Aliyempigisha ‘deki’ Mwalimu aigomea CWT

Aliyempigisha ‘deki’ Mwalimu aigomea CWT

dunia ni mapito sote tutakufa na tutaiacha2
acheni tudharauliane maana Mungu aliyaumba na hayana budi kuwepo lakini sote mwisho wetu ni kaburini.
Kilio cha samaki hakina machozi,,,,,,, machozi Imebaki majini kilioo,,, ooooo....... Wema a a a tenda wema nenda zako usitizame nyuma,,,... Yatakuletea matatizoooo tenda wema uende zakoooooo,,,, kilio,, oooo,,, mwanamama *2,,,
 
ELIUD Mwaiteleke, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, aliyeamuru Hamis Sengo, mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Shilala kudeki darasa mbele ya wanafunzi ‘amekitolea nje’ Chama Cha Walimu (CWT) mkoani Mwanza baada ya viongozi wake kutaka kumuona na kumtaka aombe radhi.

Tukio la mkurugenzi huyo kumdhalilisha mwalimu huyo mbele ya wanafunzi wake, lilitokea Oktoba 17, mwaka huu shuleni hapo, baada ya ‘bosi’ huyo wa halmashauri kukuta baadhi ya madarasa yakiwa machafu.

Mkurugenzi Mwaiteleke akiwa ameambatana na maofisa wengine wa serikali ngazi ya wilaya hiyo, alifika shuleni hapo majira ya jioni na kumuita mwalimu (Sengo) ili aeleze kwanini madarasa ni machafu na kumtaka kudeki kitendo kilichotekelezwa na mwalimu huyo bila kupinga.

Sibora Kisheri, mwenyekiti wa CWT mkoani hapa amesema kuwa wamelipokea tukio hilo kwa masikitiko na kwamba wamemtaka mkurugenzi huyo kuomba radhi bila mafanikio.

“Tumefanya mazungumzo na tukaazimia kumtaka mkurugenzi huyo kuomba radhi na kumhamisha mwalimu huyo shuleni hapo kwa gharama zake na asifanye kitendo hicho kwa mwalimu mwingine.

Endapo mkurungezi huyo atashindwa kutekeleza maagizo hayo, tutachukua hatua kali zaidi kwani tumechoka kuonewa na viongozi wa serikali kila kukicha.

Kisheri amesema kuwa viongozi wa CWT walienda kuonana na mkurugenzi huyo lakini hakutaka kuonesha ushirikiano kwao na alidai kwamba leo anasafiri hawawezi kuonana na sisi.

“Mkurugenzi ni msimamizi wa watumishi lakini tunashangaa kuona kiongozi kama huyo anageuka kuwa mnyanyasaji na viongozi wasidhani kama sisi ni wanyonge, tunaweza kuchukua maamzi magumu zaidi ya hayo,” amesema Kisheri.

Alipopigiwa simu yake zaidi ya mara tano, ilikuwa ikiita na kukatwa lakini baadae ilipokelewa na mkurugenzi huyo kumtaka mwandishi kuwa yupo barabarani na hawezi kuzungumzia suala hilo.

Mkurugenzi: Nipo barabarani, sikusikii vizuri ni tukio gani?

Mwandishi: Ni tukio la kumuamuru mwalimu kudeki darasa ulilolifanya Oktoba 17.

Mkurugenzi: Ngoja nikutumie namba za afisa habari wa wilaya (Misungwi) atakueleza suala hilo.

Chanzo: Mwanahalisi Online
Rubbish kama ni miye angefia mikononi mwangu aisee!! ni ngumi kali za uso mbele ya wanafunzi wangu!! Hawa watu wasijifanye miungu kwa kuchaguliwa na yule ambaye hata kura zetu hana uhalali nasi!!
 
Mkurugenzi wa sasa wa Misungwi ni mbovu sana na hana sifa za uongozi, kama alienda kupangua kila idara ya afya katika hospitali ya wilaya ya Misungwi na kuwapanga madaktari kila department na kuwahamisha ovyo - ovyo utafikiri na yeye ana fani ya udaktari, yaani ni shida, kwa miaka mitano ya huyu jamaa Misungwi haitoboi.
mkung'uteni makonde tuje tuwatetee kwenye mahakama hakuna jinsi!!
 
bahati nzuri ningekuwa mwalimu ningefundsha Mathematics .....ningemgomea kwa kumwambia "mimi ni mwalimu wa Mathematics ..somo ambalo wanasiasa wengi kama wewe mmepata F ..mashule mengi hata ya Private yananisubiria "" siwez kudeki amua unavyotaka ...
 
Chama DHAIFU CWT... cjui hata hao wanakatwa hela hawaamki.. Sion faida yake..

Mkurugenz hana habar nao... Ila huyo mwalimu na yy ni mother f****nta
 
Watoto wetu ndio maana wanaugua sinusitis kwa sababu ya vumbi. Kama shule haina mkakati wa kufanya usafi mwalimu atapiga deki tu.

Mkurugenzi umekata mzizi wa uzembe kwenye maswala ya hygiene.

Watu wana negative perception bila kuangalia concept ya director, kuna watu wanahitaji njia ngumu ndio wajifunze.
akili yako ni sawa na huyo mkurugenzi...kwa hyo mwl huyo ndio mwenye makosa walimu wengine walikuwa sahihi...kama shule ni chafu ilitakiwa awaite walimu wote na kutoa onyo kali wakiwa ofisini hususani kwa mkuu wa shule....sasa hao watoto wanaougua coz of poor hygiene si wangekuwa wanasafisha
 
Vitu vingine vinauma sana..mwalimu nae ikabidi atii tu masikini..
Ndio ajira anayoitegemea angefanyaje sasa?.Hicho alichofanya huyo DED akikubaliki je kama hayo maeneo yana shida ya maji?Kwanini asinge mwita pembeni nakujua shida ni nini?.Sasa ni wakati wenu walimu kujua thamani yenu,ipo siku mtendaji wa kijiji au katibu tarafa atawasimamisha.
 
Mmmmmmmmh!...kwa nini walimu wanadharaulika hivo?why?yaani kila kiongozi mwenye cheo anawaoshea waalimu.
Aisee!..mimi cwezi kubali hivo hataa ww uwe ni nani ktk nchi hii.
 
Rubbish kama ni miye angefia mikononi mwangu aisee!! ni ngumi kali za uso mbele ya wanafunzi wangu!! Hawa watu wasijifanye miungu kwa kuchaguliwa na yule ambaye hata kura zetu hana uhalali nasi!!
Naona umuhimu wa walimu kupitia mafunzo ya judo hapa.


Ngoja hiki kizazi kinachokuja kimefuzu zake JKT, walahi mi hapo tutagawana majengo
 
Mmmmmmmmh!...kwa nini walimu wanadharaulika hivo?why?yaani kila kiongozi mwenye cheo anawaoshea waalimu.
Aisee!..mimi cwezi kubali hivo hataa ww uwe ni nani ktk nchi hii.
Ukienda zahanati nyingi wodi ni chafu sijasikia wahudumu wake wakifanyiwa hivyo
 
Sijakupata! Yaani darasa likiwa chafu mwalimu awekwe sero? Je kwako kukiwa kuchafu?tukuweke korokoroni?

Hiv ni mwanaume, me nilifikiri kadada,, looh, zingepigwa hakika, kwani lokapu mdudu gani bwana, hv watu huwa hawajui job description zao?
 
Na mwalimu nae jamani, mbona anakuwa muoga hivyo? Au ana vyeti feki? Kwani angekataa? Maana najua hata wangetunishiana misuri, mbele ya mahakama haki ingetendeka tu. Halafu bado tunawaza kuja kuwa na kizazi cha free thinkers? Kwa aina hii ya uoga wa walimu? Mungu aiingilie kati.
Utii wa sheria bila shuruti
 
Mbona kawaida sana, angewekwa lokapu sibora kudeki kuliko kulala ndani?, watanzania bana mambo mengine tunayakuza kweli, ni adhabu kama adhabu zingine jamani.
Bora kuwekwa ndani kuliko kudhalilika. Kudeki mbele ya wanafunzi. Mwanaume uogope kuwekwa lokapu wewe bwana vipi? Hili swala uvunjifu wa haki za binadamu eti.
 
Back
Top Bottom