Aliyemtapeli Imamu simu, kusomewa Dua Maalum

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,156
13,249
Tapeli maarufu ambaye ameutumia mwezi Mtukufu wa Ramadhani kutapeli kwenye misikiti mbalimbali kwa minajili ya kufuturisha sasa anaandaliwa dua maalum kwa mujibu wa Imam wa Msikiti mmoja huko Temeke DSM aliyekua akihojiwa na Clouds nami kumsikia LIVE

Tapeli huyo alifika kwa imamu akiwa na toyo na kumwambia amekuja hapo kwa nia ya kufuturisha na akamwomba wanawake wawili wa kupika, alipoondoka nao kama anakwenda sokoni akawapiga simu kisha kurudi kwa imamu naye akampiga simu kwa kumwambia anataka aongee na mtu wa kumtumia fedha na kutokomea nayo kumbe alimfuata wa toyo na kumtapeli pia simu yake.

Yasemekana ameshafanya hivi huko Mbagala na kwingineko
 
Sio mchezoo.mambo ya dua tena ina-apply vipi na utapeli?asamehe 7×70.
 
Tapeli maarufu ambaye ameutumia mwezi Mtukufu wa Ramadhani kutapeli kwenye misikiti mbalimbali kwa minajili ya kufuturisha sasa anaandaliwa dua maalum kwa mujibu wa Imam wa Msikiti mmoja huko Temeke DSM aliyekua akihojiwa na Clouds nami kumsikia LIVE

Tapeli huyo alifika kwa imamu akiwa na toyo na kumwambia amekuja hapo kwa nia ya kufuturisha na akamwomba wanawake wawili wa kupika, alipoondoka nao kama anakwenda sokoni akawapiga simu kisha kurudi kwa imamu naye akampiga simu kwa kumwambia anataka aongee na mtu wa kumtumia fedha na kutokomea nayo kumbe alimfuata wa toyo na kumtapeli pia simu yake.

Yasemekana ameshafanya hivi huko Mbagala na kwingineko
Mbona Sioni Utapeli Hapo??
 
Wezi wengi tu huku mtaani kwetu huwa wanaambiwa watasomewa dua lakini mpaka leo wapo fresh. Hii dua ni Uchawi wa kufikirika tu na kumtisha mtu.
 
Comment yako imejaa mihemko na chuki zaidi kwa dini fulani,kwa hiyo wale wanaoua vibaka mitaani au wazinzi walioshikwa na wake za watu wao hua wanamrahishia kazi nani?
Hao wanaoua vibaka mtaani sio viongozi wa dini, kwa hiyo lolote wanalofanya halihusiani na mafundisho yoyote. Kumbuka ile kauli niliyoizungumzia imetoka kwa Imamu wa msikiti ambaye anaongoza waumini kadhaa katika swala zao, hivyo atakalolifanya tena msikitini halina shaka yoyote kuwa ni kwa mujibu wa mafundisho ya imani yake
 
Back
Top Bottom