Aliyekiri kumuua mpenzi wake aachiwa huru

Sheria sio soga za mtaani wewe, ..kinyume chake pia ni kua Kama mtuhumiwa angekataa na ushahidi upo usio na Shaka Basi angefungwa....hivo jaji hafuati mawazo binafsi..anafuata sheria na mwenendo wa kesi

Ni nani shahidi wa kweli kuliko alietenda kitendo na akikiri akiwa na akili timamu kwa vipimo vyote?
Kama ushahidi utosheleza kumfunga au kumuachia huru mtuhumiwa maelezo yake huhitajiwa kwa msingi upi?
Hapo hakuna sheria wala nini pananuka rushwa tu
 
Ana subiri nini kukimbia nchi ... Sifurahishiwi na kitendo alicho kifanya no kitendo cha kinyama na cha ukatili mkubwa hakifai kufanywa kwa binaadamu wala wanyama

Ila kama Mimi ningekuwa ndiye yeye baada ya kuachiwa lazima nikimbie nchi
Hat akikimbia nchi bado kuna uwezekano mkubwa huko aendako ataua tena. Ndio maana zamani ilikuwa ukiua lazima wakuue maana wanajua lazima ile damu itakusumbua na utaua tena
 
Ni nani shahidi wa kweli kuliko alietenda kitendo na akikiri akiwa na akili timamu kwa vipimo vyote?
Kama ushahidi utosheleza kumfunga au kumuachia huru mtuhumiwa maelezo yake huhitajiwa kwa msingi upi?
Hapo hakuna sheria wala nini pananuka rushwa tu
Ahaaa Aya !
 
Nimeipenda sana hii narudia "ni vyema mara 1mln kumuachia mtuhumiwa aliyetenda kosa kuliko kumfunga asiyetenda kosa"

Jaji ameonesha ukomavu wa sheria siyo tu ionekane bali pia itendeke
 
Nakumbuka kesi ya mwangosi kule iringa. Yule askari alifungwa kifungo cha maisha lakini baadae akakata rufaa na akashtakiwa kwa kosa la kuua bila kukusudia. Hoja zake zilikua ni yeye hajatokea nyumbani kwake na silaha kua anaenda kuua, silaha alipewa ofisi kwake.
Hiyo silaha iliyotumika kufanya mauaji yeye hajajichagulia bali alifanya kupewa na mkuu wake wa kazi.
Pia siku ya tukio hakujua kama mwangosi atakua eneo la tukio. Lakini hapo kabla hajawahi kumfahamu mwangosi .
Nadhani jamaa atakua keshatoka jela.
 
Duuh msala sanaa...!
 
Back
Top Bottom