Aliyemkamata mlipua bomu kanisani anena mazito!!

Aliyemkamata mlipua bomu kanisani anena mazito!!

NAPITA

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
5,077
Reaction score
2,249

ALIYEMKIMBIZA hadi kumkamata mtu anayedaiwa kuhusika na kulipua bomu katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti, jijini Arusha Jumapili iliyopita na kuua watu 3 na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa ameibuka.
Kijana huyo ambaye wakati akizungumza na watu mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari jijini Arusha juzi alisahau kutaja jina lake, alisema kuwa shughuli ya kumnasa mtuhumiwa huyo haikuwa lelemama hata kidogo.
Alisema siku ya tukio baada ya bomu hilo kulipuliwa kanisani hapo, yeye alimwona mlipuaji huyo hivyo akaungana na watu wengine kumkimbiza.
"Mtuhumiwa alikuwa akikimbia ujue, sisi tulimkimbiza bila kuogopa kama ana mabomu mengine kwenye mfuko. Alipoona hatukati tamaa, alifika kwenye shamba la miwa akajilaza, lakini mbwa waliokuwa na sisi walitusaidia sana," alisema shujaa huyo.
Aliendelea kusema kuwa walipomdaka mtuhumiwa huyo walimkuta na mfuko wa rambo, walipochungulia ndani yake walishtuka, kumbe alikuwa na mabomu yaliyosalia!

Hata hivyo, alisema yeye na mabomu yake hawakumwachia na dakika chache wananchi wenye hasira kali walifika eneo hilo wakiwa na silaha za jadi wakitaka kumuua ndipo polisi walipofika eneo hilo na kumchukua mtuhumiwa huyo kwenda naye kituoni.
Baadhi ya wananchi waliozungumza na gazeti hili walisema kijana huyo amekuwa staa ghafla, hivyo wakaitaka serikali kumfikiria kwani ameonesha kitendo cha kishujaa.

"Huyu kijana amekuwa staa ghafla aisee, kitendo alichokifanya ni cha kishujaa, si rahisi, serikali ingemfikiria kwa lolote," alisema mtu mmoja aliyejiita Massawe na kuungwa mkono na wenzake.
chanzo:globalpublisher
 
Mmh, nimeamini besaa (pesa) ni sababu ya roho; Hapa inatafutwa promo ya kulazimisha!
Enyi ndugu zangu Wachagga, pesa haitafutwi ki hivyo bana!
 
Duh! kumbe chanzo cha habari ni gazeti la mjasiliamali SHIGON......
 
Haya sasa wale walosema kuwa kijana alimpandisha mtu ndio amelipua kiko wapi? mbona mnapenda kupandikiza chuki kiasi hiki? kiko wapi? huyo ni Ambrose hakanua na Hussein wala nini? mbona babu yenu Pengo jana alisema kuwa alipigiwa simu ya kuelezwa ukweli wa tukio, kinachisikitisha hakuusema ukweli huo ni wazi anafurahia waislamu na wakirisito wanavopigana??? dhamira yake ni nini hasa yeye kama kiongozi wa dini?
 
magazeti ua ki Nyanoko sisomagi


mkiona kuna ishara ya kushindwa mnaparamia magazeti ya unoko, angesema anaitwa hussein ingekuwa jambo jingine, mna kazi kweli kweli by the way, pole sana kwa kuumia Ponda anatesa mitaani JEMBE LA UKWELI , bado uamsho! its just a matter of time ...
 
Nasikia anaitwa Hussein imeshauriwa lisitajwe hili jina kwanza kwasababu upelelezi unaendelea hivyo itavuruga upelelezi
Signature yako nimeipenda........ "Mnang'oa meno ya Tembo ili mukayauze, mnang'oa meno na Kucha za Watanzania wasio na hatia ili iweje?"....... Serikali inalo jibu sahihi maana kila wakati wanatajwa wao kuhusika japo wanajibaraguza wanaelemewa na ukweli halisi kuwa kwa kweli wanahusika mwe! Labda ni dawa ya kubaki madarakani milele.
 
Mleta Uzi na huyo Shigongo wako!

24182.gif
 
Mazito aliyonena yako wapi? Shigongo anatakiwa afike mahali apunguze hawa waandishi wa habari makanjanja wanaoandika title zenye uzito ili auze gazeti wakati ndani hakuna chochote.
Mbona unang'ka bure mkuu, taarifa hii ni ya kusisimua. Kijana kaonyesha ujasiri mkubwa!
 
kwa habari za uhakika ni kuwa aliyerusha bomu hajakamatwa. Yule Ambrosi yeye alikodishwa na mrusha bomu. Alipomfikisha kabla hajashuka kwenye bodaboda ndo akarusha na kukimbia. Ila Ambrosi ndo kakimbizwa kakamatwa baada ya mtuhumiwa kupotea
 
mkiona kuna ishara ya kushindwa mnaparamia magazeti ya unoko, angesema anaitwa hussein ingekuwa jambo jingine, mna kazi kweli kweli by the way, pole sana kwa kuumia Ponda anatesa mitaani JEMBE LA UKWELI , bado uamsho! its just a matter of time ...

Ponda aliwekwa jela na kanisa gani?
 
...Kuna vichwa vya habari ukiviona tu unajua ni Made in Udaku! Yako wapi sasa hayo Mazito hapo? Habari yenyewe inajichanganya.
Upande mmoja 'wananchi' wanaitaka serikali imfikirie Staa huyo, upande mwingine Staa mwenyewe anasema kuwa alikuwa na wenzake wakimfukuza mhusika huyo!!
 
Khaaaa jaman hatukomi tu, ili ni tukio la kisiasa tu tumeshapotezewa concetration bungeni yanapitishwa tu mafungu ya kuzika viongozi watakaokufa kama wapo, posho za lishe za wajumbe wa baraza la katiba wenye HIV, n.k. Mwisho wa siku tutasikia Dodoma imekodishwa na bunge limeridhia as for now each and everyone wako na issue ya Arusha. Tafakarini Great Thinkers
 
Back
Top Bottom