Aliyekuwa mgombea ubunge Igunga kupitia CUF ajiondoa chamani

kiongozi mmoja wa c.u.f
aliwahi kusema kuwa
kuna vyama vitakuja
kama uyoga na vitakufa
kama uyoga.hakuishia
hapo akaendelea kusema kuwa c.u.f ni
kama mti mrefu ambao
mizizi yake imejichimbia
mbalii chini,hivyo upepo
unaweza kuyumbisha tu
mti huwu na sikuung'owa.sasa
utaona kuwa kuna watu
wanatamani waone c.u.f
inakufa na hawo
wanajiita wapinzani
hizo ni ndoto za alinacha,watoke
watakaotoka waliobaki
wataimarisha chama
jamhuri ya mungano ni
baina ya nchi mbili
tanganyika na zanzibar tayari c.u.f iko ndani ya
serikali katika upande
mmoja wa jamhuri
ni hatuwa nzuri.

Natural Death...maneno ya hekima ya mwalimu..huyu sisi wazanzibar na wao watanganyika...itakuja sisi wapemba wao waunguja...na hii itawatafuna mpaka....mwenu siwapendi nyieee,MUNGU NISAMEHE.
 
Huyu mtu anayejiita mpemba mbishi akili zake za kushikiwa,siasa hajui na kujifunza hapendi namkaribisha nimpe darasa ili akili zimkae sawa akirudi humu atakuwa kabadilika lakini hivi atatusumbua huyu mtoto laini laini kama urojo.
 
Dhambi ya kuunda serikali na CCM na kuwasahau wananchi itawatafuna hadi mwisho. Huwezi kuisaliti demokrasia eti ukasema ni uamuzi wa wananchi. Sasa watu wanatembelea magari mazito huku wananchi wanataabika na referendum yao ...teh..teh..teh.

Inawezekana wazo la kuunda serikali ya mseto ilikuwa jema but jamaa wamesahau kuwatetea wananchi kabisa. Wamebaki kutetea policy za serikali ya CCM.
 
msiwe na shaka wanacuf.. hakuna anaehama.. hawa wanaohama tulishafukuza kitambo.. hali ni shwari na uchaguzi wa mwaka 2015 tutachukua dola ya nchi..
so says Mohammad Saeed Al Sahaaf bin Mtatiro..
View attachment 48524
 
Aliyekuwa mgombea ubunge kupitia CUF mwaka 2010 na uchaguzi mdogo Leonard Mhona amerejesha kadi ya CUF;na kujiunga na ADC rasmi licha ya kwamba JULIUS MTATILO alikuwepo huko hivi karibuni ktk ziara ya kuuimarisha CUF

Source Magazeti ya leo
 
Mtatiro yupo Kanda ya ziwa baada ya Tabora, yupo maeneo hayo kushuhudia na kupokea kadi za wanachama wanaokihama chama. Hawatomsahau HR
 
"Huyo Leonard Mahona alikuwa afukuzwe kwenye kikao kijacho"

Mkuu, wamfukuze kwa lipi? Hata hivyo tafsiri yangu ni rahisi sana - amewawahi hivyo hawana cha kufanya zaidi ya kutoa maelezo yanayofanana na hayo uliyotoa!
 
Mkuu, wamfukuze kwa lipi? Hata hivyo tafsiri yangu ni rahisi sana - amewawahi hivyo hawana cha kufanya zaidi ya kutoa maelezo yanayofanana na hayo uliyotoa!
Mkuu, hayo ndiyo maneno atakayosema Mtatiro. Amekuwa akiongea hivyo kila wanachama mashuhuri wanapohama
 
Hata hivyo sina imani kabisa na hiyo ADC wanayo ikimbilia kwa nini wajiegue CUF na wajiunge na ADC.
 
Na bado! Unacheza na magamba. Walikubal kuolewa so shart wakubal mashart ya mume na sasa mume kaamua indirect talaka. Hahahahahahahaha!
 
ladha ya ubaguzi ni tofauti kabisa na ladha nyingine kwasababu huwa haiisha ukibagua utabagua tena na tena na tena na baadae yutabaguliwa tena na tena na tena na mwisho mtakufa kwa dhambi hiyo ya ubaguzi rest kwa amani cuf
 
Bila shaka ADC haitashiriki uchaguzi wa marudio, labda kipate usajili haraka haraka katika siku zilizobaki. Sasa sijui huyu kijana ataamua kuwa pembeni, au atatafuta chama kingine kilichosajiliwa
 
Hizo nafasi kuna watu kibao wanazihitaji ,sasa hamuoni kama akiondoka mmoja mwengine hupata faida !
 
Back
Top Bottom