Kwanini niliamua kutozungumza na mtu yeyote duniani kwa miaka 17 na kutopanda gari kwa miaka 22

client3

JF-Expert Member
Aug 6, 2007
2,332
3,152
Kutoka kurasa za BBC Swahili.

Mmarekani John Francis alifanya uamuzi wa kubadilisha maisha akiwa kijana mwenye msimamo: aliamua kuacha kuzungumza.

Alikuwa kimya hajazungumza kwa miaka 17 kabla ya kugundua kwamba alikuwa na jambo ambalo alihitaji kulisema.

Yote haya yalianza na msiba. Ajali kati ya meli mbili za mafuta mnamo 1971 ambazo zilisababisha uchafuzi mkubwa wa mafuta katika Ghuba ya San Francisco, ambazo zaidi ya galoni nusu milioni za mafuta ghafi zilisambaa majini.

"Nilisikia juu ya taarifa hiyo na nilitaka kushuhudia, kwa hivyo niliendesha gari hadi San Francisco kutoka mji wangu mdogo wa Inverness. Niliona watu kwenye ufuo katika vikundi vidogo wakisafisha.

Walikuwa wanaingia majini na kutoka na ndege wa baharini - pelicans, samaki, shakwe na korongo - zilizolowa kwa mafuta. ".

Kuona ndege na watu wakijaribu kuwaokoa kulimshtua sana hadi akahisi ni lazima afanye jambo.

"Niliwaza, 'Nisiendeshe magari tena, na niliamua kwamba ndivyo ningefanya."
Kumbuka hii ilikuwa kitambo katika miaka ya 1970 huko California. Kila mtu alikuwa akiendesha gari kila mahali, hivyo kuacha kabisa kuendesha magari ilikuwa hatua ya ujasiri.

John alijikuta akitembea peke yake. "Nilifikiri kila mtu angetembea nami, kwa sababu umwagikaji wa mafuta ulidhuru watu sana wakasema mambo kama 'Nitaacha kuendesha gari.' Kwa hivyo haikuwa ajabu kwangu kusema. "Hata hivyo, nilipokubali, walisema, 'Unafanya nini hiki? Ni wazimu! Hakuna kitakachobadilika.'

"Hata mama yangu aliniambia, mimi ni mkaidi, lakini niliendelea kutembea." “Nikiwa nafanya hivyo kitu kilianza kutokea, nikaanza kufurahia, nikaanza kufurahia kuishi pale nilipokuwa nikiishi na kutopanda gari langu na kuingia mjini au kununua vitu madukani... nikawa sehemu ya mahali nilipoishi".

Uamuzi wake wake wa kuachana na magari ulizua utata. "Watu walinipinga na kubishana nami kuhusu kama mtu mmoja anaweza kuleta mabadiliko."
Madereva walimkosoa kwa kuwafanya wajisikie vibaya au kutaka wajisikie vibaya, na John akajitetea ... hadi akachoka, aliona kama anajiambia mwenyewe, watu hawasikii, hawataki kuacha kuendesha magari.

Zawadi​

Zawadi Katika mkesha wa siku yake ya kuzaliwa ya 27, John alikuwa akisoma kitabu kimoja "The Hobbit" cha JRR Tolkien na akapata wazo. Wazo lenyewe ni kukaa kimya, asibishane na watu, asizungumze, kwa sababu akizungumza hakuna anayemsikiliza hoja zake.
tHE hOBBIT

"Kwa hivyo nilivyoamka asubuhi kesho yake nilikuwa kimya." "Wakati wa kiapo hicho cha saa 24 cha ukimya, niligundua kuwa hapo kabla sikuwa nikimsikiliza mtu yeyote, na kwa kuwa sasa nilikuwa kimya, nilikuwa nikisikiliza, na naweza kujifunza kitu."

"Niliwaza, 'Nitanyamaza kesho yake,' ambayo iligeuka kuwa siku nyingine baada ya nyingine, wiki moja baada ya nyingine."

Familia na Marafiki zake walikuwa wanamuelewa?​

"Mpenzi wangu alifurahia na hakuwa na shida katika siku za mwanzoni, lakini baada ya wiki moja au zaidi alitaka kujua ni lini hilo litakoma (na nitaanza kuzungumza na watu pamoja na yeye). Na watu wengine wengi walifikiri nilikuwa wazimu kidogo."

"Nilijisikia vizuri kutozungumza kwa sababu nilitambua kwamba nilikuwa nikijifunza."
"Kwa wiki chache za kwanza kulikuwa na mazungumzo mengi akilini mwangu kuhusu kile nilichopaswa kusema na wakati ningeanza kuzungumza hadi hatimaye nikafikia hitimisho kwamba ningeendelea kwa mwaka mmoja."
Aliendelea kukaa kimya na kutembea kwa miguu tena na tena.

"Na mara tu nilipofanya uamuzi, kila kitu kililegea na nikatulia kimya, na kimya kikatulia ndani yangu." Huo ni msemo wa kupendeza: "Kimya kilitulia juu yangu."
John Francis

Siku yake ya kuzaliwa ilipofika baada ya mwaka kukatika, alifikiria tena uamuzi wake na kuamua kukaa kimya kwa mwaka mwingine ... ukaja mwingine na mwingine, na mwingine. Miaka 17 ilipita, ambapo alichokuwa akifanya katika miaka yote hiyo ni "kufikiria, kutembea kutoka California hadi Oregon na kwenda nyikani."

Pia alirudi kwenye elimu, kupata shahada, ingawa ni kimya kimya. "Nakumbuka nilienda kwenye ofisi ya msajili (katika Chuo Kikuu cha Oregon Kusini huko Ashland) na kujaribu kumfanya aelewe kwamba sizungumzi na kwamba nilitaka kusoma."

“Nikakaa mbele yake na kuinamisha kichwa kisha nikaunganisha viganja vyangu na kuvifungua kwa ishara ya kitabu na kujifanya ninakisoma" . John alirudia kufanya hivyo mpaka akaeleweka.
"Kwa hiyo unataka kujiunga na masomo?" Alisema msajili "Niliitikia kwa kichwa."

Kuanza kuzungumza​

John Francis

John alifanikiwa kumaliza shahada yake ya pili(uzamili) akifanya utafiti wake uliojumuisha masuala ya mabadiliko, vita, amani na mazingira, ilikuwa mwaka 1986.
Hapo Milango ikaanza kufunguka. Aliombwa kuishauri serikali ya Marekani kuhusu umwagikaji wa mafuta na kuandika kanuni kwa ajili yao. Umoja wa Mataifa walimtaka awe balozi wa mazingira.

"Inashangaza sana". Majina matatu na karibu miongo miwili baadaye, John alihisi ana jambo la kusema na akaweka tarehe katika kumbukumbu zake ya kuanza kuzungumza tena: ilikuwa Januari 2, 1990.
"Nilichagua Siku hii ya kimataifa, kwa sababu nilitaka kuzungumza juu ya mazingira, jambo ambalo kwangu lilikuwa limetoka kwa kile tunachofikiria kijadi - mabadiliko ya hali ya hewa, umwagikaji wa mafuta, uchafuzi wa mazingira na mambo kama hayo - kujumuisha na jinsi tunavyochukuliana.

"Fikiria kwa mfano jinsi tunavyochafua maji bila kufikiria watu anaoishi chini ya mto ambao wanapaswa kuyasafisha."
Uchafuzi wa mazingira hasa maji, ndio ujumbe ambao John alitaka kueneza duniani na kwamba alikuwa tayari kuvunja ukimya wake wa miaka 17.

Alijisikiaje kwa mara ya kwanza alipoanza kuzungumza?​

John Francis

Maelezo ya picha,
John Francis akipigia ala ya muziki aliyoitumia siku alipoanza kusema neno la kwanza baada ya miaka 17
"Nilianza kuzungumza huko Washington DC, kwenye hoteli ambayo ilijitolea kuniandalia tukio dogo, na niliwaalika baadhi ya marafiki na familia yangu.

Baadhi ya vyombo vya habari pia vilikuja - National Geographic, Los Angeles Times. "Nilicheza kidogo kwenye banjo (chombo mfano wa gitaa) kisha nikasema, 'Asante kwa kuwa hapa.' Na mama yangu akaruka juu kwa furaha kutoka kwenye kiti chake na kusema, 'Haleluya, Johnny anazungumza!

“Lakini kwa kuwa nilikuwa sijaisikia sauti yangu kwa muda mrefu sikuielewa kabisa ilikuwa inatoka wapi, nilitazama nyuma yangu ili nione ni nani alikuwa akisema ninachowaza. "Nilishtuka sana na kuanza kucheka na kumuona baba yangu akinitazama akiwaza, 'Ndiyo, ni kichaa kwelikweli.'
Huo ukawa mwanzo wa kuongea kwake na kuanza angalau kurejea maisha ya kawaida, ingawa anatumia magari lakini bado anatembea.

"Bado natembea. Kwa kweli, kuanzia Agosti nitakuwa natembea Afrika. Na pia wakati mwingine siongei siku nzima. Kwa vyovyote vile miaka 17 ya ukimya na miaka 22 ya kutembea haiwezi kupotea hivi hivi."

Alipuliza Je, ungewashauri wengine wafanye hivyo kwa maana ya kutozungumza? alijibu "Ningeshauri kusikilizana."
 
Hili ni tatizo
 
Back
Top Bottom