Aliyekufa na kuzikwa zaidi ya miaka 20 iliyopita apatikana ila hawezi kuongea

Man Kitoabu atakueleza kuwa HAYO MAMBO YAPO....

Ukienda kule "kusini" Wala si MAPYA...

Sayansi ya hali ya juu....
 
Nimekutana na hii habari. Mimi bado nina maswali mengi

=====

Kijana aliyefariki tangu mwaka 1994 amepatikana na kukukutana tena na familia yake

Mama yake amemtambua na kujiridhisha kuwa ni mwanaye baada ya kutambua baadhi ya maeneo ya mwili wake

Kijana huyo hana uwezo wa kuzungumza kwa sasa ingawa familia inaamini huenda akaweza kuzungumza tena

Imeelezwa kuwa kijana huyoalichukuliwa msukule na alikuwa akifanyishwa kazi tangu mwaka 1994




Wajuzi wa mambo mnasemaje?
Hayo ndio maendeleo ya kigoma
 
Mama anakumbuka mengi lakini hakumbuki mwaka gani aliompoteza na kumzika mwanawe kipenzi....?????!!!!
Kuna maswali mengi sana kwa sasa nibaki nayo, kifupi kuna ulaghai au uongo au kuna makosa ya utambulisho.
Labda aliyezikwa hakuwa mtoto wa huyo mama.
Au huyu jamaa si mtoto wa huyu mama.

Nahisi manabii feki wa kuombea watu wapo kazini, naendelea kufuatilia video labda kaburi lilifukuliwa na DNA testing zilifanyika kuthibitisha kibaolojia huyu ni mama halali wa huyu jamaa, na Yule aliyezikwa ni nani.
Huyu msukule hazeeki? Mwaka 1994 hadi sasa ni miaka 26 jamaa kama alikuwa na mingapi hwakati anakufa Hadi kumbuke mama yake hadi leo?
Maana bado anaonekana ni mdogo hajafikisha miaka 36.

Jeshi la polisi fanyeni kazi yenu hapo kuna harufu ya jinsi au uzembe wa kitabibu au wa wahudumu wa chumba cha maiti.
 
Sio muda wataanza kujitokeza waliomfufua huyu kijana ili waanze kukusanya sadaka za watu.
 
Kiufupi haya mambo kweli yapo ila na yana utaratibu maalum sio hivi mbele ya makamera,

Huu ni mchezo, narudia tena...Hii ni sinema!!!?

Kafa ana miaka minane mwaka 94 na hadi sasa imepita miaka 26, huyo anabyoonekana ana miaka 34?????

Hapa kuna mganga au mchungaji atacheza muvi ya kumrudisha hali ya kawaida ili kupiga hela za wataomuona anaweza kutatua matatizo.

Ni nani asiekumbuka sinema ya mwaka jana ilichezwa huko iringa mbibi kakutwa juu ya paa la nyumba, baada ya muda akakiri kwamba ni mchezo walicheza na pasta.

Ni nani asiekumbuka yulw kijana aliecheza sinema kaiba gunia la mahindi haliwezi kumtoka kichwani, bjbi akamzingua malipo akaweka kila kitu.wazi.

Haya na wale wakenya walionaswa live na cctv wanalipwa pesa na wakaanza kugaragara kwenye matope wajifanye ndio wezi wa gari lililowekewewa kinga 😂.

Tuweni makini, haipiti wiki kuna pasta au mganga atafanya sinema mbele ya makamera mengi ili kunasa pesa za wenye matatizo.

Hasa hasa wanawake, chonde chonde msinaswe hapa, mna imani nyepesi sana
 
Wale wahenga wenzangu nani anamkumbuka pawa mabula? Nimekumbuka alivyokua anageuza makaratasi kuwa pesa
Wewe sasa unatuangusha sisi wahenga, Power Mabula alikuwa naonesha michezo ya kutumia nguvu kama kuzuia gari au kuvunjiwa matofari kifuani, alikuwepo pia mwingine akiitwa Power Bernado, hao wa mazingaombwe walikuwa wengine,
 
Sio muda wataanza kujitokeza waliomfufua huyu kijana ili waanze kukusanya sadaka za watu.
Naona kama vile unatukana wengi kwa kutujumlisha na sisi, kutoa sadaka kanisani inakuwa nongwa, mbona kwa waganga wa kienyeji mkienda mnatoa sadaka tena kwa masharti makali ??!!
 
Wewe sasa unatuangusha sisi wahenga, Power Mabula alikuwa naonesha michezo ya kutumia nguvu kama kuzuia gari au kuvunjiwa matofari kifuani, alikuwepo pia mwingine akiitwa Power Bernado, hao wa mazingaombwe walikuwa wengine,
Nimechanganya madesa😁😁😁 mambo ya zamani sana hayo. Mambo ya darasa la kwanzaB
 
Back
Top Bottom