Aliyemwelewa Kipanya Hapa Atie Neno!

nyumbatatu

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
1,076
938
Siku zote vikaragosi vya mchoraji Masood(Kipanya) hubeba ujumbe mzito, Na Ni burudani Sana ukimwelewa. Mimi leo nimetoka kapa, lakini sijakubali kupunjika ndio maana nikualikeni mlioelewa hii twende sawa. Karibu
wp_ss_20170924_0001.png
 
kuna jamaa kavaa green anasukuma DUDE kwa MAGUVU, jamaa wanajadiliana kwa kumteta kuwa HEKIMA pia itumike ktk kusukuma dude!

Anamaanisha ili kusukuma dude, tunahitaji AKILI na HEKIMA, sa yule green kule hana vyote. Ana MAGUVU tu! Na pamoja na MAGUVU yake, dude haliendi!
 
Halafu Ni Kama vile dude limetoka kwenye maji kwa hiari yake vile.
 
hao wenye nyekundu ni wale wanaopata matibabu nairobi,wanamteta MUNGU MTU anavyotumia nguvu kuipeleka TANZANIA mbele...badala ya kutumia akili na busara,tena TANZANIA yenyewe ni samaki mkubwa na BAHARI haipo mbali,kiasi angetumia akili samaki angeingia tu automatic majini na kusonga mbele..
 
Yaani nchi imetoka nje ya misingi yake,lakini ajabu waliopewa dhamana wanatumia nguvu nyingi bila kutumia akili na hekima kuirudisha kweny mstari..

Mimi nimemuelewa hivyo.
Nashukuru mkuu nilikuwa nimeelewa ila umenielewesha zaidi
 
Kuna papa, pembeni kuna maji/ bahari kisha kuna mtu anahangaika kusukuma.

Kisha unahangaika kusukuma wakati ukimrejesha majini/ baharini utakua umezuia matumizi ya nguvu zisizo na sababu.

Sanaa ndivyo ilivyo kila mtu atatoa jibu tofauti na wote mpo sawa.
 
hao wenye nyekundu ni wale wanaopata matibabu nairobi,wanamteta MUNGU MTU anavyotumia nguvu kuipeleka TANZANIA mbele...badala ya kutumia akili na busara,tena TANZANIA yenyewe ni samaki mkubwa na BAHARI haipo mbali,kiasi angetumia akili samaki angeingia tu automatic majini na kusonga mbele..
Umetisha sana
 
Uko vizuri mkuu..
 
Yaani nchi imetoka nje ya misingi yake,lakini ajabu waliopewa dhamana wanatumia nguvu nyingi bila kutumia akili na hekima kuirudisha kweny mstari..

Mimi nimemuelewa hivyo.
Hili uliloliandika lipo karibu zaidi na kilichooneshwa na katuni ya Mosoud. You're Great thinker bro, Good
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom