Aliyempigisha ‘deki’ Mwalimu aigomea CWT

Aliyempigisha ‘deki’ Mwalimu aigomea CWT

JAMANI WAALIMU WENGINE NI WACHAFU WANASHINDWA KUSIMAMIA WANAFUNZI KUFANYA USAFI..MIMI NAMPA PONGEZI HUYO MKURUGENZI
 
Pia hajawatendea wanafunzi haki,maana watamdharau na kuwadharau waalimu,ss watapataje elim bora,duuuh
 
Itanishangaza kama maoni yangu niliyoyatoa ya kutengua uteuzi Wa Mkurugenzi Wa Halmashauri ya Misungwi Bwana Eliud Yatapuuzwa.CWT hongereni kwa hatua ya awali! Haiwezekani kuongozwa na kiongozi kama huyu kana kwamba kazi hiyo hamkuisomea,ni kheri kufukuzwa kazi kuliko kurudishwa utumwani.

Ni matarajio yangu CWT hamtoishia hapo endapo Uteuzi wake haujatenguliwa.

Pia Waziri Wa Elimu na serikali kwa ujumla sijaona Tamko lolote juu ya hili jambo kama ilivyokuwa haraka kutoa tamko kwa Mwl Msigwa.

Mwisho kabisa ni matarajio yangu kusikia kutenguliwa huyu bwana ambaye nafasi hii ameshindwa kuitendea haki na kujiona Mungu Mtu. Ata Magufuli kama Rais naimani asingechukua maamuzi aliochukua huyu Mkurugenzi.
[HASHTAG]#MagufuliTumbuaJipu[/HASHTAG]

B. P. Ishengoma

#Jfinfo#

ELIUD Mwaiteleke, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, aliyeamuru Hamis Sengo, mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Shilala kudeki darasa mbele ya wanafunzi ‘amekitolea nje’ Chama Cha Walimu (CWT) mkoani Mwanza baada ya viongozi wake kutaka kumuona na kumtaka aombe radhi.

Tukio la mkurugenzi huyo kumdhalilisha mwalimu huyo mbele ya wanafunzi wake, lilitokea Oktoba 17, mwaka huu shuleni hapo, baada ya ‘bosi’ huyo wa halmashauri kukuta baadhi ya madarasa yakiwa machafu.

Mkurugenzi Mwaiteleke akiwa ameambatana na maofisa wengine wa serikali ngazi ya wilaya hiyo, alifika shuleni hapo majira ya jioni na kumuita mwalimu (Sengo) ili aeleze kwanini madarasa ni machafu na kumtaka kudeki kitendo kilichotekelezwa na mwalimu huyo bila kupinga.

Sibora Kisheri, mwenyekiti wa CWT mkoani hapa amesema kuwa wamelipokea tukio hilo kwa masikitiko na kwamba wamemtaka mkurugenzi huyo kuomba radhi bila mafanikio.

“Tumefanya mazungumzo na tukaazimia kumtaka mkurugenzi huyo kuomba radhi na kumhamisha mwalimu huyo shuleni hapo kwa gharama zake na asifanye kitendo hicho kwa mwalimu mwingine.

Endapo mkurungezi huyo atashindwa kutekeleza maagizo hayo, tutachukua hatua kali zaidi kwani tumechoka kuonewa na viongozi wa serikali kila kukicha.

Kisheri amesema kuwa viongozi wa CWT walienda kuonana na mkurugenzi huyo lakini hakutaka kuonesha ushirikiano kwao na alidai kwamba leo anasafiri hawawezi kuonana na sisi.

“Mkurugenzi ni msimamizi wa watumishi lakini tunashangaa kuona kiongozi kama huyo anageuka kuwa mnyanyasaji na viongozi wasidhani kama sisi ni wanyonge, tunaweza kuchukua maamzi magumu zaidi ya hayo,” amesema Kisheri.

Alipopigiwa simu yake zaidi ya mara tano, ilikuwa ikiita na kukatwa lakini baadae ilipokelewa na mkurugenzi huyo kumtaka mwandishi kuwa yupo barabarani na hawezi kuzungumzia suala hilo.

Mkurugenzi: Nipo barabarani, sikusikii vizuri ni tukio gani?

Mwandishi: Ni tukio la kumuamuru mwalimu kudeki darasa ulilolifanya Oktoba 17.

Mkurugenzi: Ngoja nikutumie namba za afisa habari wa wilaya (Misungwi) atakueleza suala hilo.

Chanzo: Mwanahalisi Online
 
Watoto wetu ndio maana wanaugua sinusitis kwa sababu ya vumbi. Kama shule haina mkakati wa kufanya usafi mwalimu atapiga deki tu.

Mkurugenzi umekata mzizi wa uzembe kwenye maswala ya hygiene.

Watu wana negative perception bila kuangalia concept ya director, kuna watu wanahitaji njia ngumu ndio wajifunze.
 
Nilipitia bandiko la huyo Mkurugenzi alipokuwa anajibu tuhuma za kumdhalilisha mwalimu. Hakuna jibu lolote la maana katika ile taarifa yake. Hii ni dharau kwa walimu na watu wote wanaohusika na elimu.
Ningemuomba mwalimu aliyedhalilishwa kutafuta utaratibu wa kumshtaki kwenye mamlaka za kinidhamu huyu Mkurugenzi. Natambua watu wa CWT wanaelewa ni taratibu zipi zinastahili kuchukuliwa pindi mfanyakazi anaponyanyaswa kazini. CWT wamuelekeze huyo muathirika na kumsimamia ili apate haki zake. Haipendezi na wala haikubaliki kwa jamii iliyostaarabika kuliacha hili suala liishe kama hivi.
 
Ningekua Mimi ndio niliemteuwa huyo mkulugenzi.ningeshamuondoa kitambo tu.
 
Mwalimu Msigwa tafadhali njoo uone yaliyomkuta mwenzako kisha utwambie ungekuwa wewe ungemfanya nini huyu mkurugenzi!!
 
Hicho kitendo ni cha kutia fedheha na kinakera sana nitakuwa nakosea sana nikimlaumu Mwalimu aliyetii amri hiyo inayofedhehesha na sitokosea sana kwa mtazamo wangu kumuita Mkurugenzi huyo Mlevi wa madaraka.
Haina haja ya kulaani tena vitendo kama hivi ila ni wakati wa Waalimu kujitathmini na kuchukua hatua madhubuti kusimamia taaluma zao.
Naungana na harakati zote za kumwamsha Mwalimu na vuguvugu la kupinga kivitendo ufedheheshwaji wa namna yoyote ile kwa waalimu.
Tumeonewa sana,tumedhalilishwa sana na tumefedheheshwa sana na hii ni kutokana na kufundishwa kuwa wanyonge.
Sababu tunayo nia tunayo na nguvu tunazo za kupinga vikali udhalilishwaji kwa Waalimu.
Waalimu tuamke
 
Mkurugenzi Aliyempigisha ‘deki’ Mwalimu aigomea CWT
ELIUD Mwaiteleke, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, aliyeamuru Hamis Sengo, mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Shilala kudeki darasa mbele ya wanafunzi ‘amekitolea nje’ Chama Cha Walimu (CWT) mkoani Mwanza baada ya viongozi wake kutaka kumuona na kumtaka aombe radhi.
Tukio la mkurugenzi huyo kumdhalilisha mwalimu huyo mbele ya wanafunzi wake, lilitokea Oktoba 17, mwaka huu shuleni hapo, baada ya ‘bosi’ huyo wa halmashauri kukuta baadhi ya madarasa yakiwa machafu. Mkurugenzi Mwaiteleke akiwa ameambatana na maofisa wengine wa serikali ngazi ya wilaya hiyo, alifika shuleni hapo majira ya jioni na kumuita mwalimu (Sengo) ili aeleze kwanini madarasa ni machafu na kumtaka kudeki kitendo kilichotekelezwa na mwalimu huyo bila kupinga.
Sibora Kisheri, mwenyekiti wa CWT mkoani hapa amesema kuwa wamelipokea tukio hilo kwa masikitiko na kwamba wamemtaka mkurugenzi huyo kuomba radhi bila mafanikio. “Tumefanya mazungumzo na tukaazimia kumtaka mkurugenzi huyo kuomba radhi na kumhamisha mwalimu huyo shuleni hapo kwa gharama zake na asifanye kitendo hicho kwa mwalimu mwingine.

Endapo mkurungezi huyo atashindwa kutekeleza maagizo hayo, tutachukua hatua kali zaidi kwani tumechoka kuonewa na viongozi wa serikali kila kukicha. Kisheri amesema kuwa viongozi wa CWT walienda kuonana na mkurugenzi huyo lakini hakutaka kuonesha ushirikiano kwao na alidai kwamba leo anasafiri hawawezi kuonana na sisi. “Mkurugenzi ni msimamizi wa watumishi lakini tunashangaa kuona kiongozi kama huyo anageuka kuwa mnyanyasaji na viongozi wasidhani kama sisi ni wanyonge, tunaweza kuchukua maamzi magumu zaidi ya hayo,” amesema Kisheri. Alipopigiwa simu yake zaidi ya mara tano, ilikuwa ikiita na kukatwa lakini baadae ilipokelewa na mkurugenzi huyo kumtaka mwandishi kuwa yupo barabarani na hawezi kuzungumzia suala hilo. Mkurugenzi: Nipo barabarani, sikusikii vizuri ni tukio gani? Mwandishi: Ni tukio la kumuamuru mwalimu kudeki darasa ulilolifanya Oktoba 17. Mkurugenzi: Ngoja nikutumie namba za afisa habari wa wilaya (Misungwi) atakueleza suala hilo.
 
Yule aliyemdhalilisha askari kama sikosei alishatumbuliwa, ngoja tuone huyo aliyemdhalilisha mwalimu
 
Nakumbuka yule aliyewacharaza walimu bakora huko Bukoba, ingekuwa awamu hii angetunukiwa na cheo cha heshima ya juu maana kwenye zama hizi ni hakuna kuremba.
 
Raisi wetu msikivu... huyu mkurugenzi atawajibishwa kama yule wa Mkinga aliye mdhalilisha polisi.....mbaya zaidu huyu wa misungwi mashahidi ni wengi sana....
 
Back
Top Bottom