Aliyeshauri ofisi za mabasi ya mwendokasi (UDART) zijengwe Jangwani akamatwe mara moja

Au hizi ofisi na zenyewe zilijengwa na wananchi. Maana serikali ndo kiongozi wa kupinga ujenzi sehemu hatarishi kama hizo na zinafahamika toka mda mrefu, sijui watapatanje nguvu ya kuwalaumu wananchi waliojenga kwenye bonde hilo kama na serikali inabariki ujenzi kwa kujenga ofisi hapo.
 
Huu mradi ulifadhiliwa na WB si pesa ya Serikali directly ni mkopo, sasa unakopaje unajenga kitu kibovu!? Yule Mkuu wa TANROADS jana kasifiwa na kapewa Jina la Fly Over wakati alipaswa kuwa KEKO kwa kuitia nchi hasara kubwa kwa Barabara hii mbovu...kama mjini tena Dar hivi, huko Porini inakwaje kwenye kurekebu michoro....
 
Serikali ya UKAWA ya jijini DSM ijiepushe sana na usumbufu kwa raia wanaotumia kituo cha mabasi ya mikoani - UBUNGO unaosababishwa na ujinga uliofanywa Jangwani .

Nakala kwa Isaya Mwita
 
Jangwani ni sehemu salama ya kujenga. Kwenye bahari, hotel zimejegwa sembuse hapo funken maji yanapita tu
 
Hivi unaweza kujikamata? Wakandarasi walishauri daraja kubwa la juu lijengwe ili lipitishe maji na bajeti ilitengwa lakini pesa zikapigwa unataka ajikamate thubutu? Uliwahi msikia akiongelea kuhusu huu ufisadi uliofanywa wa huu mradi wa mwendokasi?
Sijaelewa mwishoni mkuu.. Uliwai msikia nani huyo?
 
Kwa namna yoyote ile huyu mtu hakuwa na nia njema , Jangwani kwa miaka kadhaa imefahamika kama mkondo wa Bahari , sasa kwa mtu yeyote mwenye akili timamu ama mwenye nia njema asingeleta ushauri duni wa kiwango kile .

Nasema akamatwe ahojiwe na nina hakika mengi yatafumuka .
Wajinga na wanaotakiwa kukamatwa ni waliofuata ushauri wake.
 
@kapalamsenga,
Shida ya nchi hii kwanza ni ujinga wa watanzania, wote nyie mmeingia CHAKA, shida ya jangwani ni uhusiano Kati ya serikali kuu na manispaa zake, jangwani ilikuwa haijai maji, maji hayaletwi na uamuzi wa serikali kujenga pale station ya dart, bali inaletwa na manispaa, hili ni eneo I la chini, lakini kila siku linapungua kwa nusu kwa sababu manispaa imeruhusu makazi na watu wanajaza kifusi kujenga nyumba, hii inafanyika kweupe kabisa upande wa ilala na kigogo, na hata timu pendwa nayo inajaza eneo la storm surge kujenga uwanja w mpira na watu wanashangilia, halafu kesho mnapinga Kelele kuilaumu serikali, sii kweli, ni ujinga wetu tuu, tumejaa umbumbumbu hatuelewi kinachotokea nini
 
Sasa wale waliokuwa wanajenga pale , ambao ndio hasa wanaopata hasara , hili unalolijua wewe wao hawakulijua ?
 
Back
Top Bottom