Mama TZ amefananishwa na samaki mkubwa lakini watu wabaya wakamtoa sehemu aliyopaswa kuwa yaani baharini kisha akajikuta yuko nchi kavu. Sasa inajulikana kabisa kuwa huko nchi kavu hawezi kuendelea kuwa hai, atakufa muda si mrefu. Kwa hiyo wenye dhamana ya kuhakikisha uhai wake inabidi wasaidiane uli kumrudisha mahali pake yaani baharini. Lakini nkwa bahati mbaya ni mtu mmoja tu mwenye dhamana ndiyo anajitahidi kujaribu kumsukuma arudi majini, wenzake wote wa kijani wamekula kona wakamwachia MZALENDO mmoja tu anahangaikia uzima wa mama TZ. Hii kazi ni kubwa sana na inavyoonekana hataiweza peke yake. Hawa wengine wanaodai anatumia nguvu bila akili wameshindwa kuyasoma mazingira vizuri wakidhani anatumia nguvu bila akili ndio maana hajaweza kumrudisha mama TZ mahali pake. Ukweli ni kwamba anaonekana kuelemewa na kazi ya kumrejeza mama TZ mahali pake si kwa sababu hatumii akili, bali kwa sababu ameachiwa kazi hiyo peke yake na umoja umekosekana, wakati inafahamika kuwa umoja ni nguvu. Suluhisho ni kuwahimiza wote wenye dhamana kurudisha moyo wao wa uzalendo ili gurudumu la maendeleo kuelekea uchumi wa kati lisukumwe na wote pasipo kumwachia mtu mmoja. Hawa wanaoteta pia ni rtatizo maana wameshindwa kuisoma hali halisi.