Aliyemuibia Malima ana umbo la kitutsi; Juu mwembamba chini mnene | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aliyemuibia Malima ana umbo la kitutsi; Juu mwembamba chini mnene

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by C.T.U, Mar 13, 2012.

 1. C.T.U

  C.T.U JF-Expert Member

  #1
  Mar 13, 2012
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 4,708
  Likes Received: 1,210
  Trophy Points: 280
  Na Mwandishi Wetu, Morogoro | Global Publishers

  WIZI kwenye chumba cha Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Kighoma Malima (pichani) mwishoni mwa wiki iliyopita katika Hoteli ya Nashera mkoani Morogoro, umedaiwa kufanywa na mwanamke anayejiuza, maarufu kama changudoa.

  Vyanzo vyetu mbalimbali mjini Morogoro vimedai kuwa mwanamke huyo siku hiyo ya tukio alionekana maeneo ya hoteli hiyo ambapo inadaiwa aliweza kuagiza soda na kunywa kisha kuondoka hotelini hapo na baada ya muda mfupi alirejea.

  Habari zinasema, mwanamke huyo haikujulikana aliondokaje katika hoteli hiyo, hivyo watu kumlenga yeye kuwa ndiye mwizi baada ya habari za naibu waziri kuibiwa fedha na mali mbalimbali zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 23 kuzagaa.

  Mpasha habari wetu mmoja amedai kuwa mwanamke huyo ambaye amekuwa akihusishwa na wizi pamoja na utapeli mbalimbali mkoani hapa, amekuwa akionekana katika baadhi ya hoteli kubwa.

  “Kuna jamaa yangu amewahi kuibiwa katika hoteli moja na mwanamke huyo tunayedhani kuwa kamuibia Waziri Malima. Inasemekana ana ‘funguo malaya’ na hata dawa ya usingizi.

  “Siku aliyoibiwa jamaa yangu mwanamke huyo aliingia katika chumba chake akajifanya kuomba simu, baadaye jamaa yangu akajikuta amelala fofofo, akakombwa kila kitu. “Nadhani alitumia dawa ya usingizi, sasa sijui mazingira ya chumba na hoteli aliyolala naibu waziri yalikuwaje,” kilisema chanzo hicho.

  Wajihi wa mwanamke huyo ambaye inadaiwa ana kundi la uhalifu ambalo hudiriki kuvunja sehemu wanayodhani ina mali au fedha, ni mweupe, mrefu, ana umbo mithili ya wanawake wa Kitutsi, juu mwembamba, chini mnene na inasemekana hupendelea kutembelea pia jijini Dar es Salaam na Mwanza.

  Mwandishi wetu alizungumza na mlinzi mmoja wa Hoteli ya Nashera na kumuuliza kama alimuona mwanamke yeyote siku hiyo ya tukio hotelini hapo ‘akimzengea’ waziri lakini akakataa kuzungumzia suala hilo.

  Aidha, Naibu Waziri Malima alipozungumza na gazeti hili alisema hamjui mtu aliyemuibia na hakuwahi ‘kuzengewa’ na mwanamke yeyote siku hiyo.

  ALIYEIBA ALIKUWA PEKUPEKU
  Naye Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Morogoro (RCO), Hamisi Selemani ambaye siku ya tukio alikuwa akikaimu nafasi ya kamanda wa mkoa, alisema uchunguzi wao wa awali ulibaini kuwa aliyeiba hakuwa amevaa viatu, yaani alikuwa pekupeku.

  “Nyayo za mtu huyo zilionekana nje ya chumba namba 125 alichokuwa amelala naibu waziri,” alisema Kamanda Selemani.

  ALICHOSEMA RPC
  Alipoulizwa juzi na gazeti hili juu ya changudoa huyo anayedaiwa kufanya tukio hilo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, (RPC) Adolfina Chialo alisema hajajua kama changudoa huyo anahusika lakini akakiri kuwa tayari watu watano wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo.

  “Kuna vitu vya Naibu Waziri Malima vimepatikana isipokuwa fedha lakini tunaendelea na uchunguzi wa tukio hilo,” alisema.

  Aliwataja waliokamatwa kuwa ni Maneno Juma (25), Juma Athumani (23) ambao ni wakazi wa Chamwino, Kwa Mgulasi, Ramadhani Athumani (24) na Abdallah Hassan (25) wakazi wa Mafiga.

  Kamanda alimtaja mwanamke Halima Ramadhani (37), mkazi wa Kichangani Morogoro ambaye alisema alikutwa na simu tatu na Kompyuta mpakato (Lap Top), mali za Naibu Waziri Malima.

  MALI ALIZOIBIWA
  “Tumefanikiwa kukamata mali za waziri kwa asilimia 90 nikimaanisha kwamba vitu vyote vimepatikana isipokuwa fedha,” alisema Kamanda Chialo bila kufafanua zaidi.

  Malima alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kubembelezwa kwa saa tano, alitaja mali alizoibiwa na thamani yake katika mabano kuwa ni Kompyuta mpakato tatu aina ya Dell (Sh. Milioni 5.6), Digital Recoder mbili na head phone zake (Sh. Milioni 1), simu tatu aina ya Nokia S6 ( Sh. 500,000), Nokia E200 (Sh. 250,000) na Blackberry ambayo hakutaja thamani yake.

  Vingine ni pete mbili za madini ya fedha, fedha taslimu Dola za Kimarekani 4,000 (Zaidi ya shilingi milioni 6.3), shilingi milioni 1.5, kadi mbili za benki, mabegi matatu ya nguo na nyaraka mbalimbali za serikali, zote zikiwa na thamani ya jumla ya shilingi milioni 23.25.

  CHANZO: http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/aliyemuibia-waziri-malima-ni-changudoa
   
 2. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #2
  Mar 13, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Kudadeki, "MWENYE UMBO NAMBA NANE ALIMCHANGANYA" waziri...
  Ushauri wa bure kwa Polisi wawaachie hao walugaluga waliowakamata kwani hawana hatia na wamtafute muhusika halisi ambaye ni changudoa
   
 3. M

  Massenberg JF-Expert Member

  #3
  Mar 13, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 1,173
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Tuichambue hii habari na tukio lenyewe kama ifuatavyo:

  1 - Inaonekana mwizi alikuwa ndani ya chumba cha huyu fidhuli na si nje.

  2 - Kutokana na maelezo ni kwamba nyayo zilionekana ambazo inaelekea ni za mtu mmoja; lakini je, ina maana nje ya chumba cha bei yote hiyo mwenye hoteli ameshindwa kusakafia na kuacha mchanga na vumbi mpaka nyayo zionekane? Kama kuna sakafu, je, inawezekana miguu ya huyo mwizi ilikuwa imelowa mpaka aache alama za nyayo?

  3 - Idadi ya vitu vilivyoibiwa ni kubwa kulinganisha na uwezo wa mtu mmoja kuvibeba kwa mara moja; je, huyo mwizi alirudia hivyo vitu, na kama alirudia ni wapi alikoegesha gari au wenzie walijificha umbali gani kumuwezesha kurudia vitu kama upo uwezekano kuwa alirudia?

  4 - Miongoni mwa vilivyoibiwa ni mabegi ya nguo; je, mwanamke mwizi katika hali ya kawaida atahitaji kubeba mabegi ya nguo za kiume ambazo si mpya?

  5 - Huyo mwanamke kwenye Defender inasemekana amekutwa na simu tatu na laptop, ingawa habari haisemi ni laptop zote au moja. Je, katika hali ya kawaida, inawezekana kweli hao wanaume wote waliokamatwa waondoke na vitu vingine kama hela, kadi za benki, pete na nguo halafu wamuachie mwizi mwenzao wa kike simu za bei mbaya na laptop?

  6 - Je, nyayo zilizoonekana zimepimwa na kufanana na za yeyote kati ya hao waliokamatwa?

  7 - Ulinzi katika hoteli hiyo ukoje mpaka vitu vyote hivyo viibiwe, dirisha livunjwe, mtu akimbie na kuacha nyayo - yote haya bila hata walinzi kusikia chochote?

  8 - Upo pia uwezekano kwamba aliyekuwepo mle chumbani na Malima ni mwanaume ndiyo maana pengine mabegi yake ya nguo yaliibiwa. Kusema kuwa Malima ana mke hakumaanishi yale mambo ya nanihii hayawezekani, maana wapo waliooa ili kujificha wakati kumbe huwa wanashughulikiwa na wanaume wenzao.

  Haya ni ya msingi kuzingatia.
   
 4. PakiJinja

  PakiJinja JF-Expert Member

  #4
  Mar 13, 2012
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 834
  Likes Received: 329
  Trophy Points: 80
  Kwa umbo hilo huyo atakuwa ni nguvu tu. (samaki mtu)
   
 5. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #5
  Mar 13, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Monday, 12 March 2012 21:51

  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  Fidelis Butahe

  KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Adolphina Chialo amesema kuwa aliyemwibia Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima vitu mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya Sh23.25 milioni katika hoteli ya Nashera mkoani Morogoro sio mwanamke.

  Kamanda huyo alisema mtuhumiwa aliyekamatwa na polisi alipohojiwa alieleza kuwa vitu alivyoiba alivihifadhi nyumbani kwa mama yake mdogo na kwamba waziri Malima hakuwa na bunduki aina ya SMG, kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.

  Naibu Waziri Malima alikumbwa na mkasa huo uliozua maswali mengi saa 10 alfajiri ya kuamkia Machi 9, mwaka huu baada ya watu kueleza sababu tofauti za wizi huo.Baadhi ya watu walidai kuwa Waziri huyo alikuwa na mtu chumbani anayesaidikiwa alitoroka na vitu hivyo na wengine walidai kuwa aliibiwa na mtu aliyepitia dirishani baada ya kufungua dirisha.

  Chialo aliliambia Mwananchi jana kuwa mmoja wa watuhuniwa wa tukio hilo alipobanwa alieleza wazi kuwa vitu alivyoiba alivihifadhi kwa mama yake mdogo."Unajua haya mambo yanakuzwa lakini hayana ukweli wowote, yupo mtu mmoja ambaye baada ya kumbana alieleza kuwa vitu alivyoiba alivihifadhi kwa mama yake mdogo," alisema Chialo.

  Akizungumzia taarifa kuwa Waziri Malima alikuwa na SMG katika chumba chake alisema "Hakuwa na SMG alikuwa na bastola, SMG ni silaha ambayo hata mimi Kamanda wa polisi siwezi kutembea nayo"Alifafanua kuwa silaha hiyo ya kivita humilikiwa kwa kibali maalumu na kwamba si rahisi kwa mtu kuwa nayo kienyeji.

  "Hata silaha ambazo alikuwa nazo Waziri Malima ni za kawaida na anazimiliki kihalali" alisema Chialo.

  Akitoa ufafanuzi wa tukio hilo, Machi 9 mwaka huu Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani humo, Hamisi Seleman alisema ingawa uchunguzi unaendelea kufanyika, taarifa za awali zilieleza kuwa mtu asiyejulikana alivunja dirisha la chumba namba 125 alichopanga Naibu Waziri huyo kisha kuingia ndani na kuiba vitu hivyo vyenye thamani ya zaidi ya Sh23.25 milioni.

  "Vitu alivyoibiwa ni pamoja na laptop tatu, aina ya Dell zenye thamani ya Sh5.6 milioni.

  Vinasa sauti viwili vya digitali na headphone zake zote ambavyo thamani yake ni Sh 1 milioni na simu tatu aina ya Nokia C6 ya Sh500,000, Nokia E200 ya Sh250,000 na Blackberry zenye thamani ya Sh5.5 milioni," alisema kamanda huyo na kuongeza:

  "Vitu vingine ni pete mbili za almasi zenye thamani ya Sh2.5 milioni, Dola 4,000 za Marekani ambazo ni sawa na Sh6.5milioni, Sh1.5 milioni, kadi mbili za benki, mabegi matatu ya nguo, baraghashia mbili zenye thamani ya Sh50,000 na nyaraka mbalimbali za Serikali.

  "Kaimu kamanda huyo alisema kuwa polisi waliokwenda kufanya uchunguzi wa awali walibaini kuwa mtu aliyeiba vitu hivyo hakuwa amevaa viatu kutokana na nyayo za miguu yake zilizoonekana nje ya chumba alichokuwa naibu waziri huyo.Kaimu kamanda huyo ambaye pia ni Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Morogoro, alisema kuwa hata hivyo, mwizi aliyeiba vitu hivyo hakuiba bastola na bunduki aina ya SMG alizokuwa nazo Naibu Waziri huyo ambazo zilikuwa sehemu iliyowazi.

  Katika hatua nyingine, polisi mkoani Morogoro, wanawashikilia watu watano wanaotuhumiwa kumwibia Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Malima katika Hoteli ya Nashera wiki iliyopita huku asilimia 90 ya vitu vilivyoibiwa vikipatikana kutoka kwa watuhumiwa hao.

  Kamanda Chialo alisema waliokamatwa kuwa mmoja ni mkazi wa Chamwino kwa Mgulasi na wengine ni wakazi wa Mafiga Manispaa ya Morogoro ambao kwa pamoja wanadaiwa kushiriki katika tukio hilo la wizi.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 6. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #6
  Mar 14, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Mama Mdogo?
   
 7. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #7
  Mar 14, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,787
  Likes Received: 36,795
  Trophy Points: 280
  malaya wana vinywa vilivyojaa asali, Malima alikosa namna ya kumuepuka shangazi uyu.
   
 8. Boonabaana

  Boonabaana JF-Expert Member

  #8
  Mar 14, 2012
  Joined: Oct 22, 2011
  Messages: 227
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Movie bado inaendelea......! The way the cookie crumbles.....
   
 9. B

  Bandio Senior Member

  #9
  Mar 14, 2012
  Joined: Feb 19, 2012
  Messages: 101
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Aibu sana kwa baraza la mawaziri, huu ni uhuni unaojionyesha wazi. Sijui Mhishiwa sana mkuu wa magamba anajisikiaje?!
   
 10. N

  NgomaNgumu Senior Member

  #10
  Mar 14, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Habari hizi ni afadhali ziachwe tu kwani kujaribu kuzitetea ndi kuzidi kuboronga!
   
 11. B

  Bandio Senior Member

  #11
  Mar 14, 2012
  Joined: Feb 19, 2012
  Messages: 101
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni kweli ndugu. Hata hivyo imetusaidia kujua waziri wetu na serikali yetu wasivyokuwa na uwezo wa ku'foresee madhara ya matendo yao.
   
 12. C.T.U

  C.T.U JF-Expert Member

  #12
  Mar 14, 2012
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 4,708
  Likes Received: 1,210
  Trophy Points: 280
  nimependa sana namba tano na ya mwisho ila ya namba tano ni kiboko
   
 13. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #13
  Mar 14, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,787
  Likes Received: 36,795
  Trophy Points: 280
  majina ya hawa watuhumiwa wote ni ......:gossip:
   
 14. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #14
  Mar 14, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,070
  Likes Received: 6,533
  Trophy Points: 280
  'kuwa mtu asiyejulikana alivunja dirisha la chumba namba 125 alichopanga Naibu Waziri huyo kisha kuingia ndani na kuiba vitu hivyo vyenye thamani ya zaidi ya Sh23.25 milioni.

  "Vitu alivyoibiwa ni pamoja na laptop tatu, aina ya Dell zenye thamani ya Sh5.6 milioni.

  Vinasa sauti viwili vya digitali na headphone zake zote ambavyo thamani yake ni Sh 1 milioni na simu tatu aina ya Nokia C6 ya Sh500,000, Nokia E200 ya Sh250,000 na Blackberry zenye thamani ya Sh5.5 milioni," alisema kamanda huyo na kuongeza:

  "Vitu vingine ni pete mbili za almasi zenye thamani ya Sh2.5 milioni, Dola 4,000 za Marekani ambazo ni sawa na Sh6.5milioni, Sh1.5 milioni, kadi mbili za benki, mabegi matatu ya nguo, baraghashia mbili zenye thamani ya Sh50,000 na nyaraka mbalimbali za Serikali'.

  hata malima ni mwizi tu kwanini mali zote hizo.
   
 15. Highlander

  Highlander JF-Expert Member

  #15
  Mar 14, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 3,094
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Thank you for a job well done!
   
 16. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #16
  Mar 14, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  Huyu adolfina anamjua Maokola Majogo?aulize kama hana AK-47?
  Kwani kuwa kamanda ndio kigezo cha umiliki wa silaha? Basi Hussein Mwinyi angekuwa na kifaru
   
 17. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #17
  Mar 14, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,070
  Likes Received: 6,533
  Trophy Points: 280
  alijichimbia ili afanye ngo no yakamkuta,
  si amezee tu.
   
 18. samito

  samito JF-Expert Member

  #18
  Mar 14, 2012
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 621
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kompyuta mpakato-laptop nimeisikia kwa mara ya kwanza. laptop 3 za nin huyu jamaa? na dola za nin? au kapewa alawansi huko alikotoka kufanya ziara. mwambien afunguke
   
 19. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #19
  Mar 14, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Polisi kama public institution hapa Tanzania imepoteza credibility/sifa ya kuaminiwa na wananchi sababu ya uongo wao ambao kwa sasa umekuwa ndo order of the day. Inakuwa ngumu sana kuiamini hii taarifa ya polisi kutokaa na jinsi jeshi hilo linavyojipambanua kwa wananchi siku hadi siku. Polisi ndilo limekuwa kimbilio la wezi/majambazi/mafisadi/wahafidhina/ waongo/wauaji etc. Vinywa vya viongozi wa polisi vimejaa utata mtupu, leo wanasema hivi kesho wanasema vile, leo wanadanganya hivi kesho wanadanganya vile.

  Taarifa ya awali ilitueleza Malima alikuwa na SMG, leo hii tunaelezwa ni kweli alikuwa na silaha mbili (silaha tulizomkuta nazo), ila tunaelezwa kuwa katika silaha alizokutwa nazo hapakuwepo na SMG bila kuelezwa palikuwepo na silaha gani mbadala. Je polisi waliotoa taarifa ya awali hawaijui SMG??kama hawajui hata aina ya bunduki, ni vipi mnataka tuamini kuwa malima kaibiwa vitu vyenye thamani ya 23m???

  Mbaya zaidi Mkuu huyu wa Polisi mkoa anasema si rahisi mtu kumiliki SMG kienyeji, hii maana yake nini hasa????Mbona kila leo majambazi na majangili wanamiliki hizo SMG/AK-47/G3 etc kienyeji???Mbona polisi kibao wanakamatwa wakifanya ujambazi na hizo hizo SMG???RPC anamaana gani kusema si rahisi mtu kumiliki SMG kienyeji????Kwani Malima ni mungu???Malima km waziri wa serikali ya JK anacredibility gani hata tumtoe kwenye umiliki wa SMG tena kwa sababu za kipumbavu zinazotolewa na jeshi la polisi???Kwa maelezo aliyotoa malima mwenyewe juu ya vifaa vilivyoibiwa, ningekuwa polisi makini ningeweka doubt sana.

  Hivi unatembeaje na Laptop tatu?????Hata kama anakazi nyingi sio hivyo jamani, unafanyaje nazo kazi???kwa nini usitembee na external HDD au flash disk na Laptop moja ili kuepusha risks za kuibiwa na kuvunjika???Kwanini ninanyimwa haki ya kuamini kuwa naye Malima ametoka kuziiba sehemu hizo Laptops???Maana amekutwa na SMG kienyeji na anavitu ambavyo si kawaida sana kwa mtu aliyeenda shule kukutwa navyo at per, na maelezo yake hayaeleweki sana. Kwanini asiweke hiyo mihela bank???USD na Matombo ni wapi na wapi??kuna Bureau De Change Matombo hata abebe USDs????anyway!!Kuna mengi ya kujiuliza hapa ila kwa kuwa Polisi hawataki kufanya investigation kwa vile haya yametokea ka Malima, haina shida ila tunashkuru, sisi tunaendelea kuweka kumbu kumbu zetu vizuri.

  Tunaambiwa bunduki anazomiliki Malima zinamilikiwa kihalali, kwanini waandishi wa habari msiende kuchunguza uhalali wa hizo bunduki mbili anazomiliki Malima???Its very simple hebu nendeni kuhakiki uhalali wake, naimani zitakuja sintofahamu nyingi tu mkifanya hivyo, anyway Jeshi la polisi haliaminiki. Naomba mungu rais ajaye alifutilie mbali tuanze upya. Hatuwez kuendelea kuna wa chombo cha kipumbavu kama hiki, kutwa uongo na taarifa zakizushi na za kuficha waalifu na kusafisha wezi na mafusadi. We are sick n tired kwa kweli.

  Halafu jinsi RPC alivyoweka hii story na mwisho wa siku mwanamke (mama mdogo) alivyowekwa wekwa kwenye hii story, yeyote muelewa atagundua kuwa hili sakata linahusisha mwanamke na Malima alikuwa na Mwanamke ila kwakuwa ni Malima, Polisi wameamua kumsafisha na kashfa hiyo ya uzinzi. Sio mbaya mana hiyo ndo sifa ya Jeshi la Polisi, ila the way mlivyoiweka na mwisho wa siku mwanamke alivyokuwa implicated kwenye ishu, wachambuzi wa mambo tumewaelewa na wala hatuna swali.Tunawashkuru kwa taarifa yenu. Ila mjue watanzania sio wajinga kama mnavyowafkiria.
   
 20. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #20
  Mar 14, 2012
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,543
  Likes Received: 2,253
  Trophy Points: 280
  Dah nimefurahi sana hasa hapo kwenye red
   
Loading...