Najaribu kuwaza Kama tokea 2015 Rais Magufuli angeruhusu shughuli za kisiasa kuendelea Kama ilivyokuwa kipindi Cha nyuma, na hivyo Wapinzani kupata fursa ya kufanya mikutano ya kisiasa Mara kwa Mara ili kuwaambia wananchi juu ya madudu ambayo yamefanyika ndani ya miaka 5, Basi uchaguzi wa mwaka huu Magufuli angeshindwa vibaya sana.
Alicheza karata zake vizuri, ingawa pamoja na Kwamba wapinzani wote walizibwa midomo, wakafungwa kamba wasifanye siasa, na hivyo yeye pekee kuzunguka nchi nzima kuwaeleza wananchi Yale anayoyafanya, lakini bado inaonyesha watu wanataka mabadiliko.
Upinzani unaonekana kupokelewa kuliko kawaida. Pamoja na kwamba watu wamepigwa swaga za madaraja, barabara, Ndege n.k lakini wanataka maisha Bora, ajira na huduma nzuri za afya, vitu ambavyo wamevikosa katika awamu hii.