kwao.

  Alisema tatizo la kuuza viungo vya albino limekuwa kutokana na soko kubwa kutangazwa na watu wenye imani mbaya na walemavu wa ngozi na aliwataka wananchi wote wa Tanzania na hasa Kenya kuwa makini na matapeli hao wenye imani mbaya.

  Awali Mtei alikuja Tanzania kwa mara ya kwanza Juni mwaka huu na kuonana na mganga mmoja wa jadi(msiri wa polisi) na kumueleza kuwa anauza viungo vya albino na hivyo kuandaliwa mtego baada ya msiri huo kutoa taarifa polisi.

  Source: Albino aliyenusurika kuuzwa arejeshwa Kenya
   
 3. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #3
  Aug 27, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  This is funny.

  Kifungo cha miaka 17 tu kwa jaribio la kuua!
   
Loading...