Aliyesababisha kifo cha Salome Mbatia akamatwa

mfanano wa mambo bado unanipa hisia kwamba kuna aina fulani ya uendeshaji wa nchi yetu kimafia.
chenge kagonga Bajaji na abiria wawili waliokuwemo kwenye hiyo bajaji ambayo kiuhalisia iliharibika kabisa wakafariki dunia. Lakini mpaka leo sijui kama Dereva wa ilie Bajaji keshapatikana!

Dereva wa bajaji ya Chenge na ile ajali iliyomuua mbatia wako wapi?
 
inabidi tuwe waangalifu sana siku hizi maana mbinu chafu zimekuwa jambo la kawaida
nadhani usalama wa taifa walione hili na kulifanyia kazi kwani kuna plumbing zinafanyika gizani gizani tu.
ah
 
inabidi tuwe waangalifu sana siku hizi maana mbinu chafu zimekuwa jambo la kawaida
nadhani usalama wa taifa walione hili na kulifanyia kazi kwani kuna plumbing zinafanyika gizani gizani tu.
ah

Usalama wa Taifa??
 
Vipi umeogopa hapo?
nimewataja yes kwa kuwa wapo kimya mno kana kwamba hawapo.
Idara iboreshwe
wapelekwe watalaam kule na si wacheza kungfu pekee.
 
Vipi umeogopa hapo?
nimewataja yes kwa kuwa wapo kimya mno kana kwamba hawapo.
Idara iboreshwe
wapelekwe watalaam kule na si wacheza kungfu pekee.

sijaogopa ila nilikuwa najiuliza kama wameshindwa kujua kama hapo Mabibo kuna nini kinaendelea DECI ndiyo wataweza mambo makubwa yenye harufu ya umafia kama haya.

believe me ndg yng hatuna usalama wa taifa ila tuna wavaa suti na wacheza Kung fu wanaongozana na viongozi wetu (watawala?) kwenye misafara yao.
 
Bora hata wangekuwa wanaishia kufanya shughuli hizo tu, tatizo ni kwamba badala ya kuwa usalama wa taifa wamegeuka kuwa 'usalama wa mafisadi'!
 
Aliyesababisha kifo cha Salome Mbatia akamatwa

na Mwandishi wetu

IMG_8645.JPG

HATIMAYE Dereva wa gari aina ya Fuso lenye namba za usajili T299 AFJ Daudi Mangulla (28), anayedaiwa kusababisha kifo cha aliyekuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Salome Mbatia, amekamatwa na polisi. Akithibitisha kukamatwa kwa dereva huyo aliyekuwa akitafutwa kwa zaidi ya miaka mitatu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Evarist Mangalla, alisema Daudi alikamatwa jana kwenye kituo cha mabasi ya makambako mjini hapa.
Alisema, kukamatwa kwa dereva huyo kumetokana na msaada ulioonyeshwa na wananchi kupitia dhana ya polisi jamii na ulinzi shirikishi.
"Tangu kutokea kwa ajali hiyo, Oktoba 24 mwaka 2007 saa 10 jioni eneo la Kibena barabara kuu ya Njombe -Makambako, dereva huyo alikimbia baada ya ajali hiyo iliyosababisha vifo vya watu watatu," alisema kamanda huyo.
Alisema, siku ya tukio fuso lililokuwa likiendeshwa na Daudi, liligonga gari lenye namba za usajili T 724 AGZ Nissan Patrol alilokuwemo marehemu Mbatia huku akiwataja wengine waliokufa katika ajali hiyo kuwa ni Anakleti Mbogela (42) na utingo wa Fuso hilo Castory Kulangwa (22).
Alisema dereva huyo alijificha porini na baada ya kuona mambo yamekuwa kimya aliamua kujitokeza na kuendelea na shughuli zake eneo la Mjimwema Makambako na kubainisha kwamba wakati wowote kuanzia sasa dereva huyo atafikishwa mahakamani.
 
Back
Top Bottom