PostGE2025 Aliyekuwa amepewa kesi ya uhaini adai walitumika kubeba miili ya waliouawa kwenda kuwazika Makaburi ya Kondo

PostGE2025 Aliyekuwa amepewa kesi ya uhaini adai walitumika kubeba miili ya waliouawa kwenda kuwazika Makaburi ya Kondo

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,498
Muna Love ame-share screenshot ya moja ya ndugu wa aliyekuwa amepewa kesi ya uhaini baada ya maandamano ya Oktoba 29 akidai kuwa walitumika kubeba miili ya waliuawa kwenda kuwazika kwenye makaburi ya pamoja huko Kondo ambako hata ripoti ya uchunguzi ya CNN ilieleza uwepo wa makaburi hayo.

"Dada Muna, katoka mdogo wangu lakini naogopa kukwambia walichomfanyia huko ndani. Dada, ukihadithiwa huwezi kusikiliza hadi mwisho. Hatujisikii kuwa katika nchi—hapa tupo kama kisiwa cha mauaji. Nataka nikwambie ili dunia ijue, maana huku tumezibwa midomo; sehemu ya kusema hatuna kabisa."

"Yaani huwezi kuamini, wao ndiyo wametumika kubeba maiti zilizokuwa zinaenda kutupwa, tena unabeba kwa masharti makali. Huruhusiwi kushangaa, ukishangaa unapigwa risa hapo hapo, mnapakia maiti kwenye magari ya taka mkimaliza mnalala juu yake tayari kwa kwenda kupakua makaburini kwa Kondo wamezika watoto wetu bila heshima kama Mbwa"

1764142385560.png
 
Na wengine wamelipwa milioni 2.5 ili watoe ushuhuda wa uongo kuwa walilipwa kuandamana.

Dada Muna katoka mdogo wangu lakini naogopa kukwambia walicho fanyiwa huko ndani dada ukihadisifawa huwezi sikiliza mpaka mwisho hatuna nchi hapa tupo kisiwa Cha mauaji
Nataka nikwambie ili Dunia ijue maana huku tumezibwa midomo pakusemea wenzenu hatuna
Yani huwezi amini wao ndio wametimika kubeba maiti zilizokuwa zinaenda kutupwa tena unabeba kwa mashariti huruhusiwe kushangaa ukishangaa unapigwa risas hapo hapo mnapakiza maiti kwenye magari ya taka mkimaliza mnalala juu yake tayari kwa kwenda kupakua makaburini kwakondo wamezika watoto wetu bila heshima kama mbwa.

Huu ndo utawala tulio nao ndugu zangu aisee hitler alikua na afadhali sijawahi ona watu waovu kusini mwa jangwa la Sahara kama hawa viongozi tulonao hapa kwetu

Imagine vijana wapo walopewa masharti ya kupewa milioni 2.5 ili tu waje watoe ushuhuda wa uongo kuwa walilipwa ili waandamane!View attachment 3507710View attachment 3507711
Screenshot_20251126-101237_Instagram Lite.jpg
 
Yote haya ili mtu mmoja asiye na sifa wala maono abakie madarakani illegally. Halafu mtu anasimama na kuanza kutaja eti magari ya serikali 979 yaliharibiwa. Akiulizwa waandamanaji wangapi waliuwawa anajibu kwa kejeli "hakuna maandamano yasiyo na madhara"

Halafu eti ndiyo wanataka watu wasahau hivi hivi tu. Waridhiane!

20251125_231931.png
 
Muna Love ame-share screenshot ya moja ya ndugu wa aliyekuwa amepewa kesi ya uhaini baada ya maandamano ya Oktoba 29 akidai kuwa walitumika kubeba miili ya waliuawa kwenda kuwazika kwenye makaburi ya pamoja huko Kondo ambako hata ripoti ya CNN ilieleza

Genocide and crime against humanity hii haina namna
 
Bila video habari hii ihesabike kama propaganda tu za kuwasukuma watu wakafe zaidi Disemba 9
Hamna mtu ana andamana ili afe. Hakuna sheria inasema waandamanaji wapigwe risasi
Katiba imeruhusu maandamano , wanaopiga risasi hovyo ni un professional bunch of idiots.

And this time international eyes zote zipo upon nchi hii. Watachagua wenyewe wazidi kujiaharibia or waweke sawa
 
Muna Love ame-share screenshot ya moja ya ndugu wa aliyekuwa amepewa kesi ya uhaini baada ya maandamano ya Oktoba 29 akidai kuwa walitumika kubeba miili ya waliuawa kwenda kuwazika kwenye makaburi ya pamoja huko Kondo ambako hata ripoti ya uchunguzi ya CNN ilieleza uwepo wa makaburi hayo

Halafu wanakana report ya CNN.
Nchi haina kiongozi tuna wahuni.
 
Kwahiyo mkae huko muanze kutumiana meseji zenu za udaku msecreen shot kisha mzilete JF??

JF imekuja kuwa vipi now days,hata kama tuseme ni kweli watu wameuwawa na wanakwenda kuzikwa nani mwenye akili ndogo hivyo za kuweza kuwachukua mahabusu ambao anajua wazi watakuja kwenda uraiani watumike kwenye kazi inayohitaki usiri kama hiyo?kama kazi yenyewe kweli ingekuwa ipo?
 
Hata alieweka ushahidi mmesema ni AI . Uzuri tumeshathibitisha ndugu zetu wako Kondo.
 
Kwahiyo mkae huko muanze kutumiana meseji zenu za udaku msecreen shot kisha mzilete JF??

JF imekuja kuwa vipi now days,hata kama tuseme ni kweli watu wameuwawa na wanakwenda kuzikwa nani mwenye akili ndogo hivyo za kuweza kuwachukua mahabusu ambao anajua wazi watakuja kwenda uraiani watumike kwenye kazi inayohitaki usiri kama hiyo?kama kazi yenyewe kweli ingekuwa ipo?
..mbona kuua hamjafanya siri?
 
Back
Top Bottom