Aliyejeruhiwa TEGETA kwa kupigwa risasi afariki dunia

Watu8

Platinum Member
Feb 19, 2010
60,653
2,000
Wajameni habari zenu.
Nimesikia habari za kufariki kwa yule ndugu aliyepigwa risasi na polisi kule Tegeta wakati wa operesheni ya Polisi kuondoa magari yanayoegeshwa pembezoni mwa barabara, je kuna ukweli wowote?

Aliejeruhiwa ktk vurugu zilizotokea kule Tegeta amefariki dunia.Polisi walikuwa wakiyaondosha malori yaliyokuwa yameegeshwa pembezoni mwa barabara kinyume na sheria.Polisi walifyatua risasi iliyompata raia mmoja aliekuwa akijinunulia godoro katika maduka yaliokuwa karibu na eneo la tukio.

Habari zaidi ni katika gazeti la Majira.

attachment.php

attachment.php
 
Attachments

  • IMG_0007.jpg
    IMG_0007.jpg
    158.6 KB · Views: 390
  • IMG_0014.jpg
    IMG_0014.jpg
    209.5 KB · Views: 397

Ciril

JF-Expert Member
Jan 10, 2011
8,562
2,000
Aliejeruhiwa ktk vurugu zilizotokea kule Tegeta amefariki dunia.Polisi walikuwa wakiyaondosha malori yaliyokuwa yameegeshwa pembezoni mwa barabara kinyume na sheria.Polisi walifyatua risasi iliyompata raia mmoja aliekuwa akijinunulia godoro katika maduka yaliokuwa karibu na eneo la tukio.

Habari zaidi ni katika gazeti la Majira.
 
Chupaku

JF-Expert Member
Oct 15, 2008
1,091
1,500
Hii habari niliileta hapa jamvini jana, Mods wakanipotezea...kijana wa watu amekufa, alikuwa anauza duka na ana miaka 15. Hakupigwa risasi ila ni bomu. Poor boy! Poleni wafiwa wote.
 
ligendayika

JF-Expert Member
Aug 31, 2012
1,183
1,250
mkuu nawe huna taarifa duh umetukatya steam make tulitaka kujua kumbe nawe unauliza swali lilelile. sawa mkuu
 
Rapherl

JF-Expert Member
Jun 20, 2012
3,505
2,000
Hili ndo tatizo la kuajiri Askari wengi bila kuwa na mpango mzuri wa mafunzo haiwezekani Kuruta akae miezi mitatu chuoni alafu aje uraiani uniambie kashahitimu!,hakuna mtu anaye jifunza silaha miezi mitatu.lazima utakuwa muuaji tu,Angalia asilimia kubwa ya Askari wanaoua ni hawa ambao wametoka depo miaka ya karibuni
 
Ciril

JF-Expert Member
Jan 10, 2011
8,562
2,000
Hii habari niliileta hapa jamvini jana, Mods wakanipotezea...kijana wa watu amekufa, alikuwa anauza duka na ana miaka 15. Hakupigwa risasi ila ni bomu. Poor boy! Poleni wafiwa wote.

Hivi wananchi kwa nini tusifikiri jinsi ya kufanya ili kukomesha tabia hii ambayo kwa sasa hapa nchini kwetu imeota mizizi?Tukikaa kimya watatumaliza hawa watu,kwa matendo yao ni kama vile wapo juu ya sheria.Ni nani yupo nyuma ya hawa polisi?Mbona hatuoni viongozi wa Serikali wakilivalia njuga kwa kuwachukulia hatua kali?Aliyoyafanya Nchimbi ktk sakata la Mwangosi ni kama alikuwa anafunika kombe mwanaharamu apite,tume haikusaidia chochote zaidi ya kutafuna pesa zetu wananchi.
 
Zimamoto

JF-Expert Member
Mar 28, 2012
464
195

Hivi kwa vitendo kama hivi, inawezekanaje kwa CCM na serikali yake kuonyesha sura zao mbele ya umma? Na sisi wananchi tunakuwa wa kwanza kujitokeza na kuwashabikia CCM. Hatuoni au hatusikii haya mambo? Kwa kujitokeza kuwashabikia tunakuwa ni sehemu ya kukuza tatizo.
 
HorsePower

JF-Expert Member
Aug 22, 2008
3,612
2,000
Sasa hivi imekuwa kana kwamba ni hali ya kawaida kwa Jeshi letu la Polisi kuhusika kwa namna moja au nyingine ktk kuyapoteza maisha ya Watanzania wasio na hatia. Hali hii ikiendelea tunakoelekea kutakuwa kubaya sana, ni lazima kitu fulani kifanyike ....! Ni vyema kufanyike maamuzi magumu ndani ya uongozi wa Jeshi la Polisi kulinda maisha ya watanzania wasio na hatia
 
zema21

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
619
225
Watanzania huwa tunaishiaga kulalamika tu ndio maana hao jamaa wanajua ni kelele za chura! hivi haya mauaji ya raia wasiokuwa na hatia kila siku tunayachekelea na kuishia kuandika tu hapa itatusaidia nini? Angalia wenzetu Tunisia yule aliyejilipua kwa petrol kutokana na kusumbuliwa na askari kilitokea nini?
Wenzetu wamakonde wa hapa msumbiji mkate ulipanda bei watu wakaingia barabarani! hv sisi hatuoni kuwa maisha ya mtanzania yana thamani kubwa kuliko mkate? kwanini tusiende kuwaambia polisi tumechoka na mauaji ya raia wasio na hatia? kwanini tusiwambie Polisi juu ya habari ya mwandishi wa Tanzania daima kupigwa risasi akiwa amelala na mke wake kitendo hicho hakikubaliki? hv nane aliyewapa Polisi mamlaka ya kupiga risasi watu kwa kusingizia umehisiwa jambazi?
 
Domy

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
4,700
2,000
MWENYEZI MUNGU akupumzishe PEMA PEPONI kamanda! Na AWALAANI wote wanaoongoza serikali dhalimu na kutetea udhalimu.
 
Lyimo

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,824
1,225
Tutegemee single nyingine ya polisi kujitetea. Tumekuwa kimya kila wanapotoa porojo zao ndiyo maana hawafanyi jitihada zao kukomesha mauaji holela ya wananchi wasio na hatia. Hivi vitu vizito ama vyenye ncha Kali vitatumaliza hivihivi kimzahamzaha.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom