Aliyeporwa "Range" na Makonda alipuka, atangaza kwenda Mahakamani

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,650
218,105
Hii ndiyo Taarifa iliyoripotiwa na Gazeti la Raia Mwema kwa siku ya leo, Agosti 31, 2022 kwamba yuko Mtanzania mwenzetu ambaye amemwangukia Rais Samia Suluhu Hassan, ili atie mkono wake kutokana na dhuluma aliyofanyiwa na Makonda aliyekuwa RC wa Dar es Salaam ya kuporwa gari lake la kisasa aina ya Range Rover.

Taarifa ya gazeti hilo inaonyesha kwamba kwenye sakata hilo la uporaji, yuko pia mtuhumiwa mwingine aliyejulikana kwa Jina bandia la LE MUTUZ, anayedaiwa kuwa ni mtoto wa Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, John Sigwemisi Malecela.

FbcB7ivWAAA2SWA.jpg

MFANYABIASHARA Patrick Christopher Kamwelwe mkazi wa New York nchini Marekani ameshusha tuhuma nzito dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Tuhuma hizo zinahusu madai ya kumpora gari lake aina ya Ranger Rover na kuibandika namba za RC DSM (Mkuu wa mkoa Dar es Salaam) kipindi akiwa kwenye wadhifa huo.

Kamwelwe ambaye pia anajulikana kwa jina maarufu kama PCK amedai Makonda anaendelea kuitumia gari hiyo hata baada ya kuondolewa madarakani licha ya kwamba si mali yake halali.

Akizungumza na Raia Mwema katika mahojiano maalum Kamwelwe ambaye ni mzaliwa wa Mpanda mkoani Katavi aliyekuwa akiishia jijini Dar es Salaam kabla ya kukimbilia Marekani kutokana na vitisho, amedai kwamba baada ya kufuatilia ili arejeshwe gari hiyo nyeusi yenye thamani ya Sh milioni 220, ndipo vitimbi na vitisho Vilipoanza na kubambikiwa kesi ya jinai kwa kumiliki mali haramu.

Alidai kutokana na tuhuma hizo Juni 2017 alifikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu huku akaunti zake za benki pamoja na mali zake zikishikiliwa hadi sasa.

GARI ILIVYOKWAPULIWA
Kamwelwe ambaye awali alikuwa mfanyabiashara wa magari, msanii wa Bongofleva na promota wa muziki, alisema mwaka 2017 alifuatwa na mtoto wa Waziri Mkuu mstaafu, Samwel Malecela, William Malecela maarufu kwa jina la Lemutuz na kumueleza kuwa Makonda...

Chanzo : Raia Mwema
 
Hii ndiyo Taarifa iliyoripotiwa na Gazetti la RaiaMwema kwa siku ya leo , kwamba yuko Mtanzania mwenzetu ambaye amemwangukia Mh Rais Samia , ili atie mkono wake kutokana na dhuluma aliyofanyiwa na Makonda aliyekuwa RC wa DSM ya kuporwa gari lake la kisasa aina ya RANGE ROVER .

Taarifa ya Gazeti hilo inaonyesha kwamba kwenye sakata hilo la uporaji , yuko pia Mtuhumiwa mwingine aliyejulikana kwa Jinala bandia la LE MUTUZ , anayedaiwa kuwa ni Mtoto wa Waziri Mkuu wa Zamani wa Tanzania , John Sigwemisi Malecela

Chanzo : RaiaMwema
Wewe na hilo Gazeti nawaambieni kuwa kwa Tanzania hii ya sasa hakuna wa Kumkamata na Kumfunga Paul Makonda.

Na wala msipoteze muda Wenu katika hili na huwa nawashangaa kweli kweli Kutwa mnavyohangaika hivi na Sukari ya Mzanzibari.
 
Hii ndiyo Taarifa iliyoripotiwa na Gazetti la RaiaMwema kwa siku ya leo , kwamba yuko Mtanzania mwenzetu ambaye amemwangukia Mh Rais Samia , ili atie mkono wake kutokana na dhuluma aliyofanyiwa na Makonda aliyekuwa RC wa DSM ya kuporwa gari lake la kisasa aina ya RANGE ROVER .

Taarifa ya Gazeti hilo inaonyesha kwamba kwenye sakata hilo la uporaji , yuko pia Mtuhumiwa mwingine aliyejulikana kwa Jinala bandia la LE MUTUZ , anayedaiwa kuwa ni Mtoto wa Waziri Mkuu wa Zamani wa Tanzania , John Sigwemisi Malecela

Chanzo : RaiaMwema
Bado tu wanaye..!
 
ai agrii, wani dei zei wili eventuali geti im. Ai gesi zei aa angri, endi wili trai ageni endi ageni antili zei geti im. Ifu noti nau zen weni ze kaming presidenti izi ini ofisi.
They will get him within this administration.
I am reliably told Makonda lives like an antelope. Always on the look out.
7baya has now been behind bars for over an year now.
 
They will get him within this administration.
I am reliably told Makonda lives like an antelope. Always on the look out.
7baya has now been behind bars for over an year now.
Kule pwani kuna usemi, kama umewahi kumuona mwanaume katoka chumbani kwa mama kavaa taulo muite baba.
Ukichemsha bongo vizuri utaelewa post ya hapo juu iliyotaja sukari!
 
Back
Top Bottom