Aliyemuibia Malima ana umbo la kitutsi; Juu mwembamba chini mnene

Ama! Kwa hiyo kutokana na taarifa ya awali kutoka kwa kamanda ni kuwa aliyemwibia Mh. sio mwanamke. Kwa hiyo ni mwanaume mwenye umbo la namba nane??

Halafu alikuwa peku, eti nyayo zimeonekana nje ya chumba cha mheshimiwa! - si ilimbidi asivae skuna zake in case inapiga kelele?
 
Tuichambue hii habari na tukio lenyewe kama ifuatavyo:

1 - Inaonekana mwizi alikuwa ndani ya chumba cha huyu fidhuli na si nje.

2 - Kutokana na maelezo ni kwamba nyayo zilionekana ambazo inaelekea ni za mtu mmoja; lakini je, ina maana nje ya chumba cha bei yote hiyo mwenye hoteli ameshindwa kusakafia na kuacha mchanga na vumbi mpaka nyayo zionekane? Kama kuna sakafu, je, inawezekana miguu ya huyo mwizi ilikuwa imelowa mpaka aache alama za nyayo?

3 - Idadi ya vitu vilivyoibiwa ni kubwa kulinganisha na uwezo wa mtu mmoja kuvibeba kwa mara moja; je, huyo mwizi alirudia hivyo vitu, na kama alirudia ni wapi alikoegesha gari au wenzie walijificha umbali gani kumuwezesha kurudia vitu kama upo uwezekano kuwa alirudia?

4 - Miongoni mwa vilivyoibiwa ni mabegi ya nguo; je, mwanamke mwizi katika hali ya kawaida atahitaji kubeba mabegi ya nguo za kiume ambazo si mpya?

5 - Huyo mwanamke kwenye Defender inasemekana amekutwa na simu tatu na laptop, ingawa habari haisemi ni laptop zote au moja. Je, katika hali ya kawaida, inawezekana kweli hao wanaume wote waliokamatwa waondoke na vitu vingine kama hela, kadi za benki, pete na nguo halafu wamuachie mwizi mwenzao wa kike simu za bei mbaya na laptop?

6 - Je, nyayo zilizoonekana zimepimwa na kufanana na za yeyote kati ya hao waliokamatwa?

7 - Ulinzi katika hoteli hiyo ukoje mpaka vitu vyote hivyo viibiwe, dirisha livunjwe, mtu akimbie na kuacha nyayo - yote haya bila hata walinzi kusikia chochote?

8 - Upo pia uwezekano kwamba aliyekuwepo mle chumbani na Malima ni mwanaume ndiyo maana pengine mabegi yake ya nguo yaliibiwa. Kusema kuwa Malima ana mke hakumaanishi yale mambo ya nanihii hayawezekani, maana wapo waliooa ili kujificha wakati kumbe huwa wanashughulikiwa na wanaume wenzao.

Haya ni ya msingi kuzingatia.
kwa maswali haya yenye lojiki, ningependekeza ukaombe kazi kwa manumba! (Kama huna kazi hhiyo kwake kwa sasa). Unonekana kuwazidi upeo wa kufikiri jamaa wa Intelijinsia!
 
Na Mwandishi Wetu, Morogoro | Global Publishers

WIZI kwenye chumba cha Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Kighoma Malima (pichani) mwishoni mwa wiki iliyopita katika Hoteli ya Nashera mkoani Morogoro, umedaiwa kufanywa na mwanamke anayejiuza, maarufu kama changudoa.

Vyanzo vyetu mbalimbali mjini Morogoro vimedai kuwa mwanamke huyo siku hiyo ya tukio alionekana maeneo ya hoteli hiyo ambapo inadaiwa aliweza kuagiza soda na kunywa kisha kuondoka hotelini hapo na baada ya muda mfupi alirejea.

Habari zinasema, mwanamke huyo haikujulikana aliondokaje katika hoteli hiyo, hivyo watu kumlenga yeye kuwa ndiye mwizi baada ya habari za naibu waziri kuibiwa fedha na mali mbalimbali zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 23 kuzagaa.

Mpasha habari wetu mmoja amedai kuwa mwanamke huyo ambaye amekuwa akihusishwa na wizi pamoja na utapeli mbalimbali mkoani hapa, amekuwa akionekana katika baadhi ya hoteli kubwa.

“Kuna jamaa yangu amewahi kuibiwa katika hoteli moja na mwanamke huyo tunayedhani kuwa kamuibia Waziri Malima. Inasemekana ana ‘funguo malaya’ na hata dawa ya usingizi.

“Siku aliyoibiwa jamaa yangu mwanamke huyo aliingia katika chumba chake akajifanya kuomba simu, baadaye jamaa yangu akajikuta amelala fofofo, akakombwa kila kitu. “Nadhani alitumia dawa ya usingizi, sasa sijui mazingira ya chumba na hoteli aliyolala naibu waziri yalikuwaje,” kilisema chanzo hicho.

Wajihi wa mwanamke huyo ambaye inadaiwa ana kundi la uhalifu ambalo hudiriki kuvunja sehemu wanayodhani ina mali au fedha, ni mweupe, mrefu, ana umbo mithili ya wanawake wa Kitutsi, juu mwembamba, chini mnene na inasemekana hupendelea kutembelea pia jijini Dar es Salaam na Mwanza.

Mwandishi wetu alizungumza na mlinzi mmoja wa Hoteli ya Nashera na kumuuliza kama alimuona mwanamke yeyote siku hiyo ya tukio hotelini hapo ‘akimzengea’ waziri lakini akakataa kuzungumzia suala hilo.

Aidha, Naibu Waziri Malima alipozungumza na gazeti hili alisema hamjui mtu aliyemuibia na hakuwahi ‘kuzengewa’ na mwanamke yeyote siku hiyo.

ALIYEIBA ALIKUWA PEKUPEKU
Naye Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Morogoro (RCO), Hamisi Selemani ambaye siku ya tukio alikuwa akikaimu nafasi ya kamanda wa mkoa, alisema uchunguzi wao wa awali ulibaini kuwa aliyeiba hakuwa amevaa viatu, yaani alikuwa pekupeku.

“Nyayo za mtu huyo zilionekana nje ya chumba namba 125 alichokuwa amelala naibu waziri,” alisema Kamanda Selemani.

ALICHOSEMA RPC
Alipoulizwa juzi na gazeti hili juu ya changudoa huyo anayedaiwa kufanya tukio hilo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, (RPC) Adolfina Chialo alisema hajajua kama changudoa huyo anahusika lakini akakiri kuwa tayari watu watano wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo.

“Kuna vitu vya Naibu Waziri Malima vimepatikana isipokuwa fedha lakini tunaendelea na uchunguzi wa tukio hilo,” alisema.

Aliwataja waliokamatwa kuwa ni Maneno Juma (25), Juma Athumani (23) ambao ni wakazi wa Chamwino, Kwa Mgulasi, Ramadhani Athumani (24) na Abdallah Hassan (25) wakazi wa Mafiga.

Kamanda alimtaja mwanamke Halima Ramadhani (37), mkazi wa Kichangani Morogoro ambaye alisema alikutwa na simu tatu na Kompyuta mpakato (Lap Top), mali za Naibu Waziri Malima.

MALI ALIZOIBIWA
“Tumefanikiwa kukamata mali za waziri kwa asilimia 90 nikimaanisha kwamba vitu vyote vimepatikana isipokuwa fedha,” alisema Kamanda Chialo bila kufafanua zaidi.

Malima alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kubembelezwa kwa saa tano, alitaja mali alizoibiwa na thamani yake katika mabano kuwa ni Kompyuta mpakato tatu aina ya Dell (Sh. Milioni 5.6), Digital Recoder mbili na head phone zake (Sh. Milioni 1), simu tatu aina ya Nokia S6 ( Sh. 500,000), Nokia E200 (Sh. 250,000) na Blackberry ambayo hakutaja thamani yake.

Vingine ni pete mbili za madini ya fedha, fedha taslimu Dola za Kimarekani 4,000 (Zaidi ya shilingi milioni 6.3), shilingi milioni 1.5, kadi mbili za benki, mabegi matatu ya nguo na nyaraka mbalimbali za serikali, zote zikiwa na thamani ya jumla ya shilingi milioni 23.25.

CHANZO: ALIYEMUIBIA WAZIRI MALIMA NI CHANGUDOA - Global Publishers

Nyaraka zilikuwa na thamani gani?
 
stock-vector-different-women-figures-22895122.jpg
yupi kati ya hawa
 
Kudadeki, "MWENYE UMBO NAMBA NANE ALIMCHANGANYA" waziri...
Ushauri wa bure kwa Polisi wawaachie hao walugaluga waliowakamata kwani hawana hatia na wamtafute muhusika halisi ambaye ni changudoa

Huyu naibu waziri anakana kuhusu huyo mwanamke kwa kuinusuru ndoa yake kwani najua dhahiri kutakuwa na something behind
 
Kwa vile dunia siku zote haina siri tuwe na subira tu na ukweli utajidhihirisha soon na wakuumbuka ataumbuka
 
Sometime Mtu unamwambia kweli yake hata kama Inauma, Adam Umezidi sifa sana kwa Mzee, wewe ni naibu lakini Cheki unavyojitutumua, as if Waziri Flan, Unawaza Msukuma aking'olewa wewe utabaki, nakwambia wote mwaweza kula ban, kwani mzee wa mchezo wewe si unajua ana stashahada ya undumilakuwili, huamini ..ok ona mechi after two week.. kwanini kuandikia saliver..
Look here boy, wenzio wakienda hata shambani lazima watengenezewe vyakula laini na wenyeji wao, tena wanatanguliza facilitation charges kabisa.. sasa wewe mwenzetu sisi unasubiri watu wameshakoroma ndio unachupa kutafuta kitu laini, makombo ya wenzio eti kisa uendelee kumantain sifa kwamba wewe ni kama malaika flan-hivi na huhusudishi malavidavi kutoka kwa viumbe hawa.. unafiki wa ajabu mie sijawahi ona mtu wa Pwani mshamba hivi aisee.. sasa skia, yule mlinzi uliyemkamatisha Kijibuku na kuzama na hicho kiumbedawa, na wakati anatoka pia na yeye aliwadakisha kitu, na wanamjua fika, na tayari ameshatoa ushahidi wao polisi, aisee omba wamantain uongo waliofundishwa wakauseme mahakamani, ila wakijivua gamba, wakasema true, off course wataozea jela ila Adam wa kwetu ndo na wewe utakuwa Kweisheeeeeer.. Amigo,
 
Kauli ya Malima kuwa Bastola na Bunduki kubwa walivyoviacha ni mtaji tosha wa maisha ina utata, unapoona waziri anakuja na kauli ya aina hii inakupa picha kuwa hawa watu wana mambo yao zaidi ya uongozi. Na inawezekana yeye mwenyewe alikuwa kwenye dili fulani ndio maana akabeba hiyo silaha kubwa.
 
Hivi kuna Blackberry inauzwa milioni 5.5? Na kama ipo japo sijui, ni ulimbukeni au laa? ina nini cha ziada kilichomfanya Malima kuwa nayo. Kumbe kwa hali hii kulilia posho bungeni hakutakwisha kamwe
blackberry porsche
inauzwa usd 2500

Hivi kwanini hii ishu isipelekwe holiwud tupate vidola kidogo??
 
Sometime Mtu unamwambia kweli yake hata kama Inauma, Adam Umezidi sifa sana kwa Mzee, wewe ni naibu lakini Cheki unavyojitutumua, as if Waziri Flan, Unawaza Msukuma aking'olewa wewe utabaki, nakwambia wote mwaweza kula ban, kwani mzee wa mchezo wewe si unajua ana stashahada ya undumilakuwili, huamini ..ok ona mechi after two week.. kwanini kuandikia saliver..
Look here boy, wenzio wakienda hata shambani lazima watengenezewe vyakula laini na wenyeji wao, tena wanatanguliza facilitation charges kabisa.. sasa wewe mwenzetu sisi unasubiri watu wameshakoroma ndio unachupa kutafuta kitu laini, makombo ya wenzio eti kisa uendelee kumantain sifa kwamba wewe ni kama malaika flan-hivi na huhusudishi malavidavi kutoka kwa viumbe hawa.. unafiki wa ajabu mie sijawahi ona mtu wa Pwani mshamba hivi aisee.. sasa skia, yule mlinzi uliyemkamatisha Kijibuku na kuzama na hicho kiumbedawa, na wakati anatoka pia na yeye aliwadakisha kitu, na wanamjua fika, na tayari ameshatoa ushahidi wao polisi, aisee omba wamantain uongo waliofundishwa wakauseme mahakamani, ila wakijivua gamba, wakasema true, off course wataozea jela ila Adam wa kwetu ndo na wewe utakuwa Kweisheeeeeer.. Amigo,
.......wewe!....wewe!......wewe!....
 
ni muhimu viongozi wanunuliwa mobile van kama zile za ATM za mabank ili waifadhi simu na mabunduki yao,maana kama safari ya moro wanamizigo hivyo akienda geita si italazimu kwenda na contener kabisa.bora wawe na hayo magari
 
Watu kuibiwa na machangu si jambo geni,lakini wengi wanakuwa wamelala nao.Most likely jamaa alijishindia,na binti akaona kuna noti,kwa kushirikiana na walinzi akachukua akasepa.Lakini hata hivyo kwa nini mtu utembee na hela zote hizo?Kwa jinsi hawa jamaa wanavyotuibia na kutunyanyasa,mimi nina guts za kusema binti karudisha mali yake iliyoibiwa na nampa hongera sana.
Na Mwandishi Wetu, Morogoro | Global Publishers

WIZI kwenye chumba cha Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Kighoma Malima (pichani) mwishoni mwa wiki iliyopita katika Hoteli ya Nashera mkoani Morogoro, umedaiwa kufanywa na mwanamke anayejiuza, maarufu kama changudoa.

Vyanzo vyetu mbalimbali mjini Morogoro vimedai kuwa mwanamke huyo siku hiyo ya tukio alionekana maeneo ya hoteli hiyo ambapo inadaiwa aliweza kuagiza soda na kunywa kisha kuondoka hotelini hapo na baada ya muda mfupi alirejea.

Habari zinasema, mwanamke huyo haikujulikana aliondokaje katika hoteli hiyo, hivyo watu kumlenga yeye kuwa ndiye mwizi baada ya habari za naibu waziri kuibiwa fedha na mali mbalimbali zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 23 kuzagaa.

Mpasha habari wetu mmoja amedai kuwa mwanamke huyo ambaye amekuwa akihusishwa na wizi pamoja na utapeli mbalimbali mkoani hapa, amekuwa akionekana katika baadhi ya hoteli kubwa.

“Kuna jamaa yangu amewahi kuibiwa katika hoteli moja na mwanamke huyo tunayedhani kuwa kamuibia Waziri Malima. Inasemekana ana ‘funguo malaya’ na hata dawa ya usingizi.

“Siku aliyoibiwa jamaa yangu mwanamke huyo aliingia katika chumba chake akajifanya kuomba simu, baadaye jamaa yangu akajikuta amelala fofofo, akakombwa kila kitu. “Nadhani alitumia dawa ya usingizi, sasa sijui mazingira ya chumba na hoteli aliyolala naibu waziri yalikuwaje,” kilisema chanzo hicho.

Wajihi wa mwanamke huyo ambaye inadaiwa ana kundi la uhalifu ambalo hudiriki kuvunja sehemu wanayodhani ina mali au fedha, ni mweupe, mrefu, ana umbo mithili ya wanawake wa Kitutsi, juu mwembamba, chini mnene na inasemekana hupendelea kutembelea pia jijini Dar es Salaam na Mwanza.

Mwandishi wetu alizungumza na mlinzi mmoja wa Hoteli ya Nashera na kumuuliza kama alimuona mwanamke yeyote siku hiyo ya tukio hotelini hapo ‘akimzengea’ waziri lakini akakataa kuzungumzia suala hilo.

Aidha, Naibu Waziri Malima alipozungumza na gazeti hili alisema hamjui mtu aliyemuibia na hakuwahi ‘kuzengewa’ na mwanamke yeyote siku hiyo.

ALIYEIBA ALIKUWA PEKUPEKU
Naye Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Morogoro (RCO), Hamisi Selemani ambaye siku ya tukio alikuwa akikaimu nafasi ya kamanda wa mkoa, alisema uchunguzi wao wa awali ulibaini kuwa aliyeiba hakuwa amevaa viatu, yaani alikuwa pekupeku.

“Nyayo za mtu huyo zilionekana nje ya chumba namba 125 alichokuwa amelala naibu waziri,” alisema Kamanda Selemani.

ALICHOSEMA RPC
Alipoulizwa juzi na gazeti hili juu ya changudoa huyo anayedaiwa kufanya tukio hilo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, (RPC) Adolfina Chialo alisema hajajua kama changudoa huyo anahusika lakini akakiri kuwa tayari watu watano wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo.

“Kuna vitu vya Naibu Waziri Malima vimepatikana isipokuwa fedha lakini tunaendelea na uchunguzi wa tukio hilo,” alisema.

Aliwataja waliokamatwa kuwa ni Maneno Juma (25), Juma Athumani (23) ambao ni wakazi wa Chamwino, Kwa Mgulasi, Ramadhani Athumani (24) na Abdallah Hassan (25) wakazi wa Mafiga.

Kamanda alimtaja mwanamke Halima Ramadhani (37), mkazi wa Kichangani Morogoro ambaye alisema alikutwa na simu tatu na Kompyuta mpakato (Lap Top), mali za Naibu Waziri Malima.

MALI ALIZOIBIWA
“Tumefanikiwa kukamata mali za waziri kwa asilimia 90 nikimaanisha kwamba vitu vyote vimepatikana isipokuwa fedha,” alisema Kamanda Chialo bila kufafanua zaidi.

Malima alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kubembelezwa kwa saa tano, alitaja mali alizoibiwa na thamani yake katika mabano kuwa ni Kompyuta mpakato tatu aina ya Dell (Sh. Milioni 5.6), Digital Recoder mbili na head phone zake (Sh. Milioni 1), simu tatu aina ya Nokia S6 ( Sh. 500,000), Nokia E200 (Sh. 250,000) na Blackberry ambayo hakutaja thamani yake.

Vingine ni pete mbili za madini ya fedha, fedha taslimu Dola za Kimarekani 4,000 (Zaidi ya shilingi milioni 6.3), shilingi milioni 1.5, kadi mbili za benki, mabegi matatu ya nguo na nyaraka mbalimbali za serikali, zote zikiwa na thamani ya jumla ya shilingi milioni 23.25.

CHANZO: ALIYEMUIBIA WAZIRI MALIMA NI CHANGUDOA - Global Publishers
 
..Nimetafakari na bado hainiingii akilini. Hoteli yenye gharama ya chumba shilingi 400,000.00 haina Kamera ya ulinzi? mmhh haya Pole waziri wangu. Siku ingine ukalale Ikulu ndogo. Au siku hizi hazipo??
 
Ama! Kwa hiyo kutokana na taarifa ya awali kutoka kwa kamanda ni kuwa aliyemwibia Mh. sio mwanamke. Kwa hiyo ni mwanaume mwenye umbo la namba nane??

Halafu alikuwa peku, eti nyayo zimeonekana nje ya chumba cha mheshimiwa! - si ilimbidi asivae skuna zake in case inapiga kelele?

Footprints zilizokutwa ndani ni za malima mwenyewe! kwanini tusisema huyu malima ana dili nyingine zaidi ya uongozi?
Kutembea na Bastola na SMG tusiseme ni jambazi ni haki? I wish he is!
 
WIZI kwenye chumba cha Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Kighoma Malima mwishoni mwa wiki iliyopita katika Hoteli ya Nashera mkoani Morogoro, umedaiwa kufanywa na mwanamke anayejiuza, maarufu kama changudoa.
Vyanzo vyetu mbalimbali mjini Morogoro vimedai kuwa mwanamke huyo siku hiyo ya tukio alionekana maeneo ya hoteli hiyo ambapo inadaiwa aliweza kuagiza soda na kunywa kisha kuondoka hotelini hapo na baada ya muda mfupi alirejea.
Habari zinasema, mwanamke huyo haikujulikana aliondokaje katika hoteli hiyo, hivyo watu kumlenga yeye kuwa ndiye mwizi baada ya habari za naibu waziri kuibiwa fedha na mali mbalimbali zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 23 kuzagaa.
Mpasha habari wetu mmoja amedai kuwa mwanamke huyo ambaye amekuwa akihusishwa na wizi pamoja na utapeli mbalimbali mkoani hapa, amekuwa akionekana katika baadhi ya hoteli kubwa.
“Kuna jamaa yangu amewahi kuibiwa katika hoteli moja na mwanamke huyo tunayedhani kuwa kamuibia Waziri Malima.Inasemekana ana ‘funguo malaya’ na hata dawa ya usingizi.
“Siku aliyoibiwa jamaa yangu mwanamke huyo aliingia katika chumba chake akajifanya kuomba simu, baadaye jamaa yangu akajikuta amelala fofofo, akakombwa kila kitu. “Nadhani alitumia dawa ya usingizi, sasa sijui mazingira ya chumba na hoteli aliyolala naibu waziri yalikuwaje,” kilisema chanzo hicho.
Wajihi wa mwanamke huyo ambaye inadaiwa ana kundi la uhalifu ambalo hudiriki kuvunja sehemu wanayodhani ina mali au fedha, ni mweupe, mrefu, ana umbo mithili ya wanawake wa Kitutsi, juu mwembamba, chini mnene na inasemekana hupendelea kutembelea pia jijini Dar es Salaam na Mwanza.
Mwandishi wetu alizungumza na mlinzi mmoja wa Hoteli ya Nashera na kumuuliza kama alimuona mwanamke yeyote siku hiyo ya tukio hotelini hapo ‘akimzengea’ waziri lakini akakataa kuzungumzia suala hilo.
Aidha, Naibu Waziri Malima alipozungumza na gazeti hili alisema hamjui mtu aliyemuibia na hakuwahi ‘kuzengewa’ na mwanamke yeyote siku hiyo.
[FONT='Lucida Grande', 'Lucida Sans Unicode', sans-serif]
[/FONT]ALIYEIBA ALIKUWA PEKUPEKU
Naye Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Morogoro (RCO), Hamisi Selemani ambaye siku ya tukio alikuwa akikaimu nafasi ya kamanda wa mkoa, alisema uchunguzi wao wa awali ulibaini kuwa aliyeiba hakuwa amevaa viatu, yaani alikuwa pekupeku.
“Nyayo za mtu huyo zilionekana nje ya chumba namba 125 alichokuwa amelala naibu waziri,” alisema Kamanda Selemani.

ALICHOSEMA RPC
Alipoulizwa juzi na gazeti hili juu ya changudoa huyo anayedaiwa kufanya tukio hilo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, (RPC) Adolfina Chialo alisema hajajua kama changudoa huyo anahusika lakini akakiri kuwa tayari watu watano wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo.
“Kuna vitu vya Naibu Waziri Malima vimepatikana isipokuwa fedha lakini tunaendelea na uchunguzi wa tukio hilo,” alisema.
Aliwataja waliokamatwa kuwa ni Maneno Juma (25), Juma Athumani (23) ambao ni wakazi wa Chamwino, Kwa Mgulasi, Ramadhani Athumani (24) na Abdallah Hassan (25) wakazi wa Mafiga.
Kamanda alimtaja mwanamke Halima Ramadhani (37), mkazi wa Kichangani Morogoro ambaye alisema alikutwa na simu tatu na Kompyuta mpakato (Lap Top), mali za Naibu Waziri Malima.

MALI ALIZOIBIWA
“Tumefanikiwa kukamata mali za waziri kwa asilimia 90 nikimaanisha kwamba vitu vyote vimepatikana isipokuwa fedha,” alisema Kamanda Chialo bila kufafanua zaidi.
Malima alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kubembelezwa kwa saa tano, alitaja mali alizoibiwa na thamani yake katika mabano kuwa ni Kompyuta mpakato tatu aina ya Dell (Sh. Milioni 5.6), Digital Recoder mbili na head phone zake (Sh. Milioni 1), simu tatu aina ya Nokia S6 ( Sh. 500,000), Nokia E200 (Sh. 250,000) na Blackberry ambayo hakutaja thamani yake.
Vingine ni pete mbili za madini ya fedha, fedha taslimu Dola za Kimarekani 4,000 (Zaidi ya shilingi milioni 6.3), shilingi milioni 1.5, kadi mbili za benki, mabegi matatu ya nguo na nyaraka mbalimbali za serikali, zote zikiwa na thamani ya jumla ya shilingi milioni 23.25.​
 
dU, !
Dada Bandidu huyu!...jamaa hakumlipa mapatano nini?
 
Kwa nidhamu hii ya machangu eti hata Malima naye ni Waziri katika nchi hii; my foot!!!

WIZI kwenye chumba cha Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Kighoma Malima mwishoni mwa wiki iliyopita katika Hoteli ya Nashera mkoani Morogoro, umedaiwa kufanywa na mwanamke anayejiuza, maarufu kama changudoa.

Vyanzo vyetu mbalimbali mjini Morogoro vimedai kuwa mwanamke huyo siku hiyo ya tukio alionekana maeneo ya hoteli hiyo ambapo inadaiwa aliweza kuagiza soda na kunywa kisha kuondoka hotelini hapo na baada ya muda mfupi alirejea.

Habari zinasema, mwanamke huyo haikujulikana aliondokaje katika hoteli hiyo, hivyo watu kumlenga yeye kuwa ndiye mwizi baada ya habari za naibu waziri kuibiwa fedha na mali mbalimbali zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 23 kuzagaa.

Mpasha habari wetu mmoja amedai kuwa mwanamke huyo ambaye amekuwa akihusishwa na wizi pamoja na utapeli mbalimbali mkoani hapa, amekuwa akionekana katika baadhi ya hoteli kubwa.

"Kuna jamaa yangu amewahi kuibiwa katika hoteli moja na mwanamke huyo tunayedhani kuwa kamuibia Waziri Malima.Inasemekana ana ‘funguo malaya' na hata dawa ya usingizi.

"Siku aliyoibiwa jamaa yangu mwanamke huyo aliingia katika chumba chake akajifanya kuomba simu, baadaye jamaa yangu akajikuta amelala fofofo, akakombwa kila kitu. "Nadhani alitumia dawa ya usingizi, sasa sijui mazingira ya chumba na hoteli aliyolala naibu waziri yalikuwaje," kilisema chanzo hicho.

Wajihi wa mwanamke huyo ambaye inadaiwa ana kundi la uhalifu ambalo hudiriki kuvunja sehemu wanayodhani ina mali au fedha, ni mweupe, mrefu, ana umbo mithili ya wanawake wa Kitutsi, juu mwembamba, chini mnene na inasemekana hupendelea kutembelea pia jijini Dar es Salaam na Mwanza.

Mwandishi wetu alizungumza na mlinzi mmoja wa Hoteli ya Nashera na kumuuliza kama alimuona mwanamke yeyote siku hiyo ya tukio hotelini hapo ‘akimzengea' waziri lakini akakataa kuzungumzia suala hilo.

Aidha, Naibu Waziri Malima alipozungumza na gazeti hili alisema hamjui mtu aliyemuibia na hakuwahi ‘kuzengewa' na mwanamke yeyote siku hiyo.

[FONT='Lucida Grande', 'Lucida Sans Unicode', sans-serif]

ALIYEIBA ALIKUWA PEKUPEKU

Naye Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Morogoro (RCO), Hamisi Selemani ambaye siku ya tukio alikuwa akikaimu nafasi ya kamanda wa mkoa, alisema uchunguzi wao wa awali ulibaini kuwa aliyeiba hakuwa amevaa viatu, yaani alikuwa pekupeku.

"Nyayo za mtu huyo zilionekana nje ya chumba namba 125 alichokuwa amelala naibu waziri," alisema Kamanda Selemani.

ALICHOSEMA RPC

Alipoulizwa juzi na gazeti hili juu ya changudoa huyo anayedaiwa kufanya tukio hilo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, (RPC) Adolfina Chialo alisema hajajua kama changudoa huyo anahusika lakini akakiri kuwa tayari watu watano wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo.

"Kuna vitu vya Naibu Waziri Malima vimepatikana isipokuwa fedha lakini tunaendelea na uchunguzi wa tukio hilo," alisema.

Aliwataja waliokamatwa kuwa ni Maneno Juma (25), Juma Athumani (23) ambao ni wakazi wa Chamwino, Kwa Mgulasi, Ramadhani Athumani (24) na Abdallah Hassan (25) wakazi wa Mafiga.

Kamanda alimtaja mwanamke Halima Ramadhani (37), mkazi wa Kichangani Morogoro ambaye alisema alikutwa na simu tatu na Kompyuta mpakato (Lap Top), mali za Naibu Waziri Malima.

MALI ALIZOIBIWA

"Tumefanikiwa kukamata mali za waziri kwa asilimia 90 nikimaanisha kwamba vitu vyote vimepatikana isipokuwa fedha," alisema Kamanda Chialo bila kufafanua zaidi.

Malima alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kubembelezwa kwa saa tano, alitaja mali alizoibiwa na thamani yake katika mabano kuwa ni Kompyuta mpakato tatu aina ya Dell (Sh. Milioni 5.6), Digital Recoder mbili na head phone zake (Sh. Milioni 1), simu tatu aina ya Nokia S6 ( Sh. 500,000), Nokia E200 (Sh. 250,000) na Blackberry ambayo hakutaja thamani yake.

Vingine ni pete mbili za madini ya fedha, fedha taslimu Dola za Kimarekani 4,000 (Zaidi ya shilingi milioni 6.3), shilingi milioni 1.5, kadi mbili za benki, mabegi matatu ya nguo na nyaraka mbalimbali za serikali, zote zikiwa na thamani ya jumla ya shilingi milioni 23.25.
[/FONT]

​
 
Back
Top Bottom